Tafuta

Ripoti ya McCarrick:Ukaribu wa Papa kwa waathiriwa

Papa Francisko mara baada ya katekesi yake amepyaisha jitihada za Kanisa kwa ajili ya kuondoa kabisa janga la manyanyaso ya kijinsia katika Kanisa.

VATICAN NEWS

Ukaribu wa wahanga wa manyanyaso na jitihada kwa ajili ya kufanya kwamba janga hili linaondolewa kabisa katika Kanisa, ndiyo maneno ya Papa Francisko mara baada ya tafakari ya Katekesi ya kila Jumatano  tarehe 11 Novemba 2020. Ni katika fursa ya kutangazwa kwa Ripoti kuhusu aliyekuwa Kardinali wa zamani Theodore McCarrick, ambaye alitambuliwa kuwa mhusika wa manyanyaso ya kijinsia ya watoto na kusimamishwa huduma zote za uklero mnamo mwaka 2019.

“Jana ilichapishwa Ripoti juu ya kesi chungu ya Kardinali wa zamani Theodore McCarrick, amesema Papa, mara  baada ya katekesi, yake  ambayo imefanyika kwenye runinga kutokea katika Maktaba ya Jumba la Kitume na kwamba "ninasasisha ukaribu wangu kwa wahanga wa kila unyanyasaji na jitihada za  Kanisa ili kumaliza uovu huu”.

Baada ya kutamka maneno hayo Papa Francisko amebaki kidogo kwa ukimya akisali.

Ripoti ya McCarrick, iliyoundwa na kurasa 461 na ushuhuda, inakusanya habari zote muhimu juu ya ufahamu kwa mujibu wa taasisi husika na mchakato wa kufanya uamuzi ambao ulihusisha hatua kuu katika maisha ya kadinali wa zamani, aliyepewa ngazi ya  askofu mkuu wa Washington mwishoni mwa mwaka 2000 na mwaka  mmoja baadaye aliinuliwa kuwa kardinali. Ripoti hiyo, iliyochapishwa na Sekretarieti ya Vatican kwa mamlaka kutoka kwa Baba Mtakatifu Francisko, ni matokeo ya uchunguzi wa miaka miwili.

“Ripoti hiyo alithibitisha Katibu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin kwamba itakuwa na matokeo katika hilo, hasa kwa kuwafanya wale wote wanaohusika katika uchaguzi huo kujua zaidi ule uzito wa maamuzi yao au mapungufu. Hizi ni kurasa ambazo zinatuongoza kutafakari kwa kina na kujiuliza ni nini tunaweza kufanya zaidi katika siku zijazo, tukijifunza kutokana na uzoefu wa uchungu wa wakati uliopita”.

11 November 2020, 16:13