Cerca

Vatican News
katika katekesi yake Papa amesisitizia juu ya kuheshimu wazazi kutokana na amri ya nne ya Mungu katika katekesi yake Papa amesisitizia juu ya kuheshimu wazazi kutokana na amri ya nne ya Mungu  (Vatican Media)

Mwenyeheri wa Romania aliyeuwawa mwaka 1958

Baba Mtakatifu amekumbuka kuwa tarehe 22 Septemba huko Neampţ nchini Romania atatangazwa Mwenye heri Veronica Antal, mwamini mlei msekulari wa Shirika la Mtakatifu Francisko aliyeuwawa kutokana na kukiri imani yake kunako mwaka 1958

Sr Angela Rwezaula - Vatican

Mara baada ya tafakari yake ya Siku, Baba Mtakatifu ametoa  salam kwa waamini wote na mahujaji kutoka pande zote za dunia, waliofika katika viwanja vya Mtakatifu Petro mjini Vatican, tarehe 19 Septemba 2018.

Na katika salam hizo, Baba Mtakatifu amekumbuka kuwa tarehe 22 Septemba 2018 huko Neampţ nchini Romania atatangazwa Mwenye heri Veronica Antal, mwamini mlei msekulari wa Shirika la  Mtakatifu Francisko  aliyeuwawa kutokana na kukiri  imani yake kunako mwaka 1958. Baba Mtakatifu amesema, tumshukuru Mungu kwa ajili ya mwanamke jasiri ambaye alitoa maisha yake akishuhudia upendo wa kweli kwa ajili ya Mungu na ndugu!

19 September 2018, 14:57