Tafuta

Papa bado yuko Hopstalini Genelli na siku ya pili amelala vizuri wakati huo huo matashi mema kwa Papa ili apone hara tanaendelea na Papa anawashukuru wote. Papa bado yuko Hopstalini Genelli na siku ya pili amelala vizuri wakati huo huo matashi mema kwa Papa ili apone hara tanaendelea na Papa anawashukuru wote. 

Papa amelala vizuri kwa siku ya II Hospitalini Gemelli na alikaa kwenye kiti na kusoma magazeti

Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican ilifahamisha mapema tarehe 9 Juni 2023 kwamba Papa anaendelea kupata nafuu na utulivu kwa siku ya pili baada ya upasuaji wa ukuta wa tumbo.Na baada ya kifungua kinywa Papa alitumia muda wake wa kukaa katika kiti akijisomea magazeti na kazi yake.Ujumbe wa matashi mema unaendelea kufika.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Ijumaa asubuhi tarehe 9 Juni 2023, Ofisi ya Vyombo vya Habari Vatican imetangaza kuwa: "Kwa Papa Francisko ulikuwa usiku mwingine mtulivu na uliotumika vizuri. Na wakati huohuo Ofisi ya Vyombo vya Habari Vatican ikasisitiza  kwamba taarifa zaidi zitatolewa wakati wa siku. Na wakati wa alasiri kwa mujibu wa taarifa  za Vyombo vya habari inaeleza kuwa "Timu ya madaktari wa matibabu inaarifu kwamba hali halisi ya vipimo vinaendelea kuboreshwa na hatua ya baada ya upasuaji ni ya kawaida. Baada ya kifungua kinywa, Baba Mtakatifu alianza kuamka kwa kutumia sehemu  kubwa ya wakati wa  asubuhi akiwa amekaa kwenye kiti Hii ilimruhusu kusoma magazeti na kuendelea na kazi yake ya awali."

Siku ya I ya Papa kulala Hospitalini

Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi 8 Juni 2023 siku moja baada ya kupata operesheni, alitumia siku ya kupumzika na kula chakula cha maji. Viungo ‘haemodynamic ‘na mfumo wa kupumua ni imara. Hatua zote baada ya upasuaji ni za kawaida” kwa mujibu wa madaktari wamesema. Ikumbukwe kuwa Timu ya madaktari  wa matibabu walikuwa wamethibitisha  juu ya hali ya kiafya ya Papa kwamba, mapema alasiri tarehe 7 Juni, alifanyiwa upasuaji wa laparotomy na plastiki ya ukuta wa tumbo kwa kutumia viungo bandia katika hospitali ya Gemelli. Na walifafanua jinsi gani waliweza kufanya operesheni hiyo na sababu za kufanya hivyo hasa maumivu makali kutokana na makovu ya ndani baada ya upasuaji alio wahi kuupata Papa siku za nyumba katika maisha yake.

Michoro mbali mbali kwa heshima ya Papa
Michoro mbali mbali kwa heshima ya Papa

Kupokea Ekaristi

Na katika maelezo yaliyotolewa na Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican jioni pia tunasoma kwamba: “Mchana wa leo, tarehe 8 Juni, katika fursa ya  Maadhimisho ya (Corpus Domini) Mwili na Damu ya Yesu Papa alipokea Ekaristi.” Kama walivyokuwa wametaarifa mapema asubuhi,  vilevile ilikuwa mara kwa mara timu ya matibabu karibu saa sita mchana ambao waliripoti maelezo juu ya hali ya afya ya Papa katika siku yake ya kwanza baada ya upasuaji.  Taarifa kwa vyombo vya habari ilizungumza juu ya usiku wa kwanza ulivyotumiwa kulala kwa amani, kwa hali nzuri kwa  ujumla ya Papa Francisko kupumua kwa uangalifu na kwa hiari. “Vipimo vya  udhibiti wa kawaida ni vizuri,” madaktari walisema, na kuwa “kwa siku nzima atazingatia mapumziko muhimu baada ya upasuaji”. Na ndivyo ilivyokuwa, ripoti kama ilivyothibitishwa na taarifa ya pili kwa vyombo vya habari jioni.

Mishumaa ikiwaka ishara ya kumuopea Papa Francisko na maua
Mishumaa ikiwaka ishara ya kumuopea Papa Francisko na maua

Salamu na matashi mema ili apone haraka

Kwa siku nzima kama ilivyokuwa alasiri ya tarehe 7 Juni 2023,  kulikuwa na utiririshaji wa ujumbe  uliotoka  sehemu mbali mbali za dunia: watoto wagonjwa wa Hospitali ya Kipapa  ya Gesu Bambino, ambao walichora picha na kumtumia kupitia Tweeter,  Jimbo la Roma na Mabaraza ya Maaskofu duniani, vyama na harakati za kikanisa wamemwahakikishia sala, upendo na mshikamano na pia Rais Sergio Mattarella, Italia.

Simu kwa Mama Miguel Angel, mtoto aliyembatiza

Baba Mtakatifu Francisko alipendelea  kumpigia simu mwanamke mmoja, ambaye alikutana naye tarehe 31 Machi 2023 wakati wa kulazwa hospitalini kwa ugonjwa wa bronchitis, katika wodi ya Saratani ya watoto. Katika tukio hilo, Papa alikuwa amembatiza mtoto mdogo wa siku chache, aliyelazwa hospitalini kufuatia kuanguka vibaya kutoka kiti cha juu. Hata hivyo Moto Miguel Angel hakuwa na ugonjwa mbaya ni sababu yya kuanguka  tu na kupoteza fahamu. Mama huyo kijana kwa hiyo alhamisi tarehe 8 Juni  2023  amemtumia salamu Papa za matashi mema ili aweze kupona haraka kutoka kwa familia yake. Mchana walizungumza kwenye simu: utani kidogo, salamu, maneno ya upendo kwa mtoto ambaye amepita mtihani mkubwa.

Papa anaendelea vizuri Hospitalini
 Sasisho la habari saa 10.30 jioni
09 June 2023, 10:02