Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu katika tafakari yake amekumbusha maana ya ujasiri wa kushuhudia Injili Baba Mtakatifu katika tafakari yake amekumbusha maana ya ujasiri wa kushuhudia Injili 

Baba Mtakatifu:Mfuasi wa Yesu siyo mtumwa wa hofu ni shuhuda wa tumaini!

Bwana anatualika kushirikiana katika ujenzi wa historia na kugeuka kuwa wahudumu wa amani na ushuhuda wa matumaini katika wokovu na ufufuko ujao.Ni maneno ya tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko kabla ya sala ya malaika Bwana.Mitume wa Kristo lazima wawe na mtazamo wa huruma ya Mungu katika matukio ya kibinadamu yanayosukana na wema na ubaya.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Injili ya inawakilisha maneno ya Yesu kuhusu mwisho wa nyakati katika Injili ya (Lk 21,5-19). Yesu alisema maneno hayo akiwa mbele ya hekalu la Yerusalemu, jengo ambalo lilikuwa linapendeza machoni pa watu kwa sababu ya ukubwa wake na mapambo yake.  Lakini Yesu anatabiri kwamba uzuri huo wote na ukuu wake hautabaki jiwe juu ya jiwe bila kuharibika. Uharibifu wa hekalu uliotangazwa na Yesu siyo sura kubwa ya mwisho wa historia. Kwa hakika mbele ya wasikilizaji ambao wanataka kujua ni lini hayo na ishara gani zitakazo onekana, Yesu anajibu kwa kutumia lugha ya mwisho wa dunia inaytumiwa katika Biblia. Ndiyo mwanzo wa tafakari ya Baba Mkatifu Francisko kabla ya sala ya Malaika wa Bwana Jumapili 17 Novemba ikiwa Mama Kanisa anaadhimisha Kilele cha Siku ya Maskini duniani, inayoongozwa na kaulimbiu “Matumaini ya wanyonge hayatapotea milele”  kutoka katika zaburi ya  (Zab. 9:19).

Yesu anatumia matukio mawili ya majanga na uhakika wa matumaini

Baba Mtakatifu akiendelea na tafakari amesema, Yesu alitumia sura mbili zinazo tofautiana, ya kwanza ni matukio ya kuleta hofu kama vile majanga, vita, njaa, tetemeko na mateso (Lk 21,9-12). Na sehemu nyingine ni ile ya uhakika, kwa maana anasema: “lakini hata unywele mmoja wa vichwa vyenu hautapotea” ( Lk 21,18). Sehemu ya kwanza Baba Mtakatifu anasema ina mtazamo wa hali halisi juu ya historia ambayo inajikita katika majanga hata katika vurugu na ghasia zinazoikumba kazi ya uumbaji na nyumba yetu ya pamoja, hata katika familia ya binadamu anayeishi na jumuiya ya kikristo yenyewe. “Tufikirie vita vingi leo, na  njaa leo hii”.  

Tabia ya matumaini katika Bwana

Sura ya pili inajikita kuonesha uhakika wa Yesu anaye wanaonesha hali ambayo mkristo anapaswa kuwa nayo ya kuishi historia ambayo leo  hii inajionesha kuwa na tabia na kutumia nguvu na misigano. Hii ni katika tabia ya matumaini kwa Mungu ambayo inasaidia kutotishika na matukio ya majanga. Na badala yake  ni fursa ya kutoa ushuhuda ( Lk 21,13). Wafuasi wa Kristo hawawezi kubaki watumwa wa hofu na huzuni; wanaalikwa  kuiishi historia na kuweka pembeni nguvu za ubaya zinazo haribu, kwa uhakika kwamba, anayesindikiza matendo yake ya wema daima ni Mungu na anayehakikisha uhuruma yake Bwana. Hiyo ndiyo ishara msingi ambayo Ufalme wa Mungu unatufikia na ambao upo unakaribia kutimilizika katika dunia kama Mungu anavyotaka. Ni yeye ambaye anapeleka maisha yetu na anajua siku ya mwisho wa mambo yote na matukio yote.

Bwana anatualika kushirikiana naye ili kujenga historia

Bwana anatualika kushirikiana Naye katika kujenga historia na kuwa pamoja naye kama wahudumu wa amani na ushuhuda wa maisha katika wakati ujao wa wokovu na ufufuko. Imani inaufanya tutembee na Yesu katika njia mbaya za dunia hii, kwa kuwa na uhakika kuwa nguvu ya Roho inashinda nguvu za ubaya na kuweka msukumo wa nguvu ya upendo wa Mungu. Upendo ni mkuu, upendo unazidi nguvu ya ubaya. Upendo una nguvu kwa sababu ni Mungu. Baba Mtakatifu Francisko anasema, kuna wafiadini wakristo hata wa  nyakati zetu ambao  ni zaidi ya wafiadini wa wakati ule, licha ya kuteseka, hao ni wanawake na wanawaume wa amani. Wao wanatukabidha urithi wa kutunza na kuonja Injili ya upendo na huruma. Hiyo ndiyo tunu zaidi ya thamani ambayo tuliyopewa na ushuhuda wa kweli ambao tunaweza kuutoa kwa ndugu zetu. Tunaweza kuutoa  upendo dhidi ya chuki, msamaha dhidi ya maudhi. Ndiyo Baba Mtakatifu anakiri kwamba tunauhisi uchungu, lakini ni lazima kusamehe kwa moyo. Na tunapohisi kuwa hatuchukiwi, tusali kwa upendo kwa ajili ya wale wengine wanaochukia. Kwa maombezi ya Mama Bikira Maria awalinde katika safari ya imani ya kila siku ya kumfuasa Bwana anayeongoza historia, amehimisha Baba Mtakatifu.

Mwenyeheri mpya Padre Emilio Moscoso

Mara baada ya sala ya malaika wa Bwana, kwa waamini na mahuhaji wote waliofika katika uwanja wa  Mtakatifu Petro Vatican, Baba Mtakatifu Francisko amekumbusha kuwa Jumamosi tarehe 16 Novemba huko Riobamba, nchini  Ecuador, ametangazwa mwenyeheri Padre Emilio Moscoso, mfiadini, na mwanashirika wa Kijesuiti (SJ) aliyeuwawa kunako mwaka 1897 katika hali mbaya ya dhidi ya mateso ya Kanisa katoliki nchini humo. Mfano wake  wa unyenyekevu kitawa, mtume wa sala na mwalimu wa vijana, usaidie katika safari ya imani na ushuhuda wa kikristo. Baba Mtakatifu ameomba kupigiwa makofi mwenye heri mpya …

Siku ya Maskini duniani

Leo hii tunaadhimisha Siku ya Maskini duniani ambayo imengonzwa na mada kutoka katika zaburi isemayo “Matumaini ya wanyonge hayatapotea milele” (Rej. Zab. 9:19). Mawazo ya  Baba Mtakatifu yamewaandea majimbo, na maparokia duniani kote walioanzisha mshikamano kwa ajili ya kutoa matumaini ya dhati watu wenye kuhitaji. Aidha anawashukuru madaktari na wauguzi ambao wamejitoa kutoa huduma kwa siku hizi katika Kituo kilicho wekwa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro kwa fursa ya Siku hii. Anawashukuru wote kwa kuanzishwa mambo kama hayo kwa ajili ya watu wanaoteska na hiyo lazima kushuhudia umakini na ambao haupaswi kukosekana mbele ya kaka na dada. Aidha Baba Mtakatifu amethibitisha kuwa muda mfupi kabla ameona baadhi ya takwimu kuhusu umaskini ambazo zinatia huruma, hasa kuona sintofahamu ya kijamii dhidi ya maskini…

Salam kwa mahujaji

Vile vile Baba Mtakatifu Francisko amewasalimia mahujaji wote kutoka Italia na sehemu zote duniani kwa namna ya pekee Jumuiya ya wana Ecuador wanaoishi Roma wakiwa wanaadhimisha siku ya Bikira Maria wa  Quinche; waamini wa  New Jersey wa  Toledo, Hispainia na wengine wengi.

Ziara ya Thailand na Japan

Baba Mtakatifu amehimishisha kwa kuwajulisha waamini na mahujaji wote kuwa Jumanne anaanza ziara yake ya kitume ya kwenda nchini Thailand na Japan. Kwa maana hiyo anawaomba wamwombee safari yake. N amewatakia mlo mwema na kuwaomba wasali kwa ajili yake. https://www.vaticannews.va/sw/vatican-city/news/2019-11/hija-papa-francisko-thailand-kardinali-charles-maung-bo-fabc.html

 

17 November 2019, 14:01