Hija ya kitume ya Papa Francisko Budapest:Mungu ni upendo,mtumishi msulibiwa!
Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.
Video fupi na picha vinaonesha wakati muhimu wa maadhimisho ya misa Takatifu ya Papa Francisko akiwa Budapest kufunga Kongamano la 52 la Ekaristi kimataifa. Katika mahubiri yake Papa Francisko amewaalika waamini kujifungulia wazi yale mapya ya kashfa ya Mungu mtumishi msulibiwa na sio masiha mwenye nguvu. Safari ya kila Mkristo sio kukimbilia mafanikio badala yake inaanzia na hatua ya nyuma.
Katika video ya pili na picha vinaonesha wakati wa Mkutano wa Papa Francisko na Baraza la kiekumene la makanisa na jumuiya za kiyahudi, mara baada ya kufika na kukaribishwa katika uwanja wa ndege. Kwa maana hiyo katika mkutano huo kwenye ukumbi wa jumba la makumbusho la sanaa nzuri, na wawakilishi hao, Papa amesema kuwa Mungu wa mababa anafungua daima njia mpya kwani kama alivyo badili jangwa katika njia ya kuelekea Nchi ya Ahadi, na ndivyo anapenda kutuchukua kutoka kwenye jangwa la ukame wa chuki na kutokujali ili kufikia nchi yenye shauku ya muungano.