Mwakilishi Mpya wa Kipapa katika Shirika la Kijeshi la Malta
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican
Kardinali mteule Silvano Maria Tomasi, wa shirika laWascabriani mwenye umri wa miaka 80 na ambaye aliwahi kuwa Mwakilishi wa kudumu wa Vatican katika Ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Gineva, na mhudumua wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya binadamu, kwa sasa ni Mwakilishi mpya maalum katika Hospitali ya Shirika la Kijeshi la Mtakatifu Yohane wa Yerusalem, Rhode na Malta. Ameteuliwa na Papa Francisko tarehe Mosi Novemba 2020 kuwa mwakilishi wake wa Kipapa. Kardinali mteule na wenzake watashiriki katika Baraza la Makardinali mnamo tarehe 28 Novemba na ambaye anachukua nafasi ya Kardinali Angelo Becciu, aliyekuwa ameteuliwa na Papa Francisko mnamo Februari 2017 . Jukumu lake litakuw ni lile la kuunga mkono wa mchakato wa kusasisha Mkataba wa Katiba ya Shirika hilo. Hata hivyo uteuzi huo unakuja wakati bado subira ni kubwa ya kutaka kujua atakuwa ni nani Mkuu mpya wa Shirika la Kijeshi la Malta, mara baada ya kifo cha Fra' Giacomo Dalla Torre kilichotokea tarehe 29 Aprili iliyopita.
Kwa mujibu wa barua ya Papa anaandika kuwa: “Uteuzi huwa wa kuwa mwakilishi wangu Maalum katika Shirika la Kijeshi la Hopstiali ya Mtakatifu Yohane wa Yerusalemu ya Rhode na Malta(S.M.O.M.) na katika shughuli ya kushirikishana kwa kiasi kikubwa kwa ajili ya wema wa Shirika hilo na Fra’ Ruy Gonçalo do Valle Peixoto de Villas Boas, ambaye ni Mkuu wa mpito wa shirika hilo na wakati wa kusubiri kuchaguliwa mkuu ipasavyo. Yeye atachukua majukumu yote ya lazima kuamua masuala yoyote ambayo yanaweza kujitokeza kwa utekelezaji wa agizo aliokabidhiwa, kupokea kiapo cha Mkuu ajaye na atakuwa ni msemaji wangu wa kipekee kwa yote yanayohusu uhusiano kati ya Makao haya ya Kitume na shirika la kijeshi. Ninakuomba utekeleze ofisi ya Uwakilishi wangu hadi kumalizika kwa mchakato wa kusasisha Katiba na Kanuni ya Malta na kwa hali yoyote mpaka nitakapoona ni muhimu kwa Agizo lenyewe”, Papa ameandika.
Kufuatana na jukumu hilo Kardinali Mteule ameelezea juu ya shughuli hiyo mpya ambayo amekabidhiwa na Papa Francisko kuwa “Baba Mtakatifu anao wasiwasi wa kufuatilia wema wa Shirika la Malta ambalo linajishughulisha na nyanja mbali mbali, kama vile kusaidia wakimbizi na watu walio pembezoni mwa jamii, na ambayo inatoa msaada wa kibinadamu kwa watu wengi. Shirika hili la zamani sana, ambalo sasa lina zaidi ya miaka 900 katika huduma yake na , lazima liendelee kutekeleza jukumu lake, dhamira yake ya mema, ya huduma, kwa watu wahitaji zaidi”. Aidha kwa kuongezea Kardinali Mteule amesema “kwa maana hii, Papa amejitoa na kuwa na nia ya kusaidia na kukuza ufanisi na maendeleo mazuri yashirika hili. “Nitajitahidi kadiri niwezavyo kujibu matarajio ya Baba Mtakatifu, ili, kwa roho ya ushirikiano na muungano kuelekea wema huo wa pamoja ambao ndiyo kanuni ya Shirika hilo la kuwahudumia maskini na kutetea imani, ili kusonga mbele, kusaidia na kuwezesha kufanikiwa kwa lengo hili”.
Akifafanua Kardinali mteule Silvano Maria Tomasi, juu ya roho yake ilivyo kufuatia na jukumu hili alilokabidhiwa Kardinali Mteule amesema “Mimi ni kama punda anayevuta gari. Natumaini ninaweza kufanya kazi ambayo ni muhimu. Baba Mtakatifu amenikabidhi jukumu hili, kiukweli nitajitahidi kufanya jukumu hili kuwa muhimu kwa shirika la Malta na kutimiza matakwa ya Baba Mtakatifu. Ninaipenda sana Shirika hili kwa sababu kiukweli lina historia tukufu na, kwa njia fulani, mimi ni mshiriki wa Shirika hili kwa sababu nilifanya kazi zamani, na kwa mahitaji ya Shirika mimi ni msimamizi wa Kanisa la Msalaba Mkuu. Kwa hivyo nina hakika kwamba kwa mapenzi mema ya wote, tunaweza kuchukua hatua mbele na kutekeleza kweli mageuzi ambayo Baba Mtakatifu anataka”, amesema Kardinali mteule Silvano Maria Tomasi.