Tafuta

Vatican News
Askofu Mkuu TEISSIER Askofu Mkuu TEISSIER  (AFP or licensors)

Papa:Askofu Teissier alikuwa mtu wa mazungumzo na amani

Mchungaji mkarimu na kwa ujasiri amelipitia maisha yake katika Kanisa la Algeria,katika jitihada ya mazungumzo na katika udugu.Ndivyo Papa Francisko amemkumbuka katika telegram iliyotiwa saini na Katibu wa Vatican kufuatia na kifo cha Askofu mkuu mstaafu aliyeaga dunia terehe Mosi Desemba katika kumbu kumbu ya liturujia ya Mwenyeheri Charles de Foucauld.

Na Sr. Angela  Rwezaula - Vatican

Papa Franciko ametuma salam za rambi rambi, zilizotiwa saini na Kardinali Pietro Palorin Katibu wa Vatican iliyoelekezwa kwa Askofu Paul Desfarges wa Algeria kufuatia na kifo cha Askofu Mkuu  Henri Teissier. Katika  Ujumbe huo Papa Francisko ameelezea maskitiko yake akifungua siku ambayo ilikuwa inakumbusha Kumbu kumbu ya Mwenyeheri Charles de Foucauld,  tarehe Mosi Desemba na hivyo kupata habari  za kifo cha Askofu Mkuu mstaafu Henri Teissier, aliyekuwa Askofu Mkuu wa Algeria. Papa Francisko  anamwombea kwa Bwana roho yake ya mchungaji mkarimu na ambaye alitambua kwa ujasiri mkubwa na roho ya kiinjili kuishi majaribu ya Kanisa nchini Algeria.

Alikuwa ni mtu wa mazungumzo na amani na alikwenda kukutana kwa heshima na roho ya kidugu watu wa Algeria katika michako ya  safari ya maisha yake kwa miaka mingi huku akihudumia katika majimbo ya Orano na  Algeri, aliyokuwa amekabidhiwa kichungaji. Katika kuomba kwa Baba kisima cha kila huruma na kumpokea Askofu aliyeagaza dunia katika amani na mwanga wa Ufalme wake na kwa kumkabidhi kwa maombezi ya Mama yetu wa Afrika, Mwenyeheri Charles de Foucauld na watakatifu wafiadini wa Algeria, Baba Mtakatifu anasali kwa ajili ya watu wote walioondokewa na yeye na kwa moyo wote anawatumia Baraka ya Kitume:  familia na ndugu wa marehemu, maaskofu wa Algeria, waamini wa Orano wa Algeri na watu wote wanaoshiriki liturujia ya mazishi.

Askofu Mkuu Henri Teissier, alizaliwa Lione kunako mwaka  1929, na alipata daraja la upadre huko Algeri kunako 1955  baada ya masomo yake katika Seminari ya Wakarmeli huko Paris. Alijifunza kiaraba katika Taasisi ya Kidomenicani huko Algeri manmo 1958. Aliteuliwa kuwa askofu wa  Orano 1973, baadaye msaidizi wa Algeri wa Kardinali Duval tangu  1981, na  1988 akawa mfuasi wa Kardinali Duval kuwa Askofu Mkuu wa  Algeri, mahali alikaa hapo hadi  2008. Baada ya kung’atuka kwa sababu ya umeri wake alishirikisha maisha yake kati ya Ufaransa na Algeri. Ameaga dunia akiwa amezungukwa na ndugu zake katika Hospitali ya Édouard-Herriot, baada ya kupata kiharusi.

03 December 2020, 14:56