Papa Francisko kwa mabalozi wapya:uwakilishi wa nchi zao Vatican usaidie kukutana!
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican
Ijumaa tarehe 4 Desemba 2020 Papa Francisko, amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Mabalozi wasio wakazi wanao ziwakilisha nchi zao mjini Vatican. Balozi hawa wanatoka Yordan, Kazakhstan, Zambia, Mauritania, Uzbekistan, Madagascar, Estonia, Rwanda, Danimark na India. Amewaomba kufikisha salam na pongeza zake kwa wakuu wao wa nchi pamoja na kuwahakikisha maombi yake kwa ajili yao na kwa ajili ya wazalendo wao.
Utume wao umeanzia katika kipindi cha changamoto ya familia yote ya kibinadamu. Hata kabla ya janga la Covid-19, ilikuwa wazi kuwa 2020 ingekuwa mwaka mwenye kuwa na ulazima wa dharura ya kibinadamu, ambayo ilikuwa inatokana na migogoro, vurugu na ugaidi, katika sehemu mbali mbali za Dunia, Papa amesema. Mgogoro wa kiuchumi unaendelea kusababisha njaa na wimbi la uhamiaji, wakati mabadiliko ya tabianchi yanazidi kuleta hathari za majanga ya asili, njaa na ukame. Na sasa janga linaloendelea kuongeza zaidi ukosefu wa usawa ambao ulikuwa tayari upo katika jamii zetu. Kiukweli umaskini na zaidi walio katika mazingira magumu kaka na dada, wako hatari ya kutowajali, kubaguliwa, na kusahauliwa, amesisitiza Papa. “Mgogoro umetufanya kutambua kuwa tunajikuta katika mtumbwi mmoja, wote wadhaifu na wasio na mwelekeo, lakini wakati huo huo, walio wa muhimu na lazima na kwamba tumealikwa kupiga kasia pamoja, na wote tunahitaji msaada wa pamoja”.( Vatican maombi 27 Machi 2020 Vatican).
Papa Francisko aidha akiendelea na hotuba yake amesema “ labda leo hii ni zaidi ya wakati mwingine, ulimwengu unazidi kuwa na utandawazi, una dharura ya kuwa na mazungumzo na ushirikiano wa kweli na heshima, wenye uwezo wa kukabiliana na hatari kubwa ambazo zinakumba sayari yetu na kuleta wasiwasi wa wakati ujao wa kizazi cha vijana”. Katika Wosia wa hivi karibuni wa “ Fratelli tutti” Papa amesema emeonesha shauku yake kwamba: “ Katika kipindi chetu hiki, ambacho tumepewa kuishi, kwa uambuzi wa hadhi ya kila mtu mwanadamu, tunaweza kufanya kuzaliwa kati ya wote shauku ya ulimwengu wa kidugu” (Fratelli tutti n.8). Uwakilishi wa Vatican katika Jumuiya ya Kimataifa inajikita katika huduma ya wema wa pamoja ulimwenguni na wote tunaalikwa kuwa na umakini juu ya mantiki ya kibinadamu, kimaadili na kidini katika masuala mbalimbali yanayotazama maisha ya mwandamu, watu na mataifa yote”, Papa amesisitiza.
Ni tumaini la Papa Francisko kuwa kazi yao ya kidiplomasia kama wawakilishi wa nchi zao jijini Vatican zinaweza kusaidia utamaduni wa kukutana ( Fratelli tutti, 215), ulazima ambao unasaidia kushinda tofauti na migawanyiko ambayo mara nyingi ni kikwazo cha kutimiza maono makubwa na malengo ya mapendekezo ya Jumuiya ya Kimataifa. Kila mmoja anaalikwa kushirikiana kila siku kwa ajili ya ujenzi wa ulimwengu wa haki zaidi, wa udugu na muungano. Kwa kuhitimisha hotuba yake, amesema “wakiwa wanaanza kuwakilishi wa anchi zao Vatican, amewatakia mema na kuwahakikisha uwezekano wa ushirikiano kupitia ofisi mbalimbali za sekretarieti mjini Vatican ili kuwawezesha kutimiza uwajibikaji wao. Na juu yao, familia zao, wahudumu wao na wazalendo wao amewapa baraka ya Mungu.