Hija ya kitume ya Papa Francisko Budapest:Mungu ni upendo,mtumishi msulibiwa!

Video fupi inaonesha wakati muhimu wa Ibada ya Misa Takatifu katika uwanja uliokaliwa zaidi ya waamini laki moja kwa kuhitimisha Kongamano la 52 Kimataifa huko Budapest.Hili ni Kongamano la pili tangu la 1938.Video ya pili inaonesha wakati wa mkutano wa Baraza la kiekumene la makanisa na Jumuiya ya Kiyahudi.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Video fupi na picha vinaonesha wakati muhimu wa maadhimisho ya misa Takatifu ya Papa Francisko akiwa Budapest kufunga Kongamano la 52 la Ekaristi kimataifa. Katika mahubiri yake Papa Francisko amewaalika waamini kujifungulia wazi yale mapya ya kashfa ya Mungu mtumishi msulibiwa na sio masiha mwenye nguvu. Safari ya kila Mkristo sio kukimbilia mafanikio badala yake inaanzia na hatua ya nyuma.

Papa akifukiza Picha ya Bikira Maria
Papa akifukiza Picha ya Bikira Maria
Papa akiadhimisha misa
Papa akiadhimisha misa
Papa akipokea vipaji
Papa akipokea vipaji
Mkutano wa Papa Francisko na Baraza la kiekuemene la Makanisa na jumuiya ya Kiyahudi

Katika video ya pili na picha vinaonesha wakati wa Mkutano wa Papa Francisko na Baraza la kiekumene la makanisa na jumuiya za kiyahudi, mara baada ya kufika na kukaribishwa katika uwanja wa ndege. Kwa maana hiyo katika mkutano huo kwenye ukumbi wa jumba la makumbusho la sanaa nzuri, na wawakilishi hao, Papa amesema kuwa Mungu wa mababa anafungua daima njia mpya kwani kama alivyo badili jangwa katika njia ya kuelekea Nchi ya Ahadi, na ndivyo anapenda kutuchukua kutoka kwenye jangwa la ukame wa chuki na kutokujali ili kufikia nchi yenye shauku ya muungano.

Mkutano wa Papa wa Kiekumene
Mkutano wa Papa wa Kiekumene
Mkutano wa Papa wa Kiekumene
Mkutano wa Papa wa Kiekumene
12 September 2021, 14:25