Tafuta

Watawa waliotekwa nyara wameachiwa huru huko Haiti Watawa waliotekwa nyara wameachiwa huru huko Haiti 

Kuwaachilia huru watawa waliokuwa wametekwa nyara nchini Haiti

Kuwachiliwa huru kwa watawa 4 wa mwisho waliokuwa wametekwa nyara katika shambulio la tarehe 11 Aprili 11 iliyopita umemalizika.Wengine waliachiliwa wiki moja iliyopita.Familia ya wamisionari wa makuhani wa Mtakatifu Jacques wametangaza kuachiliwa kwao.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Watawa wa 4 wa mwisho wamewachiliwa huru waliokuwa wametekwa nyara mnamo Aprili 11 huko Haiti. Ni tukio ambalo limefanyika usiku kati ya Alhamisi 29 na 30 Ijumaa Aprili. Habari hiyo, ambayo ilikuwa inasubiriwa kwa muda, imetolewa na  makuhani wa Shirika la Mtakatifu Jacques ambao kati ya wengine wanatoka shirika hilo. Ni wiki moja tu iliyopita, watekwaji nyara wengine watatu walikuwa wameachiliwa huru.

Kumshukuru Mungu

Mmoja wa watawa hao amethibitisha kuwa na afya njema na kuwashukuru mabalozi wa Ufaransa na Marekani kwa juhudi zao katika kusuluhisha jambo hilo, lakini pia na viongozi wa eneo hilo kwa msaada wao . “Maneno yetu ya kwanza yana waendea kaka na dada zetu walioachiliwa huru, kuwaonesha furaha yetu na kuridhika kwetu kwa kuwakuta salama salimini”. Kwa kuongezea, “tunazo hisia za shukrani kubwa kwa Mungu na kwa watu wote na taasisi ambazo zimehusika kufikia ukombozi wa ndugu zetu na marafiki zetu, ambao tumepamban mwili na roho”. Kikundi cha watu 10 kilisimamishwa huko Croix-des-Bouquets, karibu na mji mkuu Port-au-Prince wakati wakielekea parokia ya Galette Chambon, huko Ganthier, kushiriki sherehe za kusimikwa kwa kasisi wa parokia,  Padre Jean Arnel Joseph, inayoundwa na makuhani watano Wakatoliki, watawa wa kike wawili na walei watatu.  Kwa upande wao walikuwa wameomba fidia ya dola milioni.

Ukosefu wa usalama  Haiti

Utekaji nyara umeathiri na kuleta mkanganiko sana wa maoni ya umma na umebainisha wazi ukosefu mkubwa wa usalama ambao Haiti inaishi kwa sasa, nchi ambayo baada ya tetemeko la ardhi lenye uharibifu wa miaka 11 iliyopita, haijapata furaha kwa sababu ilikumbwa na majanga ya asili na shida za kijamii, kiuchumi na kisiasa ambazo sasa zimepelekea vurugu za magenge yenye silaha. Katika taarifa iliyosainiwa wiki chache zilizopita na askofu mkuu wa mji mkuu, Askofu  Max Leroy Mésidor, alikuwa analaani kushuka kwa maadilini ya kijamii ya wahaiti.

30 April 2021, 17:03