Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu akiwa katika maungamo tarehe 29 Machi 2019 katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Baba Mtakatifu akiwa katika maungamo tarehe 29 Machi 2019 katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro  (Vatican Media)

Papa:Liturujia ya kitubio inatoa uhuru na kumkomboa mdhambi!

Hata mwaka huu Liturujia ya Sakramenti ya toba katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro imeongozwa na Baba Mtakatifu Francisko.Baada ya liturujia hiyo,alikuwa wa kwanza kupiga magoti na kuungama.Baadaye naye aliwaungamisha waamini 11.Kitovu cha mahubiri yake ni msamaha wa Mungu,ambayo ni ishara ya upendo wake zaidi ya dhambi ya mtu

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katika liturujia ya Sakramenti ya toba tarehe 29 Machi 2019, Baba Mtakatifu Francisko tafakari yake imekazia juu ya msamaha wa Mungu, ishara ya upendo mkuu wake zaidi ya dhambi atendazo. Akianza tafakari anasema baada ya Injili iliyosoma kuhusu mwanamke aliyefumaniwa, “ walibaki wawili tu, dhambi na huruma” ( Yh 33,5). Ndivyo Mtakatifu Agostino anamalizia  kama Injili  iliyosomwa. Wale waliotaka kumtupia mawe mwanamke au kumshitaki Yesu kutokana na Sheria, waliondoka hawakuwa na jambo jingine. Lakini Yesu alibaki. Alikabaki pale kwa sababu yule mwanake alikuwa ni mwenye thamani katika machoni pake. Kwake yeye kabla ya dhambi anakuwa mbele yake mdhambi. “ Mimi, wewe na kila mmoja yupo rohoni mwa monyo wa Mungu kabla ya makosa,kanuni za sheria, ya hukumu au kuanguka kwetu”. Na tuombe neema ya kuwa na mtazamo kama huo wa Yesu, tuombe kuwa na mtazamo wa maisha ya  kikristo, mahali ambamo badala ya dhambi tumwone mdhambi huyo upendo, kabla ya makosa yake na kabla ya historia yake.

Sakramenti ni ufunguo wa wokovu

Sakramento ni ufunguo wa wokovu, kwa yule ambaye anatufahamu, anatupenda, atuhukumu ili kuweza kuanza maisha mapya.Yesu na mwanamke aliyefumaniwa kusini hawakilishi sehemu tu ya sheria, bali ni hali halisi  ambayo inamzunguka. Kwa maana hiyo yeye alibaki pale akiwa kimya. Na wakati huo huo Yesu anatimiza mara mbili ishara za fumbo, kwani aliinama, akaandika kwa kidole chake katika ardhi (Yh 8,6.8). Baba Mtakatifu anaongeza kusema,“ hatujua aliandika nini  na labda halikuwa jambo muhimu; lakini umakini wa Injili unajikita kuzama suala  ambalo Yesu mwenyewe anaandika. Hii pia inakumbusha tukio la Mlima Sinai mahali ambapo Mungu aliandika maneno ya sheria katika meza kwa njia ya kidole chake. (Kum 31,18) Na ndivyo anafanya Yesu mwenyewe wakati huu. Na kuendelea kwa njia ya manabii, alikuwa ameahidi kutoandika  tena juu ya meza ya mawe badala yake  moja kwa moja katika mioyo (Yer 31,33) katika meza ya mwili wa mioyo yetu ( 2Kor 3,3).  Pamoja na Yesu, huruma ya Mungu imewadia sasa, ni kupindi cha kuandika katika moyo wa mtu, na ilia kutoa matumanini hakika kwa umasikini wa kibinadamu. Kwake yeye sheria siyo tu za nje na ambazo zinamfanya mtu aende mbali na Mungu, badala yake ni sheria ya Rohoni, inayoingia ndani ya moyo na kumwokoa. Ndivyo inavyokuja kwa mwanamke huyo anayekutana na Yesu na kuanza kuishi kwa upya. Yesu anamwambia Enenda zako; wala usitende dhambi tena” (Yh 8,11). Yesu kwa nguvu za Roho Mtakatifu anatukomboa na mabaya yaliyomo ndani mwetu, dhidi ya dhambi ambayo sheria ingeweza kuweka vizingiti na kuondoa.

Ubaya una nguvu na uwezo wa kulaghai unavuta na kuumiza

Ubaya una nguvu na uwezo wa kulaghai, unavuta na kuumiza. Ili kuondokana nao inatosha kufanya jitihada  na kuwa na moyo mkuu anasisitiza Baba Mtakatifu. Bila msaada wa Mungu lakini siyo rahisi kushinda ubaya. Na iwapo tunataka kujikomboa na ubaya, lazima kutoa nafasi kwa Bwana  anayesamehe na kutibu. Na zaidi anafanya hivyo kwa njia ya Sakramenti ya kitubio. Ni kwa njia ya msamaha wa dhambi Mungu anabadili kwa dhati mambo mapya ndani mwetu. Isaya amesema: ninafanya mambo yote mapya (Is 43,19). Msamaha unaruhusu kuanza upya na kutoa utambulisho mpya wa kila hatua katika maungamo. Kuupokea msamaha kwa njia ya padre ni uzoefu daima mpya wa asili na usiopingika. Unatufanya tuondokane na upweke wa dhambi zetu na washtaki zetu kama yule mwanamke katika Injili na kuinuka, kuwa na ujasiri kwa Bwana ambaye anatuwezesha kuanza upya maisha.

Walibaki wawili tu, mdhambi na huruma

Walibaki wawili tu, mdhambi na huruma. Je inabidi kufanya nini ili kuweza kukimbilia huruma, ili kushimda hofu ya kwenda kuungama? Baba Mtakatifu Francisko anawaalika kupokea wito wa Isaya asemaye “je! Hamjatambua sasa?”  (Is 43,19).Hii ina maana kuwa kutambua msamaha wa Mungu ni muhimu. Ingekuwa vizuri, baada ya maungamo, kila mmoja kubaki kama mwanake yule na mtazamo juu ya  Yesu ambaye amekupa uhuru. Na si katika dhambi zetu, bali kubaki katika huruma. Kutazama Msalaba na kusema kwa mshangao: “tazama mahali ambapo nimekwenda kushia na dhambi zangu. Na wewe sasa umezichukua. Hukuninyoeshea kidole, badala yake umenifungulia mikono yako na kunisamehe kwa mara nyingie tena”. Tuanzie katika maungamo na ili kurudisha tena sakramenti inayostahili katika maisha na katika maisha ya kichungaji!

Kufanya kumbu kumbu ya Mungu, kukumbuka upendo wake,ili kuonja upya amani

Baba Mtakatifu anashauri kufanya kumbu kumbu ya Mungu, kukumbuka upendo wake na ili kuonja kwa upya amani na uhuru ambao tumefanya uzoefu. Kwa maana huo ni moyo wa maungamo. Siyo dhambi tunazo ungama, lakini ni upendo wa Mungu tunao upokea na ambao daima tunauhitaji. Inawezekana kuwa na  duku duku kwamba hakuna haja ya kuungama, kwa maana dhambi ni zile zile. Lakini Bwana anatutambua, na anatambua kuwa mapambano ya ndani ni magumu,na jinsi tulivyo wadhaifu, wanaoanguka mara kwa mara kwa kutaka kutenda vibaya.  Walibaki wawili, dhambi na huruma. “Hata leo hii tunaweza kuanza upya  na kuoja huruma ya Mungu na ili tuweze kuwa huru na amani.

30 March 2019, 09:19