Tafuta

2020.10.21 Salam ya Papa kwa mahujaji na waamini waliofika katika katekesi yake. 2020.10.21 Salam ya Papa kwa mahujaji na waamini waliofika katika katekesi yake. 

Papa akumbusha siku ya Mtakatifu Yohane Paulo II na utume wa mkristo ni sala!

Baada ya katekesi yake Papa Francisko amekumbusha mwezi wa kimisionari na umuhumu wa sala kwa ajili ya ubinadamu,hasa kwa maskini.Vile vile amekumbusha kumbukumbu ya kiliturujia ya Mtakatifu Yohane Paulo II ambayo inafanyika kila tarehe 22 Oktoba.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Mara baada ya Katekesi, Jumatano tarehe 21 Okotb 2020, Papa Francisko amewasalimia mahujaji na waamini kwa lugha mbali mbali, na amekumbusha mwezi wa kimisionari na kusisitizia wito kwa wakristo wote kuhisi uwajibikaji katika kutangaza  na kueneza Ufalme wa Mungu  na kama ilivyo hata umuhimu  wa sala kwa ajili ya ubinadamu, hasa kwa maskini na kwamba utumewa kwanza wa kimisionari ni sala.

Mtakatifu Yohane Paulo II alikwa na ibada ya kina

Akiwageukia mahujaji na waamini wa lugha ya kipoland  amewakumbusha juu ya Mama Kanisa katika lirurjia ya tarehe 22 Oktoba inakumbuka Siku ya Mtakatifu Yohane Paulo II ambayo inaangukia katika mwaka wa Jubilei ya miaka 100 tangu kuzaliwa kwake. Yeye alikuwa mtu wa kiroho kwa kina, kila siku alikuwa akitafakari uso angavu wa Mungu katika liturujia ya sala na tafakari ya zaburi. Alikuwa akiwashauri wakristo wote kuanza na siku kwa kusifu Bwana kabla ya kuanza shughuli zozote ambazo daima siyo rahisi katika maisha ya kila siku na hivyo amewabariki.

Sala inafungua mlango wa maisha kwa Mungu

Kwa waamini wa lugha ya kireno, Papa Francisko ameakumbusha juu ya sala inavyo fungua mlango wa maisha yao kwa Mungu. Na kwamba Mungu anafundisha namna ya kutoka nje yao binafsi ili kwenda kukutana na wale walioko kwenye majaribu, kwa kuwapatia  wao faraja, matumaini na msaada. Kwa moyo wote awabariki na baraka ya Mungu.

21 October 2020, 15:26