Tafuta

Vatican News
Katika Jumapili ya Matawi Papa amekumbuka maaskofu  katika majimbo yao wakiadhisha Siku ya vijana duniani kote Katika Jumapili ya Matawi Papa amekumbuka maaskofu katika majimbo yao wakiadhisha Siku ya vijana duniani kote   (Vatican Media)

Papa Fancisko amewaomba vijana wasali Rosari kwa ajili ya amani na kusoma wosia "Christus vivit"

Kabla ya Sala ya Malaika wa Bwana,Baba Mtakatifu Francisko amewasalimia vijana wanaoadhimisha Siku ya 34 ya Vijana kijimbo duniani kote na kuwaomba wasome maelekezo ya wosia wa "Christus vivit".Na hatimaye ametoa zawadi ya Rosari na kuwaomba wasali kwa ajili ya amani kwa namna ya pekee kuombea nchi Takatifu na za Mashariki

 Na Sr Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 14 Aprili 2019 Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya  maadhimisho ya Jumapili ya Matawi, ikiwa ni mwanzo wa maadhimisho ya Juma Kuu Takatifu, Kanisa linapofanya kumbu kumbu ya Mateso, kifo na Ufufuko wa Kristo na siku ambayo inakwenda sambamba na Maadhimisho ya XXXIV ya Vijana Duniani na ambayo imeadhimishwa kijimbo, Baba Mtakatifu Francisko amewasalimia wote wanaoshiriki  katika maadhimisho hayo, lakini pia hata waliokuwa wakifuata kwa njia ya vyombo mbalimbali vya mawasiliano. Baba Mtakatifu amewafikiria hata vijana wote wakiwa karibu na maaskofu wao katika majimbo wakiadhisha Siku ya vijana katika kila jimbo duniani kote.

Vijana someni Wosia wa Christus vivit

Baba Mtakatifu Fancisko akiwageukia vijana katika maadhimisho hayo anawaalika waishi kila siku kwa mujibu wa maelekezo ya Wosia wa hivi karibuni wa kitume Christus vivit yaani Kristo anaishi, na kwamba ni tunda la Sinodi ambayo iliwahusisha hata vijana wenzao. Katika waraka huo kila mmoja anaweza kupata neno lenye kuzaa katika maisha binafsi na kwa ajili ya kukua katika safari ya imani na huduma kwa ndugu.

Zawadi ya Rosari

Kwa mantiki ya Jumapili hiyo Baba Mtakatifu ametoa  zawadi kwa wote waliofikia katika uwanja wa Mtakatifu Petro, Rosari ya mti wa mizeituni ambazo zilitengenezwa katika nchi Takatifu, wakati wafursa ya  Mkutano wa Vijana duniani huko Panama mwezi Januari  na kwa ajili ya Siku ya hii. Na kwa maana hiyo Baba Mtakatifu amependa kupyaisha “wito” wake kwa vijana kusali Rosari, kwa ajili ya amani, kwa namna ya pekee, amani katika  Nchi Takatifu na nchi zote za Mashariki. Amehitimisha akiomba wote wamwelekee Bikira Maria ili aweze kusaida kuishi vema Juma Takatifu.

14 April 2019, 13:00