Baba Mtakatifu akiwa katika maungamo tarehe 29 Machi 2019 katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Baba Mtakatifu akiwa katika maungamo tarehe 29 Machi 2019 katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro 

Papa:Liturujia ya kitubio inatoa uhuru na kumkomboa mdhambi!

Hata mwaka huu Liturujia ya Sakramenti ya toba katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro imeongozwa na Baba Mtakatifu Francisko.Baada ya liturujia hiyo,alikuwa wa kwanza kupiga magoti na kuungama.Baadaye naye aliwaungamisha waamini 11.Kitovu cha mahubiri yake ni msamaha wa Mungu,ambayo ni ishara ya upendo wake zaidi ya dhambi ya mtu

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katika liturujia ya Sakramenti ya toba tarehe 29 Machi 2019, Baba Mtakatifu Francisko tafakari yake imekazia juu ya msamaha wa Mungu, ishara ya upendo mkuu wake zaidi ya dhambi atendazo mwanadamu. Akianza tafakari anasema baada ya Injili iliyosoma kuhusu mwanamke aliyefumaniwa, wao walibaki wawili tu, dhambi na huruma ( Yh 33,5). Na ndivyo Mtakatifu Agostino anamalizia  tafakari yake kuhusu Injili  iliyosomwa. Wale waliotaka kumtupia mawe mwanamke au kumshitaki Yesu kutokana na Sheria, waliondoka na hawakuwa na jambo jingine. Lakini Yesu alibaki. Alikabaki pale kwa sababu yule mwanake alikuwa ni mwenye thamani machoni pake. Kwake yeye alikuwa namwona mtu mbele yake kabla ya dhambi. Kwa maana hiyo, "Mimi, wewe na kila mmoja yupo rohoni mwa Mungu kabla ya makosa, kanuni za sheria, hukumu au kuanguka kwetu”. Na tuombe neema ya kuwa na mtazamo huo kama Yesu, tuombe kuwa na mtazamo wa maisha ya  kikristo, mahali ambamo  tuone kwamba upendo badala ya dhambi, kabla ya makosa yake na kabla ya historia yake.

Sakramenti ni ufunguo wa wokovu

Sakramento ni ufunguo wa wokovu, kwa yule ambaye anatufahamu, anatupenda, atuhukumu na  ili kuweza kuanza maisha mapya. Yesu na mwanamke aliyefumaniwa hawawakilishi tu sehemu ya sheria, bali ni hali halisi  ambayo inamzunguka mwanamke huyo. Kwa maana hiyo yeye alibaki pale akiwa kimya. Na wakati huo huo Yesu anatimiza mara mbili ishara za fumbo, kwani aliinama, akaandika kwa kutumia  kidole chake katika ardhi (Yh 8,6.8). Baba Mtakatifu Francisko anaongeza kusema,“ hatujuhi aliandika nini,  labda halikuwa jambo muhimu; lakini umakini wa Injili unajikita kuzama suala  ambalo Yesu mwenyewe anaandika. Vile vile tendo hili linakumbusha tukio la Mlima Sinai mahali ambapo Mungu aliandika maneno ya sheria katika meza kwa njia ya kidole chake. (rej. Kumb 31,18). Katika tendo hilo ndivyo anafanya Yesu mwenyewe wakati huu. Hata hivyo  kwa njia ya manabii, alikuwa ameahidi kutoandika  tena juu ya meza ya mawe, na  badala yake  kuandika moja kwa moja katika mioyo (rej. Yer 31,33), katika meza ya mwili wa mioyo yetu, ( 2Kor 3,3).  Pamoja na Yesu, huruma ya Mungu imewadia sasa, ni kupindi cha kuandika katika moyo wa mtu, ili kuweza  kutoa matumaini hakika kwa umasikini wa kibinadamu. Kwake yeye sheria siyo za nje tu  na ambazo zinamfanya mtu aende mbali na Mungu, badala yake ni sheria ya Rohoni, inayoingia ndani ya moyo na kumwokoa. Ndivyo ilivyomjia  mwanamke huyo anayekutana na Yesu na kuanza kuishi kwa upya. Yesu anamwambia "Enenda zako; wala usitende dhambi tena” (rej. Yh 8,11). Yesu kwa nguvu za Roho Mtakatifu anatukomboa na mabaya yaliyomo ndani mwetu, dhidi ya dhambi ambayo sheria ingeweza kuweka vizingiti.

Ubaya una nguvu na uwezo wa kulaghai unavuta na kuumiza

Ubaya una nguvu na uwezo wa kulaghai, unavuta na kuumiza. Ili kuondokana nao inatosha kufanya jitihada  pia kuwa na  moyo mkuu anasisitiza Baba Mtakatifu Francisko maana bila msaada wa Mungu, siyo rahisi kushinda ubaya. Na iwapo tunataka kujikomboa na ubaya, lazima kutoa nafasi kwa Bwana  anaye samehe na kutibu. Na zaidi anafanya hivyo kwa njia ya Sakramenti ya kitubio. Ni kwa njia ya msamaha wa dhambi Mungu anabadili kwa dhati mambo mapya ndani mwetu. Nabii Isaya amesema: "ninafanya mambo yote mapya", (Is 43,19). Msamaha unaruhusu kuanza upya na kutoa utambulisho mpya wa kila hatua katika maungamo. Kuupokea msamaha kwa njia ya Padre , anahimiza ni uzoefu daima mpya wa asili na usiopingika. Unatufanya tuondokane na upweke wa dhambi zetu na zaidi kwa  washitaki zetu kama yule mwanamke katika Injili na kuweza kuinuka, kuwa na ujasiri kwa Bwana ambaye anatuwezesha kuanza upya maisha!

Walibaki wawili tu, mdhambi na huruma

 Je inabidi kufanya nini ili kuweza kukimbilia huruma, ili kushinda hofu ya kwenda kuungama? Baba Mtakatifu Francisko, anawaalika kuupokea wito wa Isaya asemaye “je! Hamjatambua sasa?”  (rej. Is 43,19). Hii ina maana kwamba, kutambua msamaha wa Mungu ni muhimu. Anaongeza kusema kuwa:Ingekuwa vizuri, baada ya maungamo, kila mmoja kubaki kama mwanake yule na mtazamo juu ya  Yesu ambaye amekupa uhuru. Na si katika dhambi zetu, bali kubaki katika huruma. Kutazama Msalaba na kusema kwa mshangao wa kusema: “tazama mahali ambapo nimekwenda kuishia na dhambi zangu". "Na wewe sasa umezichukua"! Na hukuninyoshea kidole, badala yake umenifungulia mikono yako na kunisamehe kwa mara nyingine tena”. Hivyo basi, tuanzie katika maungamo na ili kurudisha tena sakramenti inayo stahili katika maisha na katika maisha ya kichungaji!

Kufanya kumbu kumbu ya Mungu, kukumbuka upendo wake ili kuonja upya amani

Baba Mtakatifu anashauri kufanya kumbu kumbu ya Mungu, kukumbuka upendo wake na ilikuweza  kuonja kwa upya amani na uhuru ambao tumefanya uzoefu. Kwa maana hiyo ni moyo wa maungamo. Siyo dhambi tunazo ungama, lakini ni upendo wa Mungu tunao upokea na ambao daima tunauhitaji. Inawezekana kuwa na  duku duku kwamba hakuna haja ya kuungama, kwa maana dhambi ni zile zile; Lakini Bwana anatutambua,na anatambua mapambano  ndani mwetu ya kuwa  ni magumu, anatambua jinsi tulivyo wadhaifu, wanao anguka mara kwa mara katika utashi wa kutenda vibaya.  Walibaki wawili, dhambi na huruma. Na hivyo: “Hata leo hii tunaweza kuanza upya  ili  kuonja huruma ya Mungu, na zaidi tuweze kuwa na uhuru na amani.

SAKRAMENTI YA KITUBIO
30 March 2019, 09:19