Cerca

Vatican News
Ziara ya kitume nchini  Lithuania, Papa akiwa mbele ya picha ya Mater misercordiae Ziara ya kitume nchini Lithuania, Papa akiwa mbele ya picha ya Mater misercordiae  (Vatican Media)

Papa katika Madhabahu, ameomba kujenga madaraja na siyo kuta!

Katika shule ya Maria inawezekana kujenga jamii yenye uwezo wa kupokea, mahali ambapo zawadi za kila mmoja zinazungukia wote. Ndiyo mawazo ya Baba Makatifu aliyo waachia waamini waliokusanyika katika madhabahu ya Mama Maria wa Huruma mjini Vilnius 22 Septemba 2018

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Madhabahu yenye jina la Mater  Misercordiae, inawakilisha kile kinachobaki cha  ukuta wa kisazamani ili kulinda mji wa Vilnius.  MJi huo uliharibiwa kunako mwaka 1799 na kubaki limesimama Lango kuu mahali ambapo tangu wakati ule hadi sasa waliweka picha ya Bikira wa Huruma. Matembezo ya Kanisa la Mama Maria ilikuwa ndiyo hatua ya kwanza ya Papa Francisko kwa waamini wa Lithuania alasiri ya Ijumaa tarehe 22 Septemba 2018.

Picha ya Mama inajionesha kwa kila kwa kila mmoja Yesu

Picha ya Mama Maria wa Vilnius haina mtoto, bali imepambwa yote, ni mama wa wote, amesema Papa Francisko, wakati wa hotuba yake ya pili Katika Madhabahu ya mama Maria na kuongeza, yeye kwa kila mmoja anaonesha  uso wa Mtoto wake Yesu. Iwapo picha ya Yesu inawekwa kama mhuri kwa kila moyo wa binadamu, kila mwanaume na kila mwanamke, ina uwezo wa kukufanya kukutana na Mungu”.

“Tunapojifungia sisi binafsi kwasababu ya kuogopa wengine, tunapojenga kuta na vizingiti, tunaishia kukosa bahati ya kupata  Habari njema ya Yesu ambaye anapeleka historia na maisha ya wengine, anathibitisha Baba Mtakatifu. Kadhalika anasisitiza:”Tumejenga vizingiti vya nguvu nyingi kipindi kilichopita, lakini leo hii tunahisi mahitaji ya kutazamana uso kwa uso na kutambuana kama ndugu na kutembea pamoja tukigundua na kufanya uzoefu na furaha na amani ya tunu msingi wa kindugu.

Kuwa na msimamo dhatibiti wa makutano kati ya wote

Shukrani kwa uwezekano wa mawasiliano na mzunguko wa ulio huru, anaendela Papa , watu wengi wanatembelea kila siku Madhabahu hiyo , kutoka nchin Lithuania, wapoland, waurusi ya magharibi na mashariki, wakatoliki na waorthodox. Jinsi gani ilivyo nzuri kuona uwezekano huo wa kusafiri kutoka sehemu moja kufika sehemu nyingine, ungeweza hata kuwa ndiyo wa kuwekwa msimama thabiti wa makutano na mshikamano kati ya wote na kuweza  kufanya  izunguke zawadi nyingi zilizopokewa kutoka kwa Mungu bure, kuondokana na ubinafsi na kuweza kuwazawadia wengine, kwa kupokea mara nyingine tena  uwepo na utofauti wa wengine kama zawadi na utajiri katika maisha yetu.

Mama anatamani kuunganisha familia ya kibinadamu

Hali halisi ya sasa, inampeleka Baba Mtakatifu kufikia kutaja masuala ya  migogoro, mivutano, chuki na uadui. Na hivyo Baba Mtakatifu Francisko amesema kuwa,  Mama wa Huruma anatamani kuunganisha familia ya binadamu na kwa kila mtu anamwamba “ Tafuta ndugu yako”. “Leo hii wanatusubiri watoto na familia wakiwa na majeraha yanayotoa damu; si madonda yale ya Lazaro, katika somo la Injili, yale ni madonda ya Yesu; ya kweli na dhati, pia ya uchungu wao na giza nene linalowasonga, wanaomboleza ili sisi tuwe mwanga wa kuponya kwa njia njia ya upendo”.

PapaFrancisko akiendalea tena na  wazo lake kwa mama Maria ametoa ushauri wa “kuomba msaada kwa ajili ya kujenga jumuiya yenye uwezo wa kutangaza Yesu Kristo, kwa ajili ya nchi, yenye uwezo wa kwapokea wote, (…) Nchi ambayo inachagua kujenga madaraja na si kuta na inayopendelea huduma na si kuhukumu”.

Kusali pamoja fungu moja la Rosari

Mwisho wa hotuba yake, Papa Francisko amewaalika waamini kusali fungu moja ya Rosari, wakitafakari tendo la tatu la matendo ya furaha, yaani Yesu anazaliwawa Betlehemu. Ni watoto na familia ambao wamekuwa mstari wa mbele kuongoza Salam Maria katika lugha ya kilithuania….

Baadaye imefuata wimbo wa salam Malkia na sala katika lugha ya kilatini iliyosomwa na Papa Francisko, na baadaye Papa Francisko ametoa zawadi yake katika Altare ya Mama wa Huruma, ambayo ni rozari ya dhahabu. Na mwisho kuwabariki kama hitimisho la mkutano huo. Nje ya madhabua alikuwa akisubiriwa watu wengi wakimsalimia wakati anaondoka kwenda kukutana na vijana waliokuwa wanamsubiri karibu na uwanja wa Kanisa Kuu Katoliki la Vilnius.

 

 

 

 

23 September 2018, 09:13