Tafuta

 Monstrance ya Ekaristi Monstrance ya Ekaristi 

Gabon:Parokia ya Abeke Ville imetendewa ishara mbaya ya ukufuru!

Kijana mmoja wa Kanisa la Abeke Ville nchini Gabon,alivunja Monstrance na kuchukua chombo kidogo kitunzacho Mwili wa Kristo.Kwa bahati nzuri kijana amerudisha nyuma akiwa na wazazi wake na kuomba msamaha!

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Paroko wa Kanisa la Mamajusi Wafalme huko Akebe Ville, mkoa wa  Libreville, nchini Gabon, Padre Benoît Dieme hivi karibuni “ni kama kuchomwa  Panga halisi moyoni kuafuatia na tukio lakunajisi Kanisani  ambalo limetokea tarehe 12 Septemba 2020.  “Kijana asiyejulikana alivunja  vipande viwili monstrance ya Sakramenti Takatifu na kuiba chombo kidogo kinachotunza Mwili wa Kristo. Kwa mujibu wa Paroko “Tumepigwa na mshangao mkubwa sana”, alisema na  kuongeza kuwashauri waamini waombe pamoja kwa malipizi ya tendo hili zito. “Tumekasirika na kusikitika, lakini tunavumilia”, alisema Padri Dieme. Kwa upande wake, Wizara ya Mambo ya Ndani, kwa maandishi, waliandikia “nalaani tukio hilo kwa uthabiti mkubwa na ninawahakikishia makasisi wa Gabon kuwa tutapata mwanga zaidi juu ya tukio hili la  uharibifu”.

Hitimisho la tendo hilo

Kufuatia na tukio hilo hata hivyo kwa bahati nzuri, limepata muafaka kwani haukuwa muda mrefu  ambapo Paroko huyo Padre Dieme alipotangaza kuwa mhusika wa tendo hilo la kukufuru amerudi parokiani na kukabidhi Monstrance.

“Kijana ameomba msamaha. Nimembariki pamoja na wazazi wake”. Tumshukuru Mungu kwa sababu Yesu katika Sakramenti ya Ekaristi amerudi katika nyumba yetu” amehitimisha Paroko huyo.

18 September 2020, 11:58