Tafuta

2023.12.04 Ripoti ya kwanza kuhusu Sister Communicate", katika Mkutano wa Kwanza wa Kimataifa kuhusu Mawasiliano ya Watawa ulioandaliwa na UISG 2023.12.04 Ripoti ya kwanza kuhusu Sister Communicate", katika Mkutano wa Kwanza wa Kimataifa kuhusu Mawasiliano ya Watawa ulioandaliwa na UISG  #SistersProject

UISG,watawa wanakua katika tasnia ya mawasiliano ya kidijitali

Katika ripoti ya Sisters Communicate iliyotolewa katika siku ya mwisho ya mkutano wa kwanza wa kimataifa kuhusu mawasiliano ya maisha ya kitawa Ulioandaliwa na (UISG),Dk.Ruffini alisema hakuna mawasiliano bila ushirika na hakuna ushirika bila mawasiliano na Mratibu wa Mpango:Ni ndoto iliyotimia kwa wawasilianaji wa mtandao wa maisha ya kitawa.

Alice Callegari na Angella Rwezaula – Vatican.

Miaka 60 baada ya Tamko la Mtaguso wa II wa Vatican kuhusu zana za mawasiliano ya kijamii kwa Hati ya( Inter Mirifica,)hata katika Maisha ya kitawa yanachukulia uzito wa mwaliko wa Kanisa wa kukaa katika ulimwengu wa kidijitali, kwa ufahamu na taaluma. Katika Muktadha huo Umoja wa Kimataifa wa Mama Wakuu wa Mashirika ya Kitawa UISG) tarehe 4 Desemba 2023 walichapisha ripoti yenye kichwa:“Sisters communicate” yaani "Masista wanawasiliana,”kuhusu mawasiliano katika maisha ya kitawa.” Na hii ni hali halisi ambayo inazidi kukua Ulimwenguni kote. Na kuwa wamisionari wa kidijitali katika kila taasisi ni katika pia kuunda ushirika na madaraja ya mazungumzo katika bara la sita, lile la kidijitali, kuongeza ufahamu wa uongozi, katika ngazi zote, wa  utamaduni wa kidijitali na uwezo wake katika uwanja wa uinjilishaji, taaluma ya uchungaji na uenezaji wa karama, kutunza kumbukumbua na kusasisha kwa waundaji, kupunguza pengo la kiutamaduni kati ya mazungumzo na dhana ya dijititali.” Haya na mengine ndiyo baadhi malengo yaliyomo katika tamko la mwisho la Mkutano wao wa kwanza wa kimataifa wa mawasiliano ya maisha ya kitawa,ambapo ni mpango uliohamasishwa na Chombo hicho cha UISG na kuhitimishwa mnamo  tarehe 4 Desemba 2023  jijini  Roma,katika makao yao makuu ya UISG.

Mkutano huo uliofanyika kwa Juma zima kwa njia ya mtandao na ana kwa ana huku ukijikita kwa kina katika mada kuu tatu za mafunzo, mitandao na mabadiliko muhimu yaliyotajirisha tukio ambalo lilihusisha watawa wa kike na kiume 200. Ka njia hiyo Hati iliyowakililishwa mwishoni  mwa Mkutano huo inatokana na utafiti uliofanywa kwenye mashirika ya kitawa ya kike 300 kuhusu ukweli wa mawasiliano katika Mashrika ya Kitawa. Kama inavyosemeka katika kurasa za kwanza  za Hati hiyo kuwa,"Tunaweza kusema kwamba leo watawa wanaonekana zaidi katika uwanja wa umma wa vyombo vya habari vya Kikatoliki japokuwa (bado kuna kazi nyingi ya kufanya kwa vyombo vya habari vya kilimwengu) na kuna watawa wengi zaidi ambao huandika wakiwa wa kwanza, huku wakihama kutoka katika kuwa vitu vya habari hadi wahusika wakuu wa neno lao na picha  halisi kwa umma.”

Daktari Ruffini:hakuna mawasiliano bila ushirika na ushirika bila mawasiliano

Miongoni mwa waliokuwapo pia mwanzoni mwa mkutano, huo na ujumbe kwa njia ya video, alikuwa ni Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Dk.Paolo Ruffini, ambaye katika kuzungumza aliwakumbusha washiriki wa Mkutano huo kwamba "hakuna mawasiliano bila ushirika na hakuna ushirika bila mawasiliano. Ni juu yetu,ni juu yako, ni juu yetu sote kujifunza lugha ya wakati wetu. Kufanya kila kitu kwa kila mtu kuwa zaidi katika huduma ya mawasiliano yanayojenga, yanayounganisha, yanayoanzia moyoni, kutoka kwa upendo, kutoka kwa kusikiliza wengine na kutoka kwa neno linalobariki". Kwa njia ya Mtandao vile vile hata Nataša Govekar,Msimamizi wa Kurugenzi ya Kitaalimungu ya Kichungaji ya Baraza la Kipapa la Mawaslialiano kwa kuzingatia mada:"Kujifunza kuwasiliana: matunda ya Mpango wa Pentekoste wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano"aliakisi ni kwa jinsi gani Baraza lenyewe la Mawasiliano lilivyanzisha Mpango huo ili kuhakikisha kwamba maisha ya kitawa ya kike yanaweza kuimarisha uwezo wa wanawake wa kitawa katika kuwatumikia watu wa Mungu na kila mtu.”https://www.vaticannews.va/sw/vatican-city/news/2023-11/ruffini-misingi-ya-inter-mirifika-ni-umoja-mawasiliano-na-upendo.html.

BARA LA SITA LA KIDIJITALI

Katika Maandishi karibu ya kurasa 120 yaliwasilisha takwimu za kiasi cha maisha ya kitawa ya  wanawake kuhusu mantiki hasa ya kuvutia kwa sababu kama tunavyosoma tena katika kurasa za kwanza za hati hiyo kwamba:“Hakuna chochote juu ya mawasiliano ya maisha ya kitawa ya  kike, wala masomo, wala machapisho; isipokuwa ni baadhi ya nadharia katika Vyuo vikuu vya kipapa, ambayo ni matunda ya matokeo ya mpango binafsi wa watawa. Na hivyo hakuna muundo na wa kitaasisi.” Wakati mwingine muhimu ulikuwa uwasilishaji wa Dichiarazione “Insieme per una comunicazione digitale efficace ed Evangelica yaani tamko la "Pamoja la mawasiliano ya kidijitali yenye ufanisi na ya Kiinjili ambapo kunatakiwa kujitolea kwa miaka ijayo kama jitahada kumi zilizochaguliwa na wawasilianaji wenyewe katika mawasiliano ya kitaalamu zaidi ya kidijitali kwa watawa. Baadhi ya mambo muhimu ya kifungu hicho kwa hakika yanaakisi umuhimu,katika Mashirika ya Kitawa kuwa wamisionari wa kidijitali ili kuunda madaraja ya ushirika na mazungumzo katika bara la sita,lile la dijitali,lakini pia kujifunza kuwasiliana kupita zaidi ya habari iliyo safi,ili kuimarisha mafunzo ya kitaaluma ya watu, kwa kuunganisha mwelekeo wa kidijitali katika mafunzo ya awali  na kujifunza kuwa na roho ya utambuzi ambapo hatimaye ni kujifunza kujenga mahusiano mazuri na vyombo vya habari vya Kikatoliki na visivyo vya Kikatoliki.

WASHAWISHI WA KIDIGITALI

Kwa upande wa  washawishi wa kidigitali Padre Jeffrey, kutoka Ufilipino na Alumera, kutoka Italia, wamisionari wa kidijitali, walizungumza kuhusu uzoefu wao na kutoa baadhi ya mapendekezo ya maisha ya kitawa. Kwa upande wa wadau wawili wa kidigitali walikumbusha kuwa Kanisa,linabadilika kulingana na mabadiliko ya wakati,Kanisa daima limekuwa bunifu  katika kujibu mahitaji ya mwanadamu. Wito  unabaki pale pale ule wa kueneza upendo wa Kristo,njia ya kuwasiliana nayo inabadilika ili kuweza kusambaza kwa kila mtu upendo huo ambao hatuwezi kuuzuia”. Na uhakika wa Patrizia Morgante, mratibu wa "Mpango alisema ni kwamba mawasiliano yanaweza kusaidia kuacha matokeo ya karama zetu, ili kueleza uzuri wa Injili". Shauku yake ya maisha ya kitawa ilikuwa ni"kufanya taaluma katika uwanja wa mawasiliano, kuunda mtandao, mafunzo, kuwekeza rasilimali za kiuchumi na watu kwa ujasiri na ubunifu."

Mkatano wa Watawa UISG na ripoti ya kwanza

Mchango wa Conrad N. Hilton

Ripoti ya "Msisita  wanawasiliana”, juu ya Mawasiliano katika maisha ya kitawa” iliyowasilishwa tarehe 4 Desemba jijini Roma, iliundwa kwa mchango wa Mfuko wa Conrad N. Hilton ambao ni moja ya mifuko mikubwa ya hisani nchini Marekani na jina ambalo mara nyingi hujirudia katika mipango ya Mashirika ya Watawa wa Kike, kwa sababu maalum. Kwa asili yake kiukweli ni Conrad N. Hilton (1887-1979), menyewe aliyeunda mlolongo wa kwanza wa hoteli za kimataifa kuanzia na sufuri na mmoja wa watu maarufu zaidi wa karne ya 20. Kwa njia hiyo Hilton alizaliwa huko Mtakatifu Antonio, katika familia ya watu wa hali ya chini.Baba alikuwa muhamiaji kutoka nchini Norway na kumiliki duka dogo la jumla, wakati mama yake wa Kimarekani mwenye asili ya Kijerumani na Mkatoliki alikuwa na tabia iliyohifadhiwa na alama ya imani kubwa. Kwa njia hiyo kijana Conrad alihudhuria shule za mitaani na mara tu alipoweza aliinga katika ulimwengu wa biashara huku akifuata nyayo za baba yake na haraka akakusanya mali, shukrani kwa talanta, maazimio na hali nzuri iliyomzunguka.

Kutokana na hiyo "Hilton akawa mhusika mkuu, mkubwa kuliko maisha kama wanavyosemakatika ulimwengu unaozungumza Kiingereza". Ndiyo hakuwa mfano wa fadhila nzuri za nyumbani kwa sababu alipata ndoa tatu, ambapo ya pili ilikuwa ya mwigizaji wa Hollywood Zsa Zsa Gabor, lakini hakuwahi kukosa kujitolea  hasa hasa  alibaki na hisia ya shukrani kwa watawa ambao walimpatia elimu yake ya kwanza ambapo alikuwa amejifunza mafundisho jamii ya Kikatoliki kutoka kwaMasista wa Loretto, au  walioitwa Masista wa Loretto chini ya miguu ya Msalaba, taasisi iliyoanzishwa mwanzoni mwa karne ya 19 huko Marekani. Hilton alipopokea barua kutoka kwa Masista wa Loretto mnamo mwaka 1944 wakiomba mchango mdogo wa kufungua shule katika eneo maskini la vijijini la New Mexico, aliwaambia masisita hao kwamba uchangishaji wao ungeishia hapo kwa sababu angelipa pesa zote za gharama za shule. Na ilikuwa ni mwanzo tu wa ushirikiano wa muda mrefu. Leo hii mfuko huo Maalum wa Conrad N.Hilton kwa ajili ya Masista unaendelea na nia ya mwanzilishi wake ili kusaidia kazi ya watawa wa Kikatoliki Ulimwenguni kote. Katika wosia wake, Conrad N. Hilton alifafanua kuwa watawa ni“walinzi na watetezi wa watoto na akawaalika kuwa wakarimu kwao na kazi zao."

05 December 2023, 16:19