Tafuta

Vatican News
IRAQ:Wakristo wanasali kwa ajili ya ujio wa Papa Francisko mwezi Machi 2021. IRAQ:Wakristo wanasali kwa ajili ya ujio wa Papa Francisko mwezi Machi 2021.  (AFP or licensors)

Iraq inasali kwa ajili ya ujio wa Papa Francisko!

Bwana Mungu wetu umpe Papa Francisko afya na mafanikio ili aweze kufanikisha ziara hii inayotarajiwa. Bariki juhudi zake za kuimarisha mazungumzo na upatanisho wa kindugu na kujenga uaminifu,kuimarisha maadili ya amani na utu wa kibinadamu,hasa kwetu Wairaq,mashahidi wa matukio ya uchungu ambayo yametugusa.Ni sala ya aliyoandika Kard.Sako kwa ajili ya kuombea ziara ya Papa inayotarajiwa.

Na Sr. Angela Rwezaula,-Vatican.

Kwa muda fulani tumekuwa tukiishi kwa hofu, lakini pia kwa tumaini, amesema Patriaki wa Babilonia ya  Wakaldayo, mara tu aliposikia juu ya ziara  ya Papa, Francisko tarehe 7 Desemba iliyopita, na alikuwa ameonesha kuwa ni ishara ya kuzaliwa upya kwa nchi, yaani Noeli mpya. Leo, hii kwa roho hiyo hiyo, Kardinali Louis Raphaël Sako ametunga sala akiomba, kupitia njia za mikondo ya Upatriaki kwamba waamini waisali pamoja wakati wa Misa kila Jumapili kuanzia  tarehe 17 Januari 2021. “Bwana Mungu wetu umpe Papa Francisko afya na mafanikio ili aweze kufanikisha ziara hii inayotarajiwa. Bariki juhudi zake za kuimarisha mazungumzo na upatanisho wa kindugu na kujenga uaminifu, kuimarisha maadili ya amani na utu wa kibinadamu, hasa kwetu Wairaq, mashahidi wa matukio ya  uchungu ambayo yametugusa”.

Hivi ndivyo inavyoanza sala  ambayo, kabla ya kumkabidhi  kwa  Mama Bikira Maria, ameomba nuru ambayo ni kichocheo kwa wote katika wakati huu kwamba: “Bwana, muumba wetu, angaza nyoyo zetu na nuru yako ili tuweze kuona mema na amani na kuanza kuyatimiza. Kwa njia hiyo  maombi ya maombezi Bikira, Mama yetu, ambaye kwa utunzaji wa umama wake amekabidhi Baba Mtakatifu anaandika “Ili Bwana atupe neema ya kuishi katika muungano kamili wa kitaifa, tukishirikiane kidugu kujenga maisha bora ya baadaye Nchi na raia wake”.

Tayari mwanzoni mwa mwezi Desemba mwaka jana, kwa maana ya mwezi mmoja uliopita, Patriaki Sako, akiandika barua kwa watu wa Iraq, alikuwa ameomba kujitayarisha vya kutosha kwa ajili ya kufika kwa Papa ambaye alisema haitakuwa safari ya kitalii au ya anasa badala yake ni hija iliyojaa ujumbe wa faraja kwa wote na kutiwa moyo wakati  huu wa kutokuwa na uhakika; na kwamba “lazima tufanye kuwa fursa ya mabadiliko makubwa ili imani na matumaini ndanu yetu iweze kuwa jitihada”.

Francisko anaanza tena kusafiri ambapo atakwenda Iraq tangu tarehe 5 hadi 8 Machi

Hija ya Papa Francis ya kwenda Iraq, kwa mwaliko wa viongozi wa serikali na Kanisa Katoliki  huko, ilitangazwa rasmi mapema Desemba iliyopita, ikiashiria kuanza tena kwa safari zilizokatizwa ghafla kwa miezi kumi na tano kwa sababu ya dharura ya kiafya ulimwenguni. Tarehe zilizopangwa ni kuanzia tarehe  5 hadi 8 Machi, na vituo vyake  vitakuwa Baghdad, uwanda wa Uru, uliounganishwa na kumbukumbu ya Ibrahim, mji wa Erbil, na Mosul na Qaraqosh katika uwanda wa Ninawi. Siku nne  muhimu  sana kwa ajili ya  ukaribu na watu ambao wameteseka na wanaendelea kuteseka kutokana na vita na ambao pole pole wameona Wakristo wakiondoka nchini humo. Ni safari ambayo Papa Francisko amekuwa akitamani  kwa muda mrefu, huku akielezea nia yake tangu 2019 na kila wakati akiongezea maneno yake ya  mwaliko wa kujenga nchi hiyo thabiti ya  kijamii ambayo inalenga manufaa kwa wote.

16 January 2021, 20:22