Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko anaendelea vizuri katika Hospitali ya A.Gemelli kwa mujibu wa Daktari na msemaji wa vyombo vya habari Vatican. Baba Mtakatifu Francisko anaendelea vizuri katika Hospitali ya A.Gemelli kwa mujibu wa Daktari na msemaji wa vyombo vya habari Vatican. 

Papa anaendelea vizuri Hospitalini Gemelli

Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyombo vya habari Vatican,kuhusu hali ya Baba Mtakatifu mara baada upasuaji wa ukuta wa utumbo kwa kiungo bandia,amelala vizuri katika hospitali ya Gemelli.Maombi na matashi mema ya kupona haraka yanaendelea kufika kutoka ulimwenguni kote.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Papa Francisko anaendelea vizuri na Dominika tarehe  11 Juni 2023 atasali Sala ya Malaika wa Bwana kwa faragha. Na wakati huo kituo cha habari cha Agostino Gemelli, Daktari Sergio Alfieri ambaye alimfanyia upasuaji Papa Francisko ameelezea kuwa: "Kila kitu kinakwenda vizuri sana, ili kuepusha juhudi tulimwomba Baba Mtakatifu atupatie busara na akakubali ushauri wetu: kesho atasali sala ya Malaika wa Bwana kwa faragha”.

Taarifa za Papa Francisko hospitalini

Kutoka kwa Telegramu ya saa (1.06) jioni kwa hiyo  Papa Francisko alitumia siku yake kati ya mapumziko na shughuli, na mchana alipokea Ekaristi. Taarifa zaidi Dominika tarehe 11 Juni 2023. Msemaji wa wa Ofisi ya Vyombo vya Habari Vatican, alitangaza kwamba (saa 6.39): “Timu ya Wafanyakazi wa matibabu walifahamisha kwamba ufuatiliaji kwa ajili ya Papa Francisko baada ya upasuaji unaendelea kuwa ya kawaida.

Dripu zote tayari zilisitishwa katika siku za hivi karibuni na Baba Mtakatifu analishwa kwa chakula nusu laini. Hana homa na Vipimo vya damu baada ya upasuaji na X-ray ya kifua ni nzuri. Baba Mtakatifu anafuatilia kwa makini maelekezi na hasa kwa kulenga kupunguza nguvu za ukuta wa tumbo, ili kuruhusu matundu bandia yaliyopandikizwa na ukarabati wa kipande cha misuli kuweza kushika na kupona kikamilifu.

Sala ya Malaika wa Bwana

Kwa ushauri wa timu ya wahudumu wa afya na msaidizi wake binafasi wa afya, na kama inavyoweza kubainishwa kutokana na nyakati za kawaida za kupona baada ya upasuaji katika operesheni za aina hii, Baba Mtakatifu Francisko Dominika atasali sala ya Malaika wa Bwana faraghani, akiunganisha kiroho, kwa upendo na shukrani, kwa waamini ambao watataka kusindikizana naye, popote walipo”.

Na wakati Telegreamu ya saa 3.23 asubuhi 10 Juni, ilieleza kuwa alilala vizuri na Habari zaidi zitaelezwa baadaye.

Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu Francisko pia alitumia usiku kulala vizuri katika siku ya tatu akiwa Hospitali ya A. Gemelli  mara baada ya operesheni ya mnamo tarehe 7 Juni 2023  ya laparotomy na upasuaji wa plastiki wa ukuta wa tumbo kwa kutumia viungo bandia. Kwa mujibu wa Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican imewasilisha, katika sasisho la kawaida la asubuhi tarehe 10 Juni 2023 , ikieleza kwamba taarifa zaidi zitatolewa wakati wa mchana.

Tarehe 9 Juni 2023 jioni tena Ofisi ya Vyombo vya Habari Vatican  ilitoa barua kutoka kwa wafanyakazi wa matibabu kufuatia afya ya kuendelea kupona Papa ambapo ilisisitizwa kuwa "shughuli za matibababu baada ya upasuaji kwa Papa Francisko zinaendelea kuwa ya kawaida na ndani ya ukawaida. Vigezo vya haemodynamic ni kawaida”, madaktari walielezea, na kwamba Papa: “amesimamisha dripu na kuendelea kujilisha chakula kilaini.”


Alasiri, tarehe 9 Juni 2023   Papa Francisko hata hivyo aliweza "kusali na  kujitolea kwa shughuli na kupokea Ekaristi jioni.” Taarifa iliyotolewa wakati huo pia ilifahamisha kwamba Papa Francisko “aliguswa na jumbe mwingi anaoendelea kupoke; kwa namna ya pekee alipenda kuelekeza mawazo yake na shukrani zake kwa watoto waliolazwa hospitalini kwa sasa, kwa mapenzi na upendo anaoupokea kupitia michoro yao na jumbe zao.

Vyombo vya habari vimepiga kambi kufuatilia moja kwa moja taarifa za afya ya Papa
Vyombo vya habari vimepiga kambi kufuatilia moja kwa moja taarifa za afya ya Papa

Kwa watoto, pamoja na wafanyakazi wa matibabu, wauguzi, wafanyakazi wa kijamii na kiafya na wasaidizi wa kiroho ambao hugusa maumivu kwa mikono yao kila siku, kupunguza uzito wake Papa Francisko alielezea shukrani zake kwa ukaribu wao na sala.

10 June 2023, 10:52