Tafuta

Vatican News
Papa Francisko Papa Francisko  (ANSA)

Mtandao wa Kimataifa wa nia za Sala umegeuka kuwa Mfuko wa Vatican

Mtandao wa kimataifa wa Nia za Maombi ya kila mwezi ya Papa imekeguka kuwa Mfuko wa kipapa Vatican na makao yake mjini Vatican na utaendelea kushughulikiwa na Jumuiya ya Yesu kama ujumte wa huruma ulimwenguni.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko ameandika kwa maandishi yake kufuatia na uchaguzi binafsi kwa mujibu wa sheria ya Kanoni kuunda Mfuko wa Vatican ujulikanao “Mtandao Kimataifa wa Sala wa Papa”. Mtandao wa Kimataifa wa Sala ya Papa umekwisha kuwa tayari Utume wa Sala, ulionzishwa nchini Ufaransa na  Padre François-Xavier Gautrelet, S.J., na ambao unasimika mzizi yake juu ya Roho ya Moyo Mtakatifu wa Yesu na kupokea nia za kila mwezi za sala, zinazopendekezwa na Baba Mtakatifu. Katika kuundwa huko, shirika hilo la kijesuit ndilo litawajibika kushughulikia utume huo.

Katika maelezo yake amesema “Miaka kadhaa iliyopita, Papa Francisko anaandika kuwa, niliridhia Mtandao wa Kimataifa wa Nia ya Maombi ya sala ya Papa kama Shughuli ya Kipapa kwa ajili ya kusisitizia tabia ya ulimwengu kwa ajili utume huo na ulazima ambao watu wote wanapaswa kusali daima na zaidi  kwa moyo wa dhati. Kwa lengo la kuratibu na kuweka chachu ya harakati hii ya kiroho na ambayo Papa ameseme anapendezwa nayo na  kwa maana hiyo ni , kuipa  muundo unaostahili  wa kipindi tunachoishi, kwa kuzingatia ukuu wake wa kitume katika Kanisa na kwa ajili ya ukuu wa Serikali ya  ya mji wa  Vatican.

Katika muktadha wa sheria Kanoni na kifungu cha  1 n. 1 ya Sheria Msingi ya Mji wa Vatican ya tarehe 26 Novemba 2000 na  kwa kukubali ombi lililowasilishwa na Mtandao wa Maombi Ulimwenguni wa Papa, ameridhia yeye binafsi sheria ya kanoni na Mfuko wa Vatican wa Mtandao wa Sala ya Papa” kwa kuwa na Makao yake katika Mji wa Vatican, inayosimamiwa na Sheria zilizounganishwa na Maandishi(Chirograph)haya, iliyoidhinishwa na mimi leo, na ambayo itaanza kutumika kuanzia tarehe  17 Desemba 2020. Barua hiyo imetiwa saini Mji wa Vatican, tarehe 17 Novemba 2020.

 

03 December 2020, 17:29