Papa anatoa mwaliko wa kila mmoja kuwa hekalu la Mungu
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.
Papa Francisko mara baada ya katekesi yake akisalimia waamini wa lugha ya kitaliano amekumbusha kuwa tarehe 18 Novemba siku kuu ya kutabarukiwa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Vatican, na lile la Mtakatifu Paulo nje ya Roma. Siku kuu hiyo iwe na mwanga muhimu wa Kanisa na jengo takatifu mahali ambamo wanakusanyika waamini na kuweza kutufanya sisi sote kuwa na utambuzi ya kwamba kila mmoja ameitwa kuwa hekalu la Mungu. Wazo la Papa limewaendea kama wakaida wazee, vijana, wagonjwa na wanandoa wapya. Amewashauri kupenda Kanisa la Bwana; kushirikiana kwa ukarimu na shauku ya ujenzi wake; kuishi kwa kujitoa sadaka na sala zao pamoja na mateso yao kama mchango muhimu wa ujenzi wa Kanisa la Bwana, nyumba ya aliyejuu katikati yetu” amesisitiza.