Tafuta

2020.12.04 Papa akipokea hati za utambulisho wa mabalozi wapya kuwakilisha nchi zao Vatican 2020.12.04 Papa akipokea hati za utambulisho wa mabalozi wapya kuwakilisha nchi zao Vatican 

Papa Francisko kwa mabalozi wapya:uwakilishi wa nchi zao Vatican usaidie kukutana!

Papa amehutubia mabalozi wapya wasio wakazi wanaoziwakilisha nchi zao mjini Vatican wakati wa kuwakilisha hati za utambulisho tarehe 4 Desemba 2020.Hawa ni mabalozi kutoka Yordan,Kazakhstan,Zambia,Mauritania,Uzbekistan,Madagascar,Estonia,Rwanda,Danimark na India.Ni matashi ya Papa Francisko kwamba uwakilishi wa nchi zao Vatica unaweza kusaidia kukutana.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Ijumaa tarehe 4 Desemba 2020 Papa Francisko, amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Mabalozi wasio wakazi wanao ziwakilisha nchi zao mjini Vatican. Balozi hawa wanatoka Yordan, Kazakhstan, Zambia, Mauritania, Uzbekistan, Madagascar, Estonia, Rwanda, Danimark na India. Amewaomba kufikisha salam na pongeza zake kwa wakuu wao wa nchi pamoja na kuwahakikisha maombi yake kwa ajili yao na kwa ajili ya wazalendo wao.

Utume wao umeanzia  katika kipindi cha changamoto ya  familia yote ya kibinadamu. Hata kabla ya janga la Covid-19, ilikuwa wazi kuwa 2020 ingekuwa mwaka mwenye kuwa na ulazima wa dharura ya kibinadamu, ambayo ilikuwa inatokana na migogoro, vurugu na ugaidi, katika sehemu mbali mbali za Dunia, Papa amesema. Mgogoro wa kiuchumi unaendelea kusababisha njaa na wimbi la uhamiaji, wakati mabadiliko ya tabianchi yanazidi kuleta hathari za majanga ya asili, njaa na ukame.  Na sasa janga linaloendelea kuongeza zaidi ukosefu wa usawa ambao ulikuwa tayari upo katika jamii zetu. Kiukweli umaskini na zaidi walio katika mazingira magumu kaka na dada, wako hatari ya kutowajali, kubaguliwa, na kusahauliwa, amesisitiza Papa. “Mgogoro umetufanya kutambua kuwa tunajikuta  katika mtumbwi mmoja, wote wadhaifu na wasio na mwelekeo, lakini wakati huo huo, walio wa muhimu na lazima na kwamba  tumealikwa kupiga kasia pamoja, na wote tunahitaji msaada wa pamoja”.( Vatican maombi  27 Machi 2020 Vatican).

Papa Francisko aidha akiendelea na hotuba yake amesema “ labda leo hii ni  zaidi ya wakati mwingine, ulimwengu unazidi kuwa na utandawazi, una dharura ya kuwa na mazungumzo na ushirikiano wa kweli na heshima, wenye uwezo wa kukabiliana na hatari kubwa ambazo zinakumba sayari yetu  na kuleta wasiwasi  wa wakati ujao wa kizazi cha vijana”. Katika Wosia wa hivi karibuni  wa “ Fratelli tutti” Papa amesema emeonesha shauku yake kwamba: “ Katika kipindi chetu hiki, ambacho tumepewa kuishi, kwa uambuzi  wa hadhi ya kila mtu mwanadamu, tunaweza kufanya kuzaliwa kati ya wote shauku ya ulimwengu wa kidugu” (Fratelli tutti  n.8).  Uwakilishi wa Vatican katika Jumuiya ya Kimataifa inajikita katika huduma ya wema wa pamoja ulimwenguni  na  wote tunaalikwa kuwa na umakini juu ya mantiki ya kibinadamu, kimaadili na kidini katika masuala mbalimbali yanayotazama  maisha ya mwandamu, watu na mataifa yote”, Papa amesisitiza.

Ni tumaini la Papa Francisko kuwa kazi yao ya kidiplomasia kama wawakilishi wa nchi zao jijini Vatican zinaweza kusaidia utamaduni wa kukutana  ( Fratelli tutti, 215),  ulazima ambao unasaidia kushinda tofauti na migawanyiko ambayo mara nyingi ni kikwazo  cha kutimiza maono makubwa na malengo ya mapendekezo ya Jumuiya ya Kimataifa. Kila mmoja anaalikwa kushirikiana kila siku kwa ajili ya ujenzi wa ulimwengu wa haki zaidi, wa udugu na muungano. Kwa kuhitimisha hotuba yake, amesema “wakiwa wanaanza kuwakilishi wa  anchi zao Vatican, amewatakia mema na kuwahakikisha uwezekano  wa ushirikiano kupitia ofisi mbalimbali za sekretarieti  mjini Vatican ili kuwawezesha kutimiza uwajibikaji wao. Na juu yao, familia zao, wahudumu wao na wazalendo wao amewapa baraka ya Mungu.

04 December 2020, 17:14