Tafuta

Vatican News
Papa Francisko anazidi kuomba waamini wote kusali kwa ajili ya nchi ya Siria.Amesema hayo mara baada ya tafakari ya Katekesi tarehe 12 Februari 2020 Papa Francisko anazidi kuomba waamini wote kusali kwa ajili ya nchi ya Siria.Amesema hayo mara baada ya tafakari ya Katekesi tarehe 12 Februari 2020 

Papa Francisko:tusali kwa ajili ya Siria inayoteseka!

Papa Francisko ameomba kusali kwa ajili ya nchi ya Silia inayoteseka na ghasia, mizozo na ukosefu wa msimamo.

Na Sr. Angela Rwezaula –Vatican

Mara baada ya tafakari ametoa wito wa kuombea nchi ya Siria suala ambalo tayari alikuwa amekwisha sema mara baada ya Sala ya malaika wa Bwana Jumapili tarehe 9 Februari 2020. Katika siku hiyo Papa Francisko alikuwa amebainisha juu ya  habari zenye kuwa na  maumivu zinavyoendelea kufika kutoka kaskazini-magharibi mwa Siria, hasa kwa hali ya wanawake na watoto, ya watu waliolazimishwa kukimbia kutokana na kuongezeka kwa wanajeshi.

Papa akiwalekea hasa wahusika wa taasisi mbalimbali alisema: “Ninasasisha wito wangu kutoka moyoni kwa Jumuiya ya kimataifa na kwa wadau wote wanohusika ili kutumia vyombo vya kidiplomasia, majadiliano na mazungumzo, kwa kufuata Sheria ya Kimataifa ya Kibinadamu, ili kulinda maisha na hatima ya raia”. Kwa njia hiyp Papa Francisko aliomba waamini na mahujaji wote waliokusanyika kuomba kwa ajili ya nchi hiyo pendwa ya Siria inayosumbuka. " Salam Maria...."

12 February 2020, 13:00