Tafuta

Vatican News
Papa Francisko wakati wa tafakari ya Neno la Mungu kabla ya sala ya Malaika wa Bwana tarehe 16 Februari 2020 Papa Francisko wakati wa tafakari ya Neno la Mungu kabla ya sala ya Malaika wa Bwana tarehe 16 Februari 2020 

Papa Francisko:Lazima kutambua kudhibiti tamaa binafsi!

Yesu hatangui sheria zinazotazama matatizo bali anaelezea maana kamili na kuelekeza roho ambayo inatakiwa.Yeye anatoa sheria mpya kutoka katika uchambuzi wa kawaida wa sheria kuwa na mtazamo msingi wa kupokea Sheria ya moyo ambao ni kitovu cha nia,cha maamuzi,maneno na ishara za kila mmoja.Papa anakumbusha kuwa kutopenda jirani ni sawa sawa na kujiua binafsi na upendo wa Yesu unasaidia kushinda hisia za ubinafsi na tamaa.

Na Sr. Angela rwezaula – Vatican

Injili ya leo kutoka Matayo 5,17-37, inajikita katika  kuelezea juu ya hotuba za mlimani na kukabìliana na masuala ya utimilifu wa Sheria. Jinsi gani napaswa nitimize sheria, je nifanyeje. Ni kama Yesu anavyotaka kuwasaidia wasikilizaji wake kuhusu amri za Mungu zilizotolewa na Musa, akiwashauri kuwa na usikivu wa  Mungu anayetufundisha kuwa na uhuru wa kweli  na jukumu la Sheria. Ndiyo Mwanzo wa tafakari ya Papa ya Neno la Mungu, Dominika tarehe 16 Februari 2020 kwa mahujaji na waamini waliounganika katika uwanja wa Mtakatifu Petro kusali naye  Sala ya Malaika wa Bwana.

Papa Francisko akiendelea na tafakari amesema, hii ina maana ya kuiishi kama zana ya uhuru. “Tusisahau hili yaani kuiishi Sheria kama zana ya uhuru inayonisaidia kuwa huru zaidi. Inayo nisaidia nisiwe mtumwa wa tamaa na dhambi".  Papa Francisko amesema, "fikirieni vita na matokeo ya vita, fikirieni mtoto wa Siria aliyekufa juzi kwa sababu ya baridi, majanga mengi”.  Yote hayo ni tunda  la tamaa na watu wanaofanya vita na hawajuhi kudhibiti tamaa zao binafsi. Wanakosa kutimiza Sheria. Ikiwa ni kutawaliwa na vishawishi na tamaa huwezi kuwa bwana na kiongozi wa maisha binafsi, bali ni kukosa uwezo wa kutekeleza utashi na uwajibikaji.

Hotuba ya Yesu imegawanyika katika sehemu nne za ufafanuzi akisema “ mmesikia kwamba imenenwa; lakini mimi nawambia…”Misemo hii inataka kuelezea hali nyingi za maisha ya kila siku amesisitiza Papa na kuongeza kusema kwa mfano mauaji, uzinifu, talaka za ndoa  na viapo. Yesu hatangui sheria zinazo tazama matatizo hayo bali anaelezea maana kamili na kuelekeza roho ambayo inatakiwa. Yeye anatoa sheria mpya ile inayotoka katika uchambuzi wa kawaida ili sheria kuwa na mtazamo ulio msingi wa kuweza kupokea Sheria katika moyo ambao ni kitovu cha nia, cha maamuzi, cha maneno na ishara za kila mmoja wetu.

Kutoka moyoni ndimo chanzo cha matendo mema na yale mabaya. Kwa kupokea Sheria ya Mungu katika moyo ndiyo kutambua kuwa usipompenda jirani ni kama kujiua binafsi kwa namna fulani na wengine kwa sababu chuki, upendeleo na migawanyiko vinaua upendo wa kidugu ambao ni msingi wa uhusiano wote wa kibinafsi. Hii ni sawa sawa, Papa francisko anabainisha kwa kile ambacho amesema juu ya vita masengenyo kwa maana mdomo unaua. Kwa kupokea Sheria ya Mungu ndani ya moyo ni kutambua kuwa tamaa zinapaswa zidhibitiwe, kwa maana si kila kitu kinachotamaniwa unaweza kuwa nacho na siyo vema kungukia kwenye hisia za ubinafsi na kutawaliwa na tamaa. Sheria ya mungu inapopokelewa kutoka moyoni ni kuelewa kwa kuna  ulazima wa kuachana na mtindo wa maisha ya kutoa ahadi bila kutimiza na kama pia kuachana na tabia za kuapa uongo na kuweza  kuwa na uamuzi wa kutokuapa kabisa ili kuweza kuchukua jukumu la tabia kamili ya kuwa mkweli kwa wote.

Papa Francisko aidha amesema kwamba “Yesu anatambua vema jinsi ambavyo siyo rahisi kuishi Amri za Mungu na kwa mtindo huo kwa ujumla. Kwa njia hiyo anatupatia msaada wake wa upendo. Yeye alikuja  duniani si kwa ajili ya kutoa maisha na  utimilifu wa Sheria tu, bali Yeye  alikuja  kutupatia neema yake na ili sisi tuweze kufanya mapenzi ya Mungu, kwa kumpenda Yeye na ndugu. Yote yanawezekana kwa Neema ya Mungu! Na zaidi utakatifu siyo jambo jingine zaidi ya kutunza zawadi hii ya neema ya bure tuliyopewa na Mungu. Hii inatakiwa kukabidhi kwake Yeye, katika  neema yake, katika zawadi yake ya bure ambayo ametujalia na kuipokea  kwa mikono ambayo yeye mwenyewe anatusibiri daima ili jitihada zetu,  ulazima wetu wa jitihada uwezekane kusaidiwa kwa msaada wake na pia  kutulizwa na wema na huruma.

Yesu leo hii anataka tuendelee katika njia ya upendo ambao alituelekeza kwa  moyo. Hii ndiyo njia ya kufuata ili kuishi kama wakristo. Bikira Maria atusaidiè kufuata njia iliyopitiwa na Mwanae ili kufikia furaha ya kweli na kueneza kila mahali haki  na amani, amehitimisha Papa Francisko tafakari yake .

17 February 2020, 10:08