Tafuta

Vatican News
Tarehe 27 Januari ni siku ya kumbukumbu ya miaka 75 tangu kukombolewa kwa kambi la maangamizi makuu ya wayahudi huko  Auschwitz Birkenau Tarehe 27 Januari ni siku ya kumbukumbu ya miaka 75 tangu kukombolewa kwa kambi la maangamizi makuu ya wayahudi huko Auschwitz Birkenau 

Papa akumbuka siku ya maangamizi makubwa ya Auschwitz!

Papa amekumbuka miaka 75 ya kukombolewa kambi ya maangamizi makubwa ya Auschwitz-Birkenau,anawaalika waamini kusali ili kila mmoja apinge tukio hili.Amekumbusha Siku ya ukoma Duniani na pia kuwakumbuka waathirika wa mlipuko wa virus nchini China wakati wa sala ya Malaika wa Bwana;ikiwa ni Dominika ya Kwanza ya Neno la Mungu anawaomba kuwa na imani katika Neno la Kristo na kujifungulia katika huruma ya Baba na kuacha kubadilisha na neema ya Roho.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Mara baada ya Tafakari ya Neno na Sala ya Malaika wa Bwana, Papa Francisko amekumbusha juu ya maadhimisho ya kumbu kumbu ya miaka 75 tangu kukumbolewa kwa kambi ya maangamizi makuu ya huko Auschwitz-Birkenau, ambayo imekuwa ishara ya mahuaji ya  kiyahudi. Mbele ya janga hili lisilo la kibinadamu, amesema Papa “hazikubaliki zile sintofahamu, hivyo ni muhimu kufanya kumbu kumbu na  tarehe 27 Januari kila mmoja anakumbushwa  kusali kwa hilo akipinga suala hili lisirudiwe tena”. amesema Papa.

Kujifungulia katika huruma ya Baba

Papa Francisko akikumbusha juu ya Dominika ya Kwanza ya Neno la Mungu kwa mahujaji na waamini wote waliokusanyika katika uwanja wa Mtakatifu Petro Vatican tarehe 26 Januari 2020 wakati wa tafakari yake kabla ya sala ya Malaika wa Bwana, amejikita juu ya Injili ya siku ya ya Jumapili ambayo ilikuwa inajikita juu ya kuanza kwa Utume Yesu kwa watu wote. Alianzia Galilaya katika eneo la pembezoni, ukilinganisha na Yerusalemu, na ambalo lilikuwa linatazama vibaya kutokana na mchanganyiko wa wapagani, lakini Yesu alianzia hapo kuhubir na kutangaza maneno haya: “Tubuni kwa kuwa Ufalme wa Mbingu unakaribia”

Mahubiri hayo Papa Francisko amebainisha kuwa ni kama yenye nguvu ya mwanga ambao inapitia katika giza. Kuja kwa Yesu ambaye ni mwanga wa ulimwengu, Mungu Baba amejionesha ubinadamu wake wa ukaribu na urafiki, uliotolewa bure, licha ya kwamba sisi kutostahili. Na hizi ndizo zawadi za kutunza anaeleza Papa Francisko. Mara nyingi inajionesha kuwa na ugumu wa kubadili maisha, kuacha njia za ubinafsi, za ubaya, kuacha njia za dhambi kwa sababu zinajikita katika mchakato wa uongofu binafsi tu na kwa njia ya nguvu binafsi na siyo kwa katika njia ya Kristo na Roho. Lakini kumfuasa Bwana, hakuishii katika nguvu binafsi, hapana. kwa kuamini hilo Papa ameongeza kusema, inaweza ikawa hata dhambi ya ukiburi. Kumfuasa Bwana hakuwezi kuishia na nguvu binafsi , badala yake lazima ufafanuiliwe kwa njia ya ufunguzi wazi katika imani ya moyo na katika akili ya kupokea Habari Njema ya Yesu. Hili ndilo Neno la Yesu, Habari Njema ya Yesu, yaani Injili ambayo inabadili ulimwengu na mioyo! Sisi tunaitwa zaidi kuamini Neno la Kristo na kujifungulia katika huruma ya Bwana na kuacha tubaidilishwa kwa neema ya Roho Mtakatifu.

Kutangaza uhuru wa kweli

Kwa kufanya hivyo Papa Francisko  anakumbusha kuwa, ndiyo kuanza mchakato wa kweli wa uongofu. Na ndiyo sawa na ilivyo watokea mitume wa kwanza. Mkutano na Mungu yaani mwalimu, kwa mtazamo wake, kwa neno lake, aliwapa msukumo wa kumfuata na kubadili maisha kwa kijikita kwa dhati katika huduma ya Ufalme wa Mungu

Kufuata nyayo za Mwokozi

Watu wote Papa Francisko anahitimisha, wanaalikwa kuwa wajumbe wa Neno la Mungu: “Kukutana kuna shangaza hajabu na ni uamuzi wa kweli na Yesu ambao ulitoa mwanzo wa wafuasi kutembea, kuwabadili na kuwa watangazaji na mashuhuda wa upendo wa Mungu kwa watu wake. Kuiga mifano ya wajumbe hao wa shauku kubwa ya Neno la Mungu , kila mmoja anaweza kweli kuanza hatua moja  ili kuelekea katika nyayo za Mwokozi na hatimaye kuwapa matumaini  wenye kiu”.

Siku ya ugonjwa wa Ukoma

Papa Francisko amekumbusha pia kwamba: “ leo inaadhimishwa Siku ya ugonjwa wa Ukoma Ulimwenguni” Tuko karibu na watu wote waliathiriwa na dalili hizi za Hansen na wale wote kwa namna nyingine wanaowasadia wagonjwa hao”. Mwaka huu umefikia toleo la 67 na ambalo linabeba kauli mbiu: "Usiwepo kamwe ukosefu wa haki, ubaguzi, ukoma ulimwenguni".

Ukaribu wa wagonjwa kwa mlipuko wa virus uliosambaa nchini China

Papa Francisko katika kuendelea amekumbusha hata ukaribu na watu wagonjwa kwa sabau ya virusi ambavyo vimesambaa nchini China.” Ee Bwana uwapokee marehemu katika amani yako, uwafariji familia na kuwasaidia katika jitihada za Jumuiya ya nchi ya China ambao wanaendelea kupambana na mlipuko huo”

Vijana wa Chama Katoliki

Papa Francisko amesalimia vijana wengi wasichana na wavulana wa Chama katoliki nchini Italia walitoka katika maparokia na shule katoliki za Jimbo la Roma, anasema wamefika wakiwa katika msafara wa amani. Watoto wawili wameweza kusoma ujumbe wao wakiwakilisha vijana wote na baadaye wakatupa mapuzo juu yenye rangi nyeupe na njano. Katika ujumbe wao wanasema, wamefika hapo kwa ajili ya kupaza sauti ya kutaka amani katika mji wao na katika dunia nzima. Wamekuja katika Dominika ya kwanza ya Neno la Mungu ili watu wote waweze kujika katika usikivu wa thamani ya Neno la Mungu linalobeba nafasi kubwa ya maisha ya kila mtu. Na mwaka huu kwa upande wao utakuwa ni kwa ajili ya mambo makuu na matarajio yao ya furaha.

27 January 2020, 09:33