Tafuta

Kardinali zuppi ameteuliwa na Papa kuwa mjumbe wa kusimamia mchakato wa kutafuta amani  nchini Ukraine. Kardinali zuppi ameteuliwa na Papa kuwa mjumbe wa kusimamia mchakato wa kutafuta amani nchini Ukraine. 

Papa amkabidhi Kardinali Zuppi utume wa amani kwa ajili ya Ukraine

Mkurugenzi wa Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican,kwa ombi la waandishi wa habari,alithibitisha kwamba Papa Francisko amemkabidhi rais wa CEI kufanya utume wenye lengo la kuzindua njia za amani nchini Ukraine.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Akijibu maswali ya waandishi wa habari, mkurugenzi wa Ofisi ya Waandishi wa Habari ya Vatican Dk. Matteo Bruni, alithibitisha kwamba Papa Francisko amemkabidhi Kardinali Matteo Zuppi, Askofu mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Bologna na Rais wa Baraza la Maaskofu wa Italia, jukumu la kuongoza utume, kwa ajili ya makubaliano na Sekretarieti ya Vatican, ambayo itachangia kupunguza mvutano katika mzozo wa Ukraine, kwa matumaini, kwamba Baba Mtakatifu ambaye hajawahi kamwe kusita katika mchakato huo  kwamba “hii inaweza kuanzisha njia za amani. Msemaji mkuu alimalizia kwa kubainisha kuwa “muda wa utume huo na mbinu zake kwa sasa zinachunguzwa”.

 

22 May 2023, 17:00