Tafuta

Vatican News
2020.08.28  Uwakilishi wa Misali Mpya ya Baraza la Maaskofu Italia (CEI ) kwa Papa Francisko. 2020.08.28 Uwakilishi wa Misali Mpya ya Baraza la Maaskofu Italia (CEI ) kwa Papa Francisko.  

Papa Francisko:Misale Mpya ya CEI itaanza kutumika rasmi wakati wa Pasaka 4 Aprili 2021!

Kardinali Bassetti na kikundi cha wawakilishi wa Baraza la Maaskofu Italia wamewakilisha kwa Papa Misale mpya ya kiliturujia ambayo itachukua nafasi ya ile ya sasa kuanzia Dominika ya Pasaka tarehe 4 Aprili 2021.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Aina mpya ya dhati ya zamani ambayo ina mizizi yake kutoka katika  Mtaguso wa II wa Vatican, ndiyo Misale mpya ya Baraza la Maaskofu Italia (CEI) ambayo Papa ameifungua  mikononi mwake asubuhi, tarehe 28 Agosti 2020, akiwa amezungukwa na Kardinali Gualtiero Bassetti, rais wa Baraza la maaskofu Italia na kikundi kilichofanya kazi ya kuandaa misale hiyo na ambapo  Papa alipendelea  kuitambua kazi hiyo na kuwashukuru ujio wao.

Kurasa za utamaduni hai

Papa Francisko ameshukuru zawadi aliyoipokea kwa kusisitiza umuhimu wa kazi iliyofanyika na mwendelezo wa Mtaguso wa Pili wa Vatican, kwa mujibu wa taarifa kutoka Baraza la Maaskofu Italia. Katika maneno ya Kardinali Bassetti anabainisha kwamba, Kitabu cha Misale ya waamini siyo zana ya kiliturujia tu, bali ni marejeo na sheria ambazo zinahifadhi utajiri wa utumaduni hai wa Kanisa na kukabidhiwa kwake kunageuka kwa mara nyingine tena kuwa fursa ya thamani ya mafunzo kwa wabatizwa wote.

Papa anafunua Misale
Papa anafunua Misale

Lugha imesasishwa na tarehe rasimi ni  4 Aprili 2021

Kitabu ambacho maparokia wataanza kutumia mara moja, lakini lakini rasimi ni kuanzia Dominika ya Pasaka  ya tarehe 4 Aprili 2021  kimeridhiwa kwa mujibu wa makubaliano  na Baraza la Maaskofu na kukubaliwa na Papa Francisko tangu tarehe 16 Mei 2019. Mbali na tofauti na uboreshaji wa toleo la tatu la Kilatino, misale hii inapendekeza maandishi mengine ya hiari ya muundo mpya, yenye kujibu zaidi hali  hali halisi ya lugha na kiuchungaji katika jumuiya, na  kwa kiasi kikubwa tayari inatumiwa  tangu toleo la pili nchini Italia la mwaka 1983 .

Habari mpya: mabadiliko ya sala ya baba yetu na utukufu

Miongoni mwa taarifa mpya, ambayo tayari unajulikana, ni kwamba kutakuwa na mabadiliko kuhusu sala ya  Baba Yetu katika sehemu isemayo  ‘usitutie katika kishawishi’ na badala yale inakuwa usituache katika kishawishi, na wakati katika  utukufu  mahali isemwapp ‘amani duniani kwa watu wenye mapenzi mema’  inabadilishwa na usemi kuwa amani duniani kwa watu, waliopendwa na Bwana. Misale hiyo ni ya kwanza kuchapishwa na Mfuko wa Jumuiya wa Dini ya Watakatifu Francis wa Assisi na Catherina wa Siena katika muundo mmoja na itasambazwa na Duka la Vitabu Vatican kuanzia mwishoni mwa mwezi Septemba.

29 August 2020, 10:41