Tafuta

Ripoti kuhusu McCarrick,ukurasa wa uchungu ambapo Kanisa linajifunza

Vatican imetangaza Ripoti kuhusu tukio la aliyekuwa Kardinali,Askofu Mkuu wa Washington aliyevuliwa mamlaka ya uklero.Kardinali Parolin anasema alisimamishwa kwa ajili ya kutafuta ukweli ili makosa ya wakati uliopita yasirudiwe tena.

VATICAN NEWS

Leo hii imatengazwa Ripoti kuhusu utambuzi kwa upande wa taasisi na maamuzi ya mchakato wa Vatican kuhusu aliyekuwa Kardinali Theodore Edgar McCarrick (tangu 1930 hadi 2017)ambapo ofisi ya katibu wa Serikali imeifanyia kazi kwa mujibu wa Papa.  Ni maandishi kamili na mazito, ambayo yamechukua miaka miwili ya kazi. Ripoti hiyo inajibu juhudi ambayo imeanzishwa na Papa Francisko, ya kuchunguza kwa kina kesi ya McCarrick, mwenye tuhuma za manyanyaso ya kijinsia kwa wadogo na watu wazima, na kuwakilisha pia kitendo cha kujali kwake jamuiya Katoliki ya Marekani, ambayo imejeruhiwa na matukio kama hayo.

Kutokana na Ripoti hiyo, imeonesha mambo fulani. La kwanza linatazama makosa yaliyotendeka, ambayo yameruhusu mtu mhusika na  uhalifu wa namna hiyo kufikia hatua ya kufunika nafasi kuu katika uongozi wa Kanisa hasa kwa kuzingatia kuwa Kanisa lilikuwa  tayari limekwisha toa kanuni mpya ya  kuzuia historia  kama hiyo isirudiwe tena. Jambo la pili linahusu kutokuwepo hadi 2017, ya tuhuma  ambazo zinatazama manyanyaso dhidi ya watoto zilizotendwa na McCarrick.  Tuhuma ya kwanza inayohusiana na watoto ni ile ya miaka mitatu iliyopita iliyopelekea ufunguzi wa haraka wa mchakato wa sheria ya Kanisa, iliyohitimishwa kwa maamuzi mawili ya Papa: kwanza kumwondolea majukumu McCarrick na kwa maana hiyo kumwachisha kutoka hali ya uklero.

Kesi hiyo ni ukurasa wa uchungu ambao Kanisa lote limejifunza. Kiukweli inawezekana kutazama baadhi ya mambo ambayo Papa Francisko baada ya Mkutano wa Maaskofu kwa ajili ya ulinzi wa watoto uliofanyika mnamo Februari 2019, ambamo katika mwanga wa tukio hilo, kati ya mambo yaliyojitokeza ni  siri ya Kipapa ya kesi za manyanyaso.

“ Kama inavyoonesha ripoti na wingi wa hati zilizofuata na maelezo yaliyomo ndani mwake, tumejikita katika kutafuta ukweli”, amesisitiza Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican na kuongeza “uchungu unasikindizwa na mtazamo wa tumaini. Ili matukio kama haya yasiweze kurudiwa tena, pamoja na kuwa na kanuni thabiti zaidi, tunahitaji uongofu wa mioyo. Kuna haja ya kuwa na wachungaji waaminifu, na watangazaji wa Injili, na lazima sote tuwe na dhamiri nzuri kwamba kile ambacho kinawezekana  ni kwa neema ya Roho Mtakatifu, katika kuamini maneno ya Yesu “bila mimi hamwezi kitu”.

Kwa mujibu wa Katibu wa Vatican anaawaalika kusoma hati yote ili hatimaye kupata hali halisi na kuepuka kutoa hitimisho lisilo sahihi. “Tunatangaza ripoti hii kwa uchungu kwa ajili ya majeraha ambayo yamesababishwa kwa waathirika na familia zao, kwa Kanisa la Marekani na Kanisa la ulimwengu. Kwa kujua zaidi soma ripoti hii:

http://www.vatican.va/resources/resources_rapporto-card-mccarrick_20201110_en.pdf

 

10 November 2020, 14:00