Tafuta

2021.05.19 : Katekesi ya Papa 2021.05.19 : Katekesi ya Papa  

Papa Francisko:ufadhaa na uzembe ni vishawishi katika sala!

Papa Francisko katika katekesi yake iliyofanyika katika uwanja wa Mtakatifu Damas Vatican,amewashauri waamini wamwombe Baba Mungu hata kwa njia ya sala ya kwanini,kama afanyavyo mtoto mdogo kwa baba yake na kutembea kwa uvumilivu hata wakati mgumu.Amebainisha vishawishi ambavyo vinajitokeza wakati wa sala kwa mfano ufadhaa na uzembe.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Jumatato tarehe 19 Mei Papa Francisko ameendeleza na katekesi yake kuhusu sala, akiwa katika uwanja wa Mtakatifu Damas Vatican, ambapo  amesema kuwa kusali siyo rahisi, kwa maana kuna matatizo mengi ambayo yanakuja wakati wa kusali. Lazima kuyatambua, kuyachambua na kuyashinda. Ugumu wa kwanza kwa yule anayesali ni fadhaa. (KKK 2729). Unaanza sala na baadaye akili inaanza kuzunguka zunguka ulimwengu mzima, moyo wako huko hapo na akili yako hapo katika jitihada ya maombi. Maombi mara nyingi yanaishi pamoja na fadhaa. Kiukweli akili ya kibadanu inapata ugumu kukaa muda mrefu katika wazo moja. Wote tunafanya uzoefu wa kuingia kwenye shimo hili na kudanganywa na mzunguko huu ambao unatusukunma hadi kufika kwenye usingizi. Wote tunatambua kuwa siyo vizuri kujiachia na kuangukia sehemu. Mapambano ili kulishinda wazo hilo wakati wa zala na ndiyo mtazamamo huo. Ikiwa hufiki hatua ya kutosha ya kujikita kwa wazo hilo huwezi kujifunza faida na wala kufanya kazi vizuri. Wanariadha wanaelewa kwamba katika mashindano hawawezi kushinda kwa kufanya mazoezi ya kimwili tu lakini pia hata nidhamu ya kiakili, hasa kuwa na uwezo wa kukaa kutafakari kwa kina na kubaki kidete na umakini.

Lazima kupambana dhidi ya fadhaa wakati wa sala

Fadhaa siyo makosa, lakini lazima kupambana nayo. Katika urithi wa imani yetu daima kuna fadhila ambayi mara nyingi inasahuliwa lakini ambayo ipo sana katika Injili. Nayo inaitwa kukesha. Yesu alisema sana “kesheni, na salini. Katika katekisimu ya Kanisa katoliki inaeleza wazi katika mafundisho yake kwenye sala. (KKK n. 2730). Mara nyingi inawaalika wafuasi wake na maisha ya dhati yanayoongozwa na wazo ambalo mapema au baadaye Yeye atarudi, kama Bwana harusi  au kama Bwana aliyekwenda safari. Lakini kwa kuwa hatujuhi siku wala saa ya kuja kwake, dakika zote za maisha yetu ni zenye thamani kuu na hayawezi kupotelea kwenye fadhaa. Katika siku ambayo hatujuhi, sauti moja itasikika ya bwana wetu. Katika siku hiyo, heri wale ambao Bwana atawakuwa wanafanya kazi wako tayari wanajali kile ambacho ni muhimu sana.

Hawakupotea kwa kufuata kila fadhaa ambayo ilikuwa inajitokeza katika akili yao, lakini walitambua kutafuta kuembea katika njia ya haki, ya kufanya mema na kazi yao vema.  “Fadhaa hiyo ambayo huzunguka akini, mtakatifu Teresa alikuwa anaiita mweu katika nyumba. Na ni kama mwehu anayekufanya uzunguke zunguke. Lazima kumsimamisha na kufungulia umakini.”Suala hilo linapaswa kuitwa kipindi cha ukavu. Katekisimu ya Kanisa Katoliki inafafanua kwamba: “Ukavu ni sehemu ya taamuli ambamo moyo umetengwa bila muonjo wa fikra kumbu kumbu na hisia hata za kiroho. Huu ni muda wa imani tu inayojishinikiza pamoja na Yesu katika mateso yake katika makali  na kaburin i(n. 2731).  Ukavu unatufanya kufikika Ijumaa Kuu, katika usiku na Jumamosi kuu Takatifu, siku nzima. Yesu hayupo, yuko kaburini; Yesu amekufa. Tuko peke yetu. Na hili ni wazo, yaani mama wa ukavu.

Hatujuhi sababu za ukavu

Mara nyingi hatujuhi ni sababu zipi zitokanazo  na ukavu. Inawezekna kutokana nasi wenyewe lakini pia hata kwa Mungu ambaye anayeruhusu aina fulani ya hali ya maisha ya nje au ndani. Au wakati mwingine inawezekana kuumwa kichwa au figo ambalo linakuzuia kuingia vema katika sala. Walimu wa kiroho wanaelezea uzoefu wa imani kama mwendelezo wa kubadilishana vipindi vya faraja na vya upweke; vipindi ambavyo kila kitu ni rahisi na wakati vingine vipo katika hali  ngumu sana. Papa ameongeza kutoa mfano: unapokutana na rafiki ukauliza  hali yake aatakujibu leo sijisikuu. Na mara nyingi hatujisikii vema yaani hatuna hisia nzuri, hatuna faraja , hatuna jinsi ya kufanya. Ni siku ya kijivu… na zipo nyingi sana katika maisha. Hatari ni kuwa na moyo wa kijivu, hali hiyo ikifikia moyo unaugua… na kuna watu wengi wanaisha na moyo wa kijivu.

Hii ni hatari. Huwezi kubadilika, huwezi kuhisi faraja kwa sababu moyo ni kijivu. Na haiwezekani kupeleka mbele ukavu wa kiroho na moyo wa kijivu. Moyo lazima uwe wazi na angavu ili mwanga wa Bwana uingie. Na ikiwa haiungii, subiri kwa matumaini, Lakini usiufungie katika ukijivu. Papa Francisko aidha amesema kishwaishi kingine ambamo kiburi hufungua lango lake ni uzembe, ambao kwa hakika ni kweli kishawishi dhidi ya sala na zaidi kwa ujumla dhidi ya maisha ya kikristo. Uziembe ndio mtindo wa mhemuka ambao umetokana na udhaifu na hivyo kukosa ari ya kukesha na kukosa kulinda moyo wake (KKK2733).

Uzembe katika sala ni moja ya dhambi saba

Uzembe ni moja wapo ya dhambi mbaya saba kwa sababu, ikichochewa na dhana, inaweza kusababisha kifo cha roho. Kwa maana hii ni jinsi ya kufanya katika mfululizo huu wa shauku na unyong’onyevu? Ndiyo lazima ajifunze kutembea kila wakati. Maendeleo ya kweli ya maisha ya kiroho hayajumuishi katika kuzidisha furaha, lakini katika kuweza kudumu katika nyakati ngumu: tembea, tembea, tembea ... Na ikiwa umechoka, simama kwa muda na utembee tena. Lakini kwa uvumilivu. Tukumbuke mfano wa Mtakatifu Fransi juu ya shangwe kamili: sio katika bahati isiyo na kipimo iliyonyesha kutoka Mbinguni, kwamba ustadi wa mtu wa kweli pimwa, lakini kwa kutembea kwa utulivu, hata wakati mtu hatambuliwi, hata wakati mtu anatendewa vibaya, hata wakati kila kitu kimepoteza ladha ya mwanzo.

"Watakatifu wote wamepitia bonde la giza, na tusishangae ikiwa, tukisoma katika shajara zao tunasikiliza ripoti za sala ya jioni isiyo na maana, waliishi bila ladha. Lazima tujifunze kusema: Hata ikiwa Wewe, Mungu wangu, unaonekana kufanya kila kitu ili kunifanya niache kukuamini, badala yake ninaendelea kukuomba tu. Waamini kamwe hawachoki kusali! Wakati mwingine inawezekana kufanana na ile ya Ayubu, ambaye halikubali kwamba Mungu amtendee isivyo haki, aliandamana na kumhukumu. Hata hivyo mara nyingi, hata kupinga mbele za Mungu ni njia ya kuomba au kama vile yule mama mzee alivyosema kumkasirikia Mungu ni njia ya maombi, pia kwa sababu mara nyingi mtoto hukasirika na baba yake, ni njia ya uhusiano na baba; kwa sababu anamtambua kama baba na hivyo, hukasirika".Papa amesisitiza

Tuombe na kuwa na subira

Papa Francisko akiendelea  na ufafanuzi wake amesema: "Na sisi pia, ambao ni watakatifu kidogo na na wasio na subira kuliko Ayubu, tunajua kwamba mwishowe, katika wakati  wa mwisho wa ukiwa, ambao tumepaza kilio Mbinguni kama  bubu na wengi kwa kusema kwanini", Mungu atatujibu. Baba Mtakatifu ameongeza kusema: “Msisahau sala ya kwanini?”: Ni sala ambayo watoto hufanya wakati wanaanza kuelewa mambo na wanasaikolojia wanaiita umri wa kwa nini, kwa sababu mtoto anamuuliza baba yake: “Baba, kwanini ... ? Baba, kwanini ...? Baba, kwanini ...? ". Lakini tuwe waangalifu: Yeye hasikilizi jibu la baba. Kwa sababu Baba anapoanza kujibu na [yeye] anarudia swali jingine la kwanini."

Kwa kutoa sababu yake Baba Mtakatifu amesema "Hiyo ni kwasababu anataka tu kuvutia macho ya baba yake kwake mwenyewe; na tunapomkasirikia Mungu kidogo na kuanza kusema kwanini, tunavuta moyo wa Baba yetu kuelekea shida zetu, kuelekea ugumu wetu, katika maisha yetu. Lakini ndiyo, uwe na ujasiri wa kumwambia Mungu kuwa kwa nini ...? Kwa sababu wakati mwingine, kukasirika kidogo ni kuzuri, kwa sababu inatufanya tuamshe uhusiano huu kutoka kwa mwana kwenda kwa Baba, kutoka kwa binti kwenda kwa Baba, ambapo lazima tuwe nao na Mungu.Na pia ni kielelezo chetu  kigumu na kichungu zaidi, Yeye atayapokea kwa upendo wa baba, na kutuchukulia  kama tendo la imani, na kama sala", amehitimisha Papa Francisko katekesi yake.

KATEKESI YA PAPA 19 MEI 2021

 

19 May 2021, 15:31

Mikutano ya Baba Mtakatifu kwa siku za hivi karibuni

Soma yote >