Tafuta

Vatican News
2021.02.21  YESU WA HURUMA 2021.02.21 YESU WA HURUMA  

Papa Francisko:Tufungulie mioyo yetu katika Huruma ya Mungu

Mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana,Papa amekumbuka miaka 90 iliyopita tangu Mtakatifu Faustina Kowalska,alipooneshwa picha ya Yesu wa Huruma.Ujumbe huo umefikia ulimwenguni kote na sio mwingine isipokuwa Injili ya Yesu Kristo,aliyekufa na kufufuka,ambaye anatupatia huruma ya Baba”,Papa amesema.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Mara baada ya tafakari na sala ya Malaika wa Bwana, Papa Francisko, Jumapili tarehe 21 Februari 2021 akiwageukia waamini na mahujaji  waliounganika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, Vatican amewasalimia wote. Kwa namna ya pekee wapoland. Wazo lake kwa maana hiyo ni katika madhabahu ya Płock, nchini Poland, mahali ambapo miaka 90 iliyopita Bwana Yesu alimtokea Mtakatifu Faustina Kowalska, akimkabidhi  ujumbe maalam wa Huruma ya Mungu.

Papa Francisko akiendelea amesema “Kwa njia ya Mtakatifu Yohane Paulo II, Ujumbe huo umefikia ulimwenguni kote na sio mwingine isipokuwa Injili ya Yesu Kristo, aliyekufa na kufufuka,  na mbaye anatupatia huruma ya Baba”.  “Tumfungulie mioyo na kusema kwa imani: “Yesu ninakutumainia”.  Papa Francisko aidha amewasalimia vijana na watu wazima wa kikundi cha Talità Kum, cha Parokia ya Mtakatifu Yohane wa Fiorentini, Roma. Amewashukuru uwepo wao na kuwaomba waendelee mbele kwa furaha na mipango yao ya wema. Na kwa wote, Papa Francisko amewatakia Dominika Njema. Na ilikuwa ni Domika ya jua! Hatimaye amewaomba wasisahau kusali kwa ajili yake.

21 February 2021, 15:45