Tafuta

Vatican News
Misa ya Baba Mtakatifu Sacrofano Ijumaa 15 Februari 2019 Misa ya Baba Mtakatifu Sacrofano Ijumaa 15 Februari 2019  (Vatican Media)

Papa anawashukuru sana kwa kile wanachofanya!

Baba Mtakatifu kabla ya kuwaaga ili kurudi nyumbani amependelea kuwashukuru kila mmoja wao kwa kile wanachofanya,na kwamba ni hatua ndogo,lakini inayofanya safari kubwa ya historia hivyo waendelee mbele na wasiogope

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Baba Mtakatifu Francisko, kabla ya kuondoka, aliwasalimia watu wote wanaojikita katika hali halisi ya mapokezi ya  wahamiaji ambao wameunganika katika Jumuiya ya Domus huko Sacrofano Roma, akiwatia moyo wa kuendelea mbele na kuwakumbusha kuwa ni hatua ndogo inayofanya safari kubwa ya historia. Maneno yake: kabla ya kuondoka ninapenda kumshukuru kila mmoja wenu kwa kile mfanyacho: hatua ndogo… ni hatua ndogo lakini ambayo inafanya safari kubwa ya historia. Njoo mbele! Msiogope, jipeni moyo! Na Bwana awabariki. Asante. Na pia kuhusiana na  mahubiri yake Baba Mtakatifu Francisko, Rais wa Chama cha Migrantes,Monsinyo Guerino Di Tora, amefafanua  kuwa ni ishara ya ukaribu na umoja, sababu ya kupyaisha matumaini na ushauri.

Wahudumu wamemshukuru Papa

Kadhalika katika furaha hiyokubwa na utambuzi wa kutembelewa na Baba Mtakatifu katika mkutano huo, imeonesha kwa shauku kubwa na wahudumu wote walei na watawa wanaojikita katika vituo mbalimbali vya hali halisi ya kukaribisha, walio kuwapo katika maadhimisho ya Ekaristi Takatifu, wakati wa ufunguzi wa Mkutano  unaongozwa na mada: Huru dhidi ya hofu. Ni mkutano ulioandaliwa na Chama cha Migrantes, Caritas ya Italia na Kituo cha Astalli katika Mkutano wa  siku mbili kuanzia tarehe 15 -17 Februari 2019. Ziara hii ilikuwa na  tabia ya kifaragha kwa washiriki hao tu.

16 February 2019, 09:38