Tafuta

2020.09.06 Kardinali Marian Jaworski 2020.09.06 Kardinali Marian Jaworski 

Ukraine:Kardinali Marian Jaworski,ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 94

Kardinali Marian Jaworski alijenga Kanisa kwa upya nchini Ukraine na kuwa na urafiki mkubwa na Mtakatifu Yohane Paulo II ambapo mwaka 1998 alichaguliwa kuwa katika baraza la makardinali.Baada ya mgogoro wa vita ya Dunia alikuwa mstari wa mbele katika kuweka pamoja Kanisa lililokuwa limechanwa na utawala wa kikomunisti.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 5 Septemba ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 94, Kardinali Marian Jaworski, askofu Mstaafu wa Lviv ya Kilatino nchini Ukraine. Kwa mujibu wa Baraza la Maaskofu Poland, Marehemu huyo kwa kuwa aliishi miaka mingi nchini humo (1981- 1987) aliweza kujenga urafiki kindugu na Mtakatifu Yohane Paulo wa II ambapo aliwahi hata kumpatia sakramenti ya mpako wa wagonjwa. Ndiye alikuwa Gombera wa kwanza wa Taasisi ya Kipapa ya Elimu ya Taalimungu huko Crackow nchini Poland. Aliongozwa na nembo yake ya kiaskofu  kwenye  utume wake  isemayo “ kuishi kwangu ni Kristo” na ambayo ilikuwa kiongozi msingi wa maisha yake.

Kila mara akijibu aliyekuwa akimwomba ushauri, kwa waliokuwa wanaomba kuingia katika mafunzo ya ukasisi alijibu kwa  kumtaja mfano wa Mtakatifu Faustina Kowalska: “upendo mkuu wa pekee ni ule wa kumpatia Yesu tu”. Kufuatia kifo chake makardinali waliobaki ni 219 kwa ujumla na ambapo 122 ni wenye sifa ya kuchaguliwa na 97 hapana. Kardinali Jaworski alikuwa ni mmoja  wa kiongozi asili kutoka Ukraine ndani ya Baraza la Makardinali na kwa sasa Nchi hiyo inabaki bila  kuwa na mwakilishi.

Kardinali Marian Jaworski alizaliwa tarehe 21 Agosti 1926, huko  Lviv, na  kunako mwaka 1945, Marian Jaworski alijiunga na Seminari Kuu ya mji. Lakini kutokana na kuingiliwa na kikosi cha majeshi ya bolsceviche eneo hilo, alihamishiwa huko Kalwaria Zebrzydowska, nchini Poland.  Hapo aliendelea na masomo ya falsafa na Taalimungu. Alipewa daraja la Upadre tarehe 25 Juni 1950. Mwaka huo huo akapata magisterium ya Taalimungu katika Kitivo cha Kitaalimungu cha Chuo Kikuu cha Jaghellonica huko Crakow. Baadaye aliendelea na mafunzo katika Kitivo cha Kitaalimungu cha Krakow na kile cha Kifalsafa cha Chuo kikuu Katoliki cha Lublino. Kwa miaka mingi amekuwa Profesa ya Masomo ya Taalimungu katika Chuo Kikuu Katoliki cha Varsacia na kunako mwaka 1976, Profesa wa kawaida wa Kitivo cha Kitaalimungu Chuo Kikuu cha Kipapa Krakow. Mwaka 1985 akatunukiwa shahada ya heshima ya Chuo Kikuu cha Bochum, nchini Ujerumani.

Badala ya madhabahu, waliweka kitambaa cha sinema, badala ya madawati waliweka  vifaa vya kufanyia mazoezi. Yalikuwa ni makovu ya ujamaa wa kifalme kwenye makanisa ya pazia la nje. Kuna idadi kubwa isiyo na kipimo katika nchi za kisoviet, katika miaka ambayo udikteta wa Kremlin walitafuta kuangamiza kabisa imani waliona kama adui. Ukraine haikuwa tofauti  kwa maana hiyo ndiyo hali iliyomkabili hata Kadinali Marian Jaworski wakati anarudi katika mji wake  Lviv nchini Ukraine. Nchi ambayo alikuwa ameicha kwa miaka 46 wakati ni  mseminari kabla ya kuhama mara baada ya kuingia kwa majeshi ya kisovieti. Na kwa wakati huo aliingia akiwa tayari na mavazi ya uaskofu Mkuu katika mji Mkuu. Ilikuwa ni mwezi Mei 1991, ambapo vifusi vya ukuta  wa Berlin bado vilikuwa vinasikika arufu yake  na kwa Kanisa la Ukraine  kama hata kwa nchi nyingine za Ulaya Mashariki, ulikuwa ni mwaka wa sufuri, yaani kuanza na moja. Alisema inahitajika pia kujenga juu ya kifusi cha wale ambao hawajawahi kujitwisha Injili lakini akailipia mara nyingi gharama kubwa na  ngumu sana.

Akiwa kama kiongozi mkuu wa Kanisa la Kilatino huko Lviv Kardinali Jaworski alianza  hatua kwa hatua ya kuponyesha  majeraha  na aliweza kuhudhuria matamasha au michezo ya kuigiza mahali ilipokuwa na taratibu huku akianza kuadhimisha hata misa. Vile vile kulikuwa na haja ya kujenga makanisa kwa sababu sehemu nyingine hayakuwapo tena; kulikuwa na haja ya kuweka msimamo wa Uklero ili kuwarudisha na kuwahakikisha mustakabali wa wito mpya ambapo  tayari mwaka 1997 Seminari Kuu ya Lviv ilikuwa ni hali ya kweli. Mantiki hiyo hiyo ilikuwa pia ni kwa upande wa walei ambao shukrani kwa kuwatia moyo na  kuungwa mkono na Jiji kuu la Lviv waligundua kwa upya ya kuwa wanayo hadhi iliyoonyeshwa vizuri miaka mingi kabla ya Mtaguso, lakini hadi wakati huo ilikuwa imesongwa na ukandamizwaji.

Urafiki na  Wojtyla: Kwa  upande wa Kardinali Marian Jaworski,  Krakow ilikuwa  ni mji wa kiasili. Kwani hapo ndipo njia yake ilipitia kati yake na ile ya Karol Wojtyla, yaani Mtakatifu Yohane Paulo II. Kwa miaka kadhaa na  mara nyingi  wakati wa udaktari wake, katika hali ngumu, alimsaidia na kumkaribisha nyumbani kwake. Dhamana na heshima ambayo inakua zaidi bila kufifia wakati wa karibu   67 na baadaye Papa kuchaguliwa kuwa Kiongozi mkuu wa Kanisa na kuhamia Roma.

Miaka mitatu iliyopita, Rais wa Kipoland Duda alimpatia Tuzo ya Tai Nyeupe, tuzo ya juu zaidi ya kitaifa. Lakini siku zote yeye amekuwa ni mtu wa utamaduni mzuri na mchamungu, anakumbuka askofu mkuu wa Krakow Marek Jędraszewski. Alifurahia mamlaka na heshima kubwa kutoka kwa Mtakatifu Yohane Paul II. Kwa wastani alibaki na mshangao wa ushuhuda wa imani yake Kardinali kwa ajili ya huduma ya Kanisa hadi mwisho na kwa ajili ya unyenyekevu wake mkubwa.

07 September 2020, 15:11