Tafuta

2023.11.27 Padre Hans Joachim Lohre, aliyekuwa ametekwa nyara mwaka mzima ameachiwa huru huko Mali. 2023.11.27 Padre Hans Joachim Lohre, aliyekuwa ametekwa nyara mwaka mzima ameachiwa huru huko Mali. 

Baada ya mwaka wa kutekwa nyara Padre Ha-Jo Lohre,ameachiwa huru

Padre Hans-Joachim Lohre,ajukakanaye sana kwa jina“Ha-Jo”wa Shirika la Wamisionari wa Afrika,ameachiwa huru nchini Mali baada ya kutekwa nyara kwa mwaka mzima.Habari kutoka Shirika la Kipapa la Habari za Kimisionari Fideslimesema kuwa Mmisionari huyo wa Ujerumani kwa sasa amesafirishwa kwenda kwao.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Padre Hans Joachim Lohre, aliyejukana sana kwa jina  Ha – Jo, Mmisionari wa Afrika wajulikanao White Fathers na raia wa Ujerumani, aliyekuwa ametekwa nyara nchini Mali, mnamo  Dominika tarehe 20 Novemba 2022 ameachiwa huru. Mwaka mmoja baada ya kutekwa nyara, mmisionari huyo aliachiliwa Dominika tarehe 26 Novemba 2023. Mazingira ya kuachiliwa kwake hayako wazi. Ukombozi wa Padre  Lohre ulitangazwa Dominika  na mwakilishi wa serikali ya Mali na wawakilishi wawili wa  Jimbo Kuu la  Bamako ambao hawakutaka kutajwa majina yao. Kwa mujibuwa Taarifa kutoka Shirika la Kipapa la Habari za Kimisionari Fides,  kuachiliwa kwake kumejadiliwa moja kwa moja na serikali ya Ujerumani, na mara mmisionari huyo alipoachiliwa na watekaji wake na kukabidhiwa kwa mamlaka ya Mali, mara moja aliwekwa chini ya ulinzi na wawakilishi wa mamlaka ya Berlin na kuhamishiwa Ujerumani wakati wa usiku kwa ndege maalum.

Kikosi cha kijeshi cha Ujerumani bado nchini Mali

Ujerumani bado ina kikosi chake cha wanajeshi nchini Mali ambao ni sehemu ya kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa cha Minusma, ambacho kinatarajiwa kusitisha shughuli zake mwishoni mwa mwaka huu 2023, kama ilivyoombwa na mamlaka ya kijeshi ya mapinduzi ambayo yalichukua mamlaka kwa mapinduzi mwaka 2020. Anajulikana nchini  humo kwa jina la utani "Ha-Jo," Padre  Hans-Joachim Lohre, mwenye umri wa miaka 66, alikuwa ameishi nchini Mali kwa zaidi ya miaka 30 ambapo, pamoja na mambo mengine, alifundisha katika Taasisi ya Mafunzo ya Kiislamu-Kikristo (Ific) na alikuwa na jukumu la Kituo cha Imani na Mikutano huko Hamdallaye.

Shughuli nyingine za Padre Lohre alizokuwa nazo

Siku ya utekaji nyara mmisionari alitarajiwa kusherehekea misa katika jumuiya ya Kalaban Coura. Gari lake liliegeshwa mbele ya nyumba yake na wachunguzi baadaye walipata mkufu uliokuwa na msalaba wa Padre  uliokutwa karibu na gari lake. Utekaji nyara huo haukudaiwa lakini hata hivyo ulihusishwa na vyanzo vya kidiplomasia na usalama kwa JNIM, Kundi la Kuunga mkono Uislamu na lenye uhusiano na al-Qaeda. Padre  Lohre ni Mjerumani wa pili kuachiliwa katika  Ukanda wa Sahel chini ya mwaka mmoja, kufuatia kuachiliwa kwa mfanyakazi wa  Huduma ya misaada Jörg Lange mnamo Desemba 2022 ambaye alitekwa nyara tarehe 11 Aprili 2018 magharibi mwa Niger, kwenye mpaka na Mali. Lakini idadi ya mateka wa kigeni, ikiwa ni pamoja na Mwafrika Kusini na wanandoa wa Kiitaliano na mtoto wao wa kiume, bado wanazuiliwa ukanda wa Sahel.

Wamisionari wa Afrika,Padre Paul Sanogo na Frt Mahinini
Wamisionari wa Afrika,Padre Paul Sanogo na Frt Mahinini

Na ikumbukwe ilikuwa pia Padre Paul Sanogo na Mseminari Melkiori Dominick Mahinini, waliokuwa ametekwa nyara mnamo  tarehe 3 Agosti 2023 waliachiliwa huru. Habari hizo zilichapishwa tarehe 24 Agosti 2023 na Shirika la kipapa la Habari za Kimisionari (FIDES). Padre Sanogo na Mseminari Melkiori walikuwa ni  wamisionari wa Afrika, Shirika ambalo linajulikana sana zaidi kama Mababa Weupe(White Fathers. Utekaji nyara huo ulitokea katika shambulio la parokia ya Mtakatifu Luka  huko Gyedna Jimbo Katoliki la  Minna), Mkoa wa  Niger kaskazini-kati mwa Nigeria.

https://www.vaticannews.va/sw/church/news/2023-08/nigeria-watawa-wamisonari-wa-afrika-walitoekwa-nyara-agosti-3.html

Mmisionari wa Afrika Padre Ha Jo kuachiwa huru
27 November 2023, 14:30