Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko baada ya katekesi amewwza kuwasalimia watu  wote mahujaji kama vile wagonjwa, vijana wanandoa wapya Baba Mtakatifu Francisko baada ya katekesi amewwza kuwasalimia watu wote mahujaji kama vile wagonjwa, vijana wanandoa wapya  (Vatican Media)

Papa:Pasaka inakaribia na tukiishi kipindi hiki kwa ukamilifu!

Baba Mtakatifu mara baada ya tafakari ya katekesi yake kwa waamini na wahujaji waliofika katika uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican kuungana naye tarehe 10 Aprili 2019 amewasalimia wote na kuwahimiza kujiandaa mioyo yao ili kuishi kipindi cha Pasaka kwa ukamilifu.

Baba Mtakatifu mara baada ya tafakari ya katekesi yake kwa waamini na wahujaji waliofika katika uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican kuungana naye tarehe 10 Aprili 2019 amewasalimia.  Hata hivyo katika tafakari  imekuwa ni mwendelezo wa sala ya Baba yetu, baada ya sehemu ya  kuomba Mungu Mkate wa kila siku, na kujikita  leo hii na sala ya maombi kwa Bwana kuhusu msamaha wa dhambi kama alivyo fundisha Yesu: “utusamehe makosa yetu kama tunavyo wasahamehe waliotukosea” (Mt 6,12).

Salam kwa mahujaji na waamini,  vijana, wagonjwa na wanandoa wapya

Ametoa salam kwa mahujaji wote kutoka pande zote za dunia. Bila kuwasahau vijana, wazee,wagonjwa na wanandoa wapya. Kadhalika amewasalimia watawa wanao udhuria Kozi ya Umoja Wamama wakuu wamashirikia ya kitawa nchini Italia na Kitivo cha Kipapa cha elimu ya sayansi.  Aidha na kuwakumbusha kuwa,“tunakaribia kuhitimisha safari ya Kwaresima. Mwanga na faraja za Pasaka ya Bwana zinakaribia! Tuombe, ili kuwa na hisia za Kristo  na kuishi kwa ukamilifu katika siku za mateso na utukufu wake”.

 

10 April 2019, 13:40