Tafuta

Kwa mujibu wa ombi la Papa,Kardinali Zuppi atatimiza utume wake huko Kyiv nchini Ukraine tarehe 5 na 6 Juni katika kutafuta njia za kufikia amani. Kwa mujibu wa ombi la Papa,Kardinali Zuppi atatimiza utume wake huko Kyiv nchini Ukraine tarehe 5 na 6 Juni katika kutafuta njia za kufikia amani.  (ANSA)

Juni 5-6,Kard.Zuppi atakuwa mjini Kyiv,Ukraine kwa utume

Kuanzia tarehe 5-6 Juni 2023,Kardinali Zuppi atatimiza ziara yake huko Kyiv kama ilivyokuwa tayari imetangazwa kwa ombi la Baba Mtakatifu.“Lengo msingi ni kusikiliza kwa namna ya kina Mamlaka ya Ukraine uwezekano wa kufikia njia za amani na kusaidia ishara za kibinadamu ambazo zinachangia kupungunza mivutano.”

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Kufuatia na kile kilichokuwa kimekwisha tangazwa mwanzo na Vatican, taarifa nyingine imetolewa  kuwa katika siku ya tarehe 5 na 6 Juni, 2023, Kardinali Matteo Zuppi, Askofu Mkuu wa Bologna na Rais wa Baraza la Maaskofu katoliki nchini Italia (CEI) atatimiza ziara yake huko jijini Kyiv nchini Ukraine kufuatia na mwaliko alioombwa na  Baba Mtakatifu Francisko hivi karibuni.

Huu ni mpango ulioanzishwa ambao ni wenye lengo kuu la kutaka kusikiliza kwa namna ya kina Mamlaka za Ukraine katika kutafuta haraka iwezekanavyo njia za kufikia hali ya amani na kisaidia ishara za kibinadamu ambazo zinachangia kupunguza mivutano.

Utume wa Kardinali Zuppi huko Kyiv nchini Ukraine aliotumwa na Papa
05 June 2023, 11:06