Tafuta

Vatican News
2020.09.06 cardinali Marian Jaworski 2020.09.06 cardinali Marian Jaworski 

Papa Francisko:Kard.Jaworski alikuwa mwaminifu na shuhuda wa Injili!

Papa Francisko katika telegram yake anaungana kwa dhati na waamini wa Kanisa la Poland na Ukraine,kwa namna ya pekee Jimbo kuu la Krakow,Jimbo la Zamość-Lubaczów na Jimbo Kuu la Lviv katika sala za kuombea roho ya Marehemu Kardinali Marian Jaworski.Papa anamshukuru Bwana kwa maisha na huduma ya kitume kwa uaminifu na shuhuda wa Injili.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican.

Tarehe 8 Septemba 2020 Papa Francisko ametuma Telegram kwa Askofu Mkuu MAREK JĄDRASZEWSKI wa jimbo Kuu Katoliki la Krakow nchini Poland, akitoa salam za rambi rambi kufuatia na kifo cha Kardinali Marian Jaworski. Katika salamu hizo Papa Francisko anaonesha uchungu na maskitiko yake kwa habari za msiba huo. Anaungana kwa dhati katika sala za kuombea roho yake na waamini wa Kanisa la Poland na Ukraine, kwa namna ya pekee Jimbo kuu la Krakow, Jimbo la Zamość-Lubaczów na Jimbo Kuu la Lviv. Aidha Papa  anamshukuru Bwana kwa maisha na huduma ya kitume ya uaminifu na shuhuda wa Injili.

Jitahada za kitaaluma, falsafa, taalimungu na mtu wa sayansi

Papa kwa shukrani kubwa anamkumbuka Kardinali huyo kwa  jitihada zake za kitaaluma, jinsi ambavyo alithaminiwa kama mtu wa sayansi na mwalimu wa Taalimungu na Falsafa katika Vyuo Vikuu vya Kipapa huko Varsavia, Krakow na Lviv. Na zaidi amekuwa  kama Dekano na Mkuu wa kwanza wa Chuo cha Kipapa cha Taalimungu huko Krakow. Mtakatifu Yohane Paulo II mara nyingi alizungumzia juu ya mchango wake maalum na wa thamani katika maendeleo ya kisayansi.

Kuishi kwangu ni Kristo

“Mihi vivere Christus est”, yaani “kuishi kwangu ni Kristo” ndiyo ilikuwa kauli yake mbiu na namna yake ya kufikiria, kutathimini, kutimiza uchaguzi, kufanya maamuzi na kuelekeza matarajio tofauti ya utafiti, Papa Francisko amesisitiza. Katika mioyo ya wale waliomfahamu, alibaki kama mtu mwenye haki, mkweli, jasiri na ambaye alipenda Kanisa. Ameacha ushuhuda unaostahili wa bidii ya ukuhani, elimu, uaminifu katika Injili na uwajibikaji kwa jamuiya ya waamini.

Rafiki wa Mtakatifu Yohane Paulo II na mtoa sakramenti ya upako

Papa Francisko akiendelea kuelezea wasifu wake anasema, alikuwa ni rafiki mzuri wa Mtakatifu Yohane Paulo II. Alimsaidia katika kazi za huduma kiaskofu na upapa. Pia yeye aliweza kutoa sakramenti ya Upako kwa Papa aliyekuwa karibu ya kukata roho. Kama mfalsafa na mtaalimungu alishirikiana kwa dhati na Papa Mstaafu Benedikto XVI. Na kwa upande wa Papa Francisko anaelezea kile kinacho waunganisha ni tarehe moja ya Baraza la Makardinali kunako mwaka 2001, wakati wote wawili walipochaguliwa kuwa makardinali. Yesu Kristo Mwenye Huruma, anasema ambaye Kardinali Marian, kwa mwanga wake wa kumbu kumbu alijitoa maisha yake yote, ampokee katika utukufu wake.

Baraka ya Papa kwa washiriki wote wa Mazishi

Kwa kuhitimisha Papa Francisko anawageukia makardinali na washiriki wote wa liturujia ya mazishi, kwa maaskofu, familia ya marehemu, watu wote wa Mungu wa Kanisa la Poland na Ukraine,na washiriki wote katika kumsindikiza, anawapa Baraka yake kwa moyo wote kwa  Jina la baba, la Mwana na Roho Mtakatifu.

08 September 2020, 13:28