Tafuta

Mbingwa Alex Zanardi anayepambana kati ya maisha na kifo mara baada ya ajali mbaya barabarani. Mbingwa Alex Zanardi anayepambana kati ya maisha na kifo mara baada ya ajali mbaya barabarani. 

Papa amwandikia barua Alex Zanardi.Asante kuwapa nguvu waliokuwa wamepoteza!

Katika barua ya iliyotangazwa kwenye gazeti la michezo kila siku,Papa Francisko anatoa maneno ya shukrani kwa mwanambingwa ambaye yupo anapambana kati ya maisha na kifo mara baada ya kupata ajali mbaya sana barabarani iliyotokea siku ya Ijumaa tarehe 19 Junu 2020.

Sr. Angela Rwezula – Vatican

Katika barua ya Papa Francisko anashukuru kwa namna ya pekee mwana michezo kwa uwezo wake wa kueneza ujasiri hata katika hali ngumu na mateso. Historia ya Alex Zanardi, dereva maarufu wa magari ya mashindano kwa kiitaliano ya (formula 1) ya zamani ambaye kwa bahati mbaya sana alipoteza miguu mara baada ya ajali mbaya kunako mwaka 2001, ni ushuhuda wa thamani ya kuanza tena kwa upyya na hivyo ni somo kwa ubinadamu kupitia ulemavu. Papa Francisko amejikita na tafakari hizi na ukaribu wa sala katika barua iliyomwandikia bingwa wa wa michezo ya kiolimpiki aliyelazwa hospitalini tangu Ijumaa iliyopita katika kitengo wagonjwa mahututi cha hospitali ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Maria alle Scotte huko Siena nchini baada ya ajali nyingine mbaya ya barabarani  iliyotokea tarehe 19 Juni katika manispaa ya Pienza.

Alex amewapa nguvu waliopoteza

Katika barua hiyo, Papa Francisko anamshukuru mwanariadha huyo hasa kwa uwezo wake wa kuhamasisha ujasiri hata katika hali ya mateso makubwa akiandika: Mpendwa Alessandro, historia yako ni mfano wa jinsi ya kuweza kuanza tena baada ya kuacha kwa ghafla. Kupitia michezo ulifundisha kuishi maisha kama waliomstari wa mbele na kufanya ulemavu kuwa somo la ubinadamu. Asante kwa kuwapa nguvu wale ambao walikuwa wamepoteza. Katika wakati huu wenye uchungu,niko karibu nawe, ninakuombea wewe na familia yako. Bwana awabariki na Mama yetu akulinde”.

Alex na hisani

Ajali iliyotokea wiki iliyopita ilikuwa ni katika wakati wa kufanya mashindano ya mshikamano, kwa mwezi mzima ambapo  Alex Zanardi alikuwa mstari wa mbele wa kampeni hata ya mnada wa “We run together”, yaani 'tunakimbia pamoja', iliyoanzishwa na Papa kwa lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya mahospitali ya di Bergamo na Brescia, Italia ambayo yanajikita mstari wa mbele kupambana na covid-19. Katika hisani hii Alex Zanardi aliweka hata jezi yake kwenye mnada aliyoshinda olimpiki kunako mwaka 2016 huko Rio de Janeiro.

24 June 2020, 14:17