Papa:Tarehe 8 Juni ni dakika moja ya kuomba kukomesha vita duniani!
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Amani nchini Ukraine, Zuppi alitumwa na Papa huko Kyiv mnamo 5 na 6 Juni 2023 kwa Mwaliko mpya wa kuombea amani duniani. Papa Fransisko alihutubia kabla ya kuhitimisha katekesi yake katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican huko , akiomba kila mtu kuomba maelewano kati ya watu. Papa ameomba kwa hiyo sala hasa kwa ajili ya Ukraine, ambapo ujumbe wa Kardinali Matteo Zuppi ulihitimishwa tarehe 6 Juni uliotumwa kusikiliza kwa kina mamlaka ya Ukraine juu ya njia zinazowezekana za kufikia amani ya haki na kuunga mkono ishara za kibinadamu zinazochangia kupunguza mvutano”, kama ilivyoelezwa katika taarifa kutoka mjini Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko kwa maana hiyo ameonesha mawazo yake kwa nchi ya Ulaya Mashariki kwa zaidi ya mwaka mmoja iliyojaribiwa na vita pia kwa maneno aliyolekezwa kwa waamini wanaozungumza Kipoland, ambao alipendekeza, kwa mara nyingine tena, kudumu katika upendo wa Kikristo na kuunga mkono Waukraine na kuhitimishwa kwa , salamu yake kwa mahujaji wa Italia, akiwaomba waamini wa imani mbalimbali na madhehebu ya kidini, kujiunga, Alhamisi tarehe 8 Juni katika mpango wa Chama cha matendo KatolikiKimataifa kwa Dakika ya Amani kwa Ukraine, Nchi Takatifu na dunia nzima. Kwa hiyo saa saba kamili Mtanadao wa Kimataifa wa matendo kikatoliki inapendekeza kwamba wamini wa maungamo na dini mbalimbali wakusanyike katika sala, wakitoa muda wa daskika moja. Tunakaribisha mwaliko huu, tukiombea mwisho wa vita duniani na hasa kwa Ukraine mpendwa na anayeteswa”.
Ni mpango rahisi" kwa mujibu wa msemaji wa Jukwaa la Kimataifa la Matendo ya Kikatoliki, likipendekeza kwamba kila mtu aeneze ndani ya familia, kati ya marafiki, katika vyama, mahali pa kusoma na kazini. Pendekezo ni kusimama kwa dakika moja ili kuomba au kutoa mawazo kwa ajili ya amani”, tarehe 8 Juni saa saba katika nchi na mahali popote walipo. “A minute for peace” ilizinduliwa kwa mara ya kwanza tarehe 6 Juni, 2014, kwa kuunga mkono “Ombi la Amani”lililohamaishwa na Papa Francisko, ambayo ingefanyika siku mbili baadaye katika Bustani ya Vatikani pamoja na rais wa Israeli wa wakati huo Simon Peres na rais wa Mamlaka ya Palestina Maḥmūd ʿAbbas, na ambapo patriki Konstantinople Bartholomew I alikuwapo. Ili kukuza mpango wa maombi, Jukwaa la Kimataifa la Matendo ya Kikatoliki lilizindua hashtag #unminutoporlapaz kwenye mitandao ya kijamii na kufanya kupatikana kwenye tovuti yake mfululizo wa nyenzo na mwongozo mdogo wa kukusanyika na kusali na tarehe 10 Juni inaalika mkutano mfupi wa maombi mtandaoni na baadhi ya marafiki kutoka nchi zenye migogoro.