Tafuta

2020-11-02 Papa Francisko na Kardinali mteule  Silvano Maria Tomasi 2020-11-02 Papa Francisko na Kardinali mteule Silvano Maria Tomasi 

Mwakilishi Mpya wa Kipapa katika Shirika la Kijeshi la Malta

Mahojiano na Kardinali mteule,Silvano Maria Tomaso ambaye Papa tarehe Mosi Novemba amemteua kumwakilisha katika mchakato wa kusasisha Mkataba wa Katiba la Shirika la kijeshi la Malta amesema kuwa anao uhakika kwamba kwa mapenzi mema ya wote,wanaweza kupiga hatua mbele na ya kweli kufanya marekebisho ambayo Baba Mtakatifu anataka.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kardinali mteule Silvano Maria Tomasi, wa shirika laWascabriani mwenye umri wa miaka 80 na ambaye aliwahi kuwa Mwakilishi wa kudumu wa Vatican katika Ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Gineva, na mhudumua wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya binadamu, kwa sasa ni Mwakilishi mpya maalum katika Hospitali ya Shirika la Kijeshi la Mtakatifu Yohane wa Yerusalem, Rhode na Malta. Ameteuliwa na Papa Francisko tarehe Mosi Novemba 2020 kuwa mwakilishi wake wa Kipapa. Kardinali mteule na wenzake watashiriki  katika Baraza la Makardinali mnamo tarehe 28 Novemba na ambaye  anachukua nafasi ya Kardinali Angelo Becciu, aliyekuwa ameteuliwa na Papa Francisko mnamo Februari 2017 . Jukumu lake litakuw ni lile la kuunga mkono wa mchakato  wa kusasisha Mkataba wa Katiba ya Shirika hilo. Hata hivyo uteuzi huo unakuja wakati bado subira ni kubwa ya kutaka kujua atakuwa ni nani Mkuu mpya wa Shirika la Kijeshi la Malta, mara  baada ya kifo cha Fra' Giacomo Dalla Torre kilichotokea tarehe 29 Aprili iliyopita.

Kwa mujibu wa barua ya Papa anaandika kuwa: “Uteuzi huwa wa kuwa mwakilishi wangu Maalum katika Shirika la Kijeshi la Hopstiali ya Mtakatifu Yohane wa Yerusalemu ya Rhode na Malta(S.M.O.M.) na katika  shughuli ya kushirikishana kwa kiasi kikubwa kwa ajili ya wema wa Shirika hilo na  Fra’ Ruy Gonçalo do Valle Peixoto de Villas Boas, ambaye ni Mkuu wa mpito wa shirika hilo na wakati wa  kusubiri kuchaguliwa mkuu ipasavyo.  Yeye atachukua majukumu yote ya lazima kuamua masuala yoyote ambayo yanaweza kujitokeza kwa utekelezaji wa agizo aliokabidhiwa, kupokea kiapo cha Mkuu ajaye na atakuwa ni msemaji wangu wa kipekee kwa yote yanayohusu uhusiano kati ya Makao haya ya   Kitume na shirika la kijeshi.  Ninakuomba utekeleze ofisi ya Uwakilishi wangu hadi kumalizika kwa mchakato wa kusasisha Katiba na Kanuni ya Malta na kwa hali yoyote mpaka nitakapoona ni muhimu kwa Agizo lenyewe”,  Papa ameandika.

Kufuatana na jukumu hilo  Kardinali Mteule ameelezea juu ya shughuli hiyo mpya ambayo amekabidhiwa na Papa Francisko kuwa “Baba Mtakatifu anao wasiwasi wa kufuatilia wema wa  Shirika la Malta ambalo linajishughulisha na nyanja mbali mbali, kama vile kusaidia wakimbizi na watu walio pembezoni mwa jamii, na ambayo inatoa msaada wa kibinadamu kwa watu wengi. Shirika  hili la zamani sana, ambalo sasa lina zaidi ya miaka 900 katika huduma yake na , lazima liendelee kutekeleza jukumu lake, dhamira yake ya mema, ya huduma, kwa watu wahitaji zaidi”.  Aidha kwa kuongezea Kardinali Mteule amesema “kwa maana hii, Papa amejitoa na kuwa na  nia ya kusaidia na kukuza ufanisi na maendeleo mazuri yashirika  hili.  “Nitajitahidi kadiri niwezavyo kujibu matarajio ya Baba Mtakatifu, ili, kwa roho ya ushirikiano na muungano kuelekea wema huo wa  pamoja ambao ndiyo kanuni ya Shirika hilo  la kuwahudumia maskini na kutetea imani, ili kusonga mbele, kusaidia  na kuwezesha kufanikiwa kwa lengo hili”.

Akifafanua Kardinali mteule Silvano Maria Tomasi, juu ya roho yake ilivyo kufuatia na jukumu hili  alilokabidhiwa Kardinali Mteule amesema “Mimi ni kama punda anayevuta gari. Natumaini ninaweza kufanya kazi ambayo ni muhimu. Baba Mtakatifu amenikabidhi jukumu hili, kiukweli nitajitahidi kufanya jukumu hili kuwa muhimu kwa shirika  la Malta na kutimiza matakwa ya Baba Mtakatifu. Ninaipenda sana Shirika hili kwa sababu kiukweli lina historia tukufu na, kwa njia fulani, mimi ni mshiriki wa Shirika hili  kwa sababu nilifanya kazi  zamani,  na kwa mahitaji ya Shirika  mimi ni msimamizi wa Kanisa la  Msalaba Mkuu. Kwa hivyo nina hakika kwamba kwa mapenzi mema ya wote, tunaweza kuchukua hatua mbele na kutekeleza kweli mageuzi ambayo Baba Mtakatifu anataka”, amesema Kardinali mteule Silvano Maria Tomasi.

02 November 2020, 15:00