Tafuta

KANISA LA ROHO MTAKATIFU LENYE PICHA YA YESU WA HURUMA, ROMA KANISA LA ROHO MTAKATIFU LENYE PICHA YA YESU WA HURUMA, ROMA 

Papa Francisko:Moto wa Yesu wa huruma umeenea ulimwenguni kote!

Katika kilele cha kumbu kumbu ya miaka 90 tangu tokea la Yesu wa huruma kwa Mtakatifu Faustina Kowalska,mnamo 22 februari 193,Papa Francisko ametuma ujumbe wake kwa Askofu wa Plock,nchini Poland akitoa ushauri wa kurudi katika kisima cha huruma ili kugeuka kuwa wavumilivu, msamaha na upendo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko amemwandikia Barua Askofu Piotr Libera, wa  Jimbo la Plock nchini Poland na jumuiya nzima ya Kanisa la Plock akionesha  kushiriki kikamlifu pamoja nao kiroho katika kuadhimisha kumbu kumbu ya miaka 90 tangu kutokewa Yesu wa Huruma kwa Mtakatfu Faustina Kowalska, manamo tarehe 22 Februari 1931. Papa anaungana nao kushiriki katika Maadhimisho ya Misa kwenye Madhabahu ya Huruma na wale wote ambao wanashiriki misa hiyo kwa njia ya vyombo vya  habari na matangazo. Katika barua hiyo Papa Francisko anabainisha kwamba anakumbuka maneno ya Mtakatifu Faustina ya wakati ule aliyoambia na Yesu kuwa: “Uchore picha hiyo kwa mujibu wa kile uonacho, ikiwa na maelezo: “Yesu, ninakutumainia”. Ninatamani kuwa picha hii iweze kuheshimiwa kwanza katika kikanisa chenu na baadaye ulimwengu mzima” (taz shajara 47).

Mtakatifu Faustina Kowalska katika picha ya huruma
Mtakatifu Faustina Kowalska katika picha ya huruma

Katika barua hiyo Papa Francisko anashirikisha furaha ya Kanisa la  Płock  kwamba tukio hili maalum ambalo tayari linajulikana ulimwenguni kote na linabaki kuwa hali  halisi katika moyo wa waamini. Katika fursa hii ya kumbu kumbu, Papa amependa pia maneno mengine ya Bwana Yesu ambayo yaliandikwa kwenye shajara la Mtakatifu Fautina: “Ubinadamu hautajua amani mpaka utakapogeukia kisima  cha huruma  yangu” (taz. 699). Kwa njia hiyo, Papa anawatia moyo ili  wageukie kisima hicho, kwa kuomba Kristo zawadi ya huruma. Kuacha kukumbatiwa naye na ili yeye apate  kupenyeza. Lazima kuwa na ujasiri wa kurudi kwa Yesu na kukutana na upendo wake na huruma katika sakramenti. Kuhusu ukaribu wake na upole na kwa njia hiyo itawezekana kuwa na uwezo wa huruma, uvumilivu, msamaha na upendo.

Papa Francisko aidha ameandika kwamba Mtume wa Upendo, Mtakatifu Yohane Paulo II ambaye alipendelea kuwa ujumbe wa upendo wa huruma ya Mungu uweze kufikia wakazi wote wa dunia, alikuwa akiwatia moyo akisema “Moto wa huruma lazima utangazwe ulimwenguni. Katika huruma ya Mungu, ulimwengu utapata amani na binadamu atapata furaha” (Kracow - Łagiewniki, 17 Agosti 2002). Papa Francisko amesema hii ni changamoto maalum kwa ajili ya Kanisa la Płock, iliyooneshwa ufunuo huo, kwa ajili ya Shirika la watawa wa Mama Yetu wa Huruma, kwa jiji la Płock na kwa kila mmoja wao. Waoneshe moto wa Yesu wa Upendo ulimwenguni. Wawe ishara ya uwepo wake kati yao na kwa kila mtu. Kwa kuhitimisha kwa upande wa Askofu, Jimbo zima la Płock na washiriki wote wa maadhimisho ya miaka 90 ya kumbu kumbu ya kutokewa Yesu wa Huruma, Papa Francisko amewapa baraka yake ya kitume kwa moyo wote, na kuhitimisha barua hiyo.

22 February 2021, 14:46