Tafuta

2020.09.14 Kanisa Kuu la Manila nchini Ufilippino. 2020.09.14 Kanisa Kuu la Manila nchini Ufilippino. 

Papa kwa walimu katoliki nchini Ufilippino:elimu ishuhudie imani na maadili!

Papa Francisko ametuma ujumbe katika warsha ya walimu katoliki nchini Ufilipino akiwashauri wawe mashuhuda wa dhati wa imani.Elimu Katoliki lazima ifundishe sio tu kufikiria kwa uchambuzi,lakini pia malezi katika mafundisho ya Kikristo na maadili ameshauri Papa.Kwa kufanya hivyo itapelekea kuundwa kwa wanawake na wanaume walio tayari kuchukua majukumu ndani ya jamii na kushuhudia imani ya kweli kwa ulimwengu.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican

Kuwafundisha vijana na si tu kuwa wanafunzi bora tu, bali pia mashuhuda halisi wa imani. Ndiyo muhtasari wa mwaliko wa Papa  Francisko kwa waalimu katoliki wa Ufilipino waliounganika kuanzia  tangu 21 na watamaliza 25 Septemba, kwenye Warsha  yao ya kila mwaka. Tukio hilo limenadaliwa na Chama cha Elimu Katoliki cha Ufilipino (Ceap), kiungo ambao kinakusanya zaidi ya shule za Kikatoliki 1,500 nchini humo. Kwa sababu ya janga la corona, warsha  mwaka huu inafanyika moja kwa moja kupitia tovuti na kwenye mitandao ya kijamii kama vile facebook. Ushauri wa Papa umewafikia kupitia ujumbe uliosainiwa na Katibu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin. Ndani mwa ujumbe huo , Papa anakumbusha kwamba elimu Katoliki lazima ifundishe sio tu kufikiria kwa uchambuzi, lakini pia malezi katika mafundisho ya Kikristo na maadili.

Kwa kufanya hivyo itapelekea kuundwa kwa wanaume na wanawake ambao watakuwa tayari kuchukua majukumu makubwa ndani ya jamii na kushuhudia imani ya kweli kwa ulimwengu. Ujumbe wa kipapa ulisomwa na Padri Elmer Dizon, rais wa CEAP, kabla ya kuchaguliwa mwingine ambaye katika hotuba yake ya uzinduzi, hata hivyo  alisisitiza jinsi janga hilo lilivyokuwa na athari kubwa kwenye sekta ya elimu. Katika ujumbe wa Papa amesema katikati ya changamoto za sasa juhudi zinazoendelea zinafanywa ilibkuhakikisha kuwa shule Katoliki zinakuwa vichocheo vya mabadiliko.

Kwa upande wake, Monsinyo Roberto Calara Mallari, mjumbe wa Tume ya Maaskofu ya Katekesi na Elimu Katoliki, amehimiza kila shule kuwa ya ubunifu, ili kila mmoja apate njia za kusoma ambazo zinakidhi mahitaji ya wanafunzi wake. Akiendelea amesema na Chama cha Elimu Katoliki cha Ufilipino (Ceap) hakitazuiliwa na woga, lakini kitajitahidi kutenda kama mwongozo kwa wanafunzi na shule ambazo zinajitahidi katikati ya janga hilo. Hatimaye  amkumbusha  kwamba mada ya Kardinali Luis Antonio Tagle, Rais wa Baraza la Kipapa la  Uinjilishaji wa Watu, inatarajiwa  kutolewa siku ya  Ijumaa tarehe 25 Septemba 2020. Kama unataka kujiunga unaweza kutmia link hii hapa: https://www.facebook.com/CatholicEdPH/videos/977848552684485

23 September 2020, 14:26