Papa: Maombi na ukaribu kwa waathirika wa Raganello Calabria
Sr. Angela Rwezaula - Vatican
Katika salam zake nyingi alizotoa Baba Mtakatifu kwa kwa lugha mbalimbali mwishoni mwa katekesi yake Baba Mtakatifu wazo lake limetazama janga jingine lilitokea siku za hivi karibuni huko Raganello Carabria nchini Italia. Janga hili hili limewapoteza watu 10 katika moja ya maporomoko ya maji, wakiwa katika mzunguko wa kutembelea maporomoko hayo kama sehemu ya mchezo wakati wa kiangazi na kusababisha majeruhi akiwemo hata mtoto. Hawa ni wanawake 6 na wanaume 4.
Ni janga ambalo lingekuwa pia hatari zaidi na kwa maana yalikuwa ni makundi mawili jumla yao wakiwa 36, ambao walikuwa wameganyika wakitembelea eneo hilo bila kuwa na habari ya hatari ambayo wangekutana nayo! Hadi sasa watu 23 wameokolewa ambapo kati yao kuna mtoto msichana mwenye umri wa miaka 8 ambaye hali yake ni mbaya kulingana na taarifa za vyombo vya habari.
Kutokana na hayo, watu wanaoteseka na msiba huo, Baba Mtakatifu Francisko anawaonesha ukaribu wake wa maombi kwa familia zao , majeruhi na kuwakabidhi watu waliopoteza maisha katika huruma ya Mungu .
Papa kuomba sala kwa ajili ya ziara yake ya kitume nchini Ireland
Kadhalika ametoa salam zake kwa vijana, wazee, wagonjwa na wanandoa wapya. Baba Mtakatifu pia anasema kuwa katika Liturujia ya leo hii ni Sikukuu ya Bikira Maria Rejina. Kwa maana hiyo Mama wa Mungu awe kimbilio katika kipindi kigumu na kuwafundisha kupenda mwanaye kwa upendo wake wa dhati kama alivyompenda. Baba Mtakatifu amewaomba pia ala kwa ajili ya ziara yake ya kitume ijayo tarehe 25-26 Agosti na kwamba, katika fursa ya Mkutano wa Familia duniani, uweze kuwa kipindi cha neema na kusikiliza sauti ya wanafamilia wakristo duniani. Bwana awabariki nyote.