Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu alikutana na Timu ya Taifa ya mpira Italia na kuwahimiza juu ya huruma  na  kazi ya uumbaji Baba Mtakatifu alikutana na Timu ya Taifa ya mpira Italia na kuwahimiza juu ya huruma na kazi ya uumbaji   (ANSA)

Timu ya Taifa Italia:ipo thamani ya mpira wa vitambaa chakavu!

Kabla ya kuanza maadhimisho ya Misa Takatifu kwa ajili ya kuwatangaza watakatifu wa Kanisa wapya tarehe 13 Oktoba 2019,Baba Mtakatifu Francisko alikutana na Kikundi cha Timu ya Kitaifa ya mpira wa miguu nchini Italia ambao Jumamosi 12 Oktoba 2019 katika uwanja wa Mpira mjini Roma walicheza na Timu ya mpira ya Ugiriki wakashinda kwa mabao 2 kwa bila.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na kusalimiana na kikundi cha Timu ya Taifa ya  wanamichezo wa mpira wa miguu nchini Italia, tarehe 13 Oktoba 2019, kabla ya kuanza maadhimisho ya Misa Takatifu kwa ajili ya kuwatangaza watakatifu wa 5  wapya wa Kanisa. Akizungumza nao amewashukuru kumtembelea hasa ujasiri wao  mara baada ya mchezo wao Jumamosi 12 Oktoba katika uwanja wa Mpira mjini Roma wakipambana na  Timu ya mpira kutoka nchini Ugiriki na wakashinda kwa mabao 2 kwa bila. Baba Mtakatifu amesema wamefika kwa haraka wakiwa wanaonekana na roho ya ibada. Aidha ameeleza kwa jinsi gani kabla wametembelea watoto katika Hospitali ya Bambin Gesù, ambapo pale wamewezeza kuonesha upendo wa kila mmoja ambao mara nyingi unafichika ndani mwao, lakini mbele ya watoto daima unajitokeza nje.

Baba Mtakatifu amebainisha kuwa  wakati anaingia katika ukumbi  kushoto kwake  ameona mchoro wa ubunifu unaohusu kazi ya uumbaji wa dunia. Na hivyo amewashauri watakaopoondoka wautazame kwa upya. Akiataka kuelezea mchoro huo amesema ni mikono ya Mungu ambayo  inafanya kuzaliwa mtoto. Msanii wakati wa kuchora alifikiri kila  mtoto anayezaliwa kwamba ni kazi ya  uumbaji. Daima  ni uumbaji hata wakati mwingine kiumbe anapokuwa na itilifu, kuna uchungu wa watoto, na kama wao walivyo fanya uzoefu wa ziara hiyo kwa watoto, pia wanafahamu hata wengine, jinsi ilivyo mara nyingi  msalaba wa familia. Lakini yote hayo ni mikono ya huruma, anasisitiza Baba Mtakatifu Francisko. Watoto wanaelewa lugha na kuwa na karibu daima kwa njia ya huruma itumikayo. Ni lugha ya upendotu  ambayo  mtoto anaweza kuelewa. “Ninatambua jinsi mlivyokuwa nao. Ninawashukuru kwa ishara hiyo ya upendo. Asante”

Baba Mtakatifu aidha amegusia juu ya zawadi waliyo wapatia watoto hao. Zawadi hiyo ni mpira na kwamba, wamewapatia jambo zuri sana, ameongeza kusema kwa kutoa mfano kuwa hata Mtakatifu Don Bosco alikuwa anasema hivyo! jinsi gani ya kuwafanya watoto wawe na furaha, kwa  jinsi gani ya kuwakusanya watoto? Nyakati zile katika mtaa wa kimasikini na uliobaguliwa, alitupa mpira barabarani na mara watoto walikusanyika”. Mpira una kivutio. Baba Mtakatifu Francisko akiendelea na hisotria hii kuhusu mpira amekumbuka kuwa, kulikuwa na kiwanja kidogo sana, mita chache karibu na nyumbani kwao. Pale walikuwa wanacheza japokuwa si wakati wote walikuwa na mpira kwa sababu wakati ule mpira ulikuwa wa ngozi na ulikuwa ni gharama. Hapakuwapo bado na plastiki na ile ya mipira haikuwapo… kulikuwapo na mipira ya vitambaa chakavu. Hata kwa njia ya mpira wa vitambaa chakavu unafanya miujiza. Aidha amekumbua kwamba,“mtoto mmoja nchini Msumbiji nikiwa katika ziara aliniletea mpira wa vitambaa chakavu. Ndiyo ndiyo mpira tuliokuwa tunacheza hivyo.  Ni muhimu kuwa na mpira pale na pale wao wanacheza ndani yake.

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea na  mazungumzo yake na wachezaji wa Timu ya Kitaifa ya mpira wa miguu amesema, kuna filamu  moja ya Argentina yenye kichwa “Pelota de trapo”, yaani “ mpira wa vitambaa chakavu, ambao unafanya kuona roho ya ajabu  na kama alivyofafanua haya  Rais wao (FIGC) kuwa “hata kwa njia ya mpira wa vitambaa chakavu”. Filamu iliyotengenzwa kwa miaka ya 40 ilikuwa nzuri sana na ya kimashairi. Baba Mtatifu akihitimisha amewaachia kazi mbili ya kisanaa ya kutafakari kwa kina, kwamba ya mchoro kuhusu huruma ya Mungu katika uumbaji wa kila mtu na ya mtoto; pili ile inayohusu mpira wa kitambaa chakavu katika filamu. Labda wao wanaweza kupendelea kuitazama, amesbainisha.  Kadhalika amewashukuru sana  tena kwa ishara hiyo ya watu wakubwa na wenye uwezo wa kuwa na huruma na  kukaribia watoto. Na labda mmoja wapo kati yao , ameweza kulia. Huruma ya Mungu haisaliti kamwe! Mtu anafanya ishara ya huruma na baadaye anajificha na kulia kwa sababu ndiyo hivyo! Maisha ndiyo hivyo. Na ndiyo ishara zinazofanya vizuri maisha na ndizo ishara zinazopelekea kuleta afya bora!

 

14 October 2019, 14:44