Tafuta

Imetokea ajali mbaya huko Makedonia na Burgaria ya Bus iliyokuwa na watalii kutoka Instanbul. Imetokea ajali mbaya huko Makedonia na Burgaria ya Bus iliyokuwa na watalii kutoka Instanbul. 

Masikitiko ya Papa kwa waathirika wa ajali mbaya ya Bus nchini Burgaria

Papa Francisko ametuma ujumbe wake,uliotiwa saini na Kardinali Parolin,kuonesha mshikamano na sala kwa Rais wa Makedonia Kaskazini kufuatia na vifo vya watu 46 waliunguzwa na moto katika Bus moja iliyopta ajali barabarani ikiwa inatoka katika utalii jijini Instanbul.

Na Sr. Angella Rwezaula - Vatican

Ajali ya Busi  usiku  ambalo liligeuka kuwa mtego wa moto kwa kusababisha vifo vya  abiria 46 waliokuwa wamelala usingizi wakisafiri. Ni wanaume watatu, wanawake watatu na mvulana mmoja tu  waliofanikiwa kuvunja madirisha na kujiokoa, lakini ambao hawatasahau tukio ambalo katika dakika chache lilibadilisha safari yao ya siku moja katika jiji la Istanbul ambapo walikuwa wameishi vizuri kabla ya ajali hiyo mbaya zaidi kutokea katika maisha  kwenye barabara za Ulaya kwa miaka iliyopita.

Kufuatia na hilo hata Baba Mtakatifu Francisko amesikitishwa sana na habari hiyo, hasa kifo cha watoto 12 na kutuma, telegram yake iliyotiwa saini na Katibu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin, huku ikieleza mshikamano wa dhati na sala kwa waathirika na  ukaribu kwa ajili ya manusura. Telegram hiyo imeelekezwa kwa rais wa Makedonia Kaskazini, nchi ambayo  walikuwa wanatoka waathirika hao.

Tukio hilo la ajali lilitokea  nchini Bulgaria, karibu na kijiji cha Bosnek. Moto wa Bus hilo ulilipuka mara baada ya gari la kampuni ya Beta Trans, maalum kwa ajili ya usafiri wa Istanbul, kuacha barabara. Wakati  huo huo Makedonia imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa na kupeperusha bendera nusu mlingoti; hata nchini Bulgaria pia ilitangaza siku moja  ya maombolezo na  uchunguzi wa mamlaka ya Bulgaria kufunguliwa ili kutoa mwanga juu ya sababu za ajali, kuvunjika au makosa ya kibinadamu, ambayo yameharibu kabisa familia nyingi. Kwa maana hiyo watajaribu kuchunguza ikiwa safari hiyo ilifanywa kwa kufuata hatua na kanuni  za usalama, pia kwa msingi wa shuhuda za walionusurika.

24 November 2021, 16:21