Tafuta

Vatican News
Siku ya mabaharia kimataifa.Mabaharia ni wanadamu,ni wafanyakazi walioko mstari wa mbele na ni kwa sababu ya kujitoa kwao kwa  huduma yao  sisi sote  tunaweka chakula meza na kupokea dawa na vifaa, Siku ya mabaharia kimataifa.Mabaharia ni wanadamu,ni wafanyakazi walioko mstari wa mbele na ni kwa sababu ya kujitoa kwao kwa huduma yao sisi sote tunaweka chakula meza na kupokea dawa na vifaa,  

Ufilippino-Maskofu: msiogope mabaharia kwani Kanisa liko upande wenu!

Mabaharia ni wanadamu na wafanyakazi walioko mstari wa mbele na kwa sababu ya kujitoa katika huduma yao,sisi sote tunaweka chakula mezani na kupokea dawa na vifaa.Ni tafakari ya Askofu Ruperto Cruz Santos,mhusika wa Utume wa Bahari wa Baraza la Maaskofu nchini Ufilippino na ambaye anatazama muktadha wao mgumu uliochangiwa na janga la Covid-19 wakati wa kuadhimisha siku yao kimataifa hivi karibuni.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican

Katika Siku ya Mabaharia Kimataifa, Maaskofu nchini Ufillipino wanasema“ msiongope kwani Kanisa liko upande wenu”. Hata hivyo katika kilele cha siku hiyo kunako tarehe 25 Juni 2020, Jumuiya ya Umoja wa Mataifa imesema kuwa mabaharia pamoja na wavuvi ni kati ya wafanyakazi mashuhuri, wanaosaidia kusongesha mbele gurudumu la maendeleo fungamani duniani. Kwa mujibu wa Maaskofu wa Ufillipino wanasema “kufikia lengo, kuwasiliana na kuendeleza jitihada za kujifunza, ndiyo njia muhimu kwao. Maisha yana mambo mengi ambayo upiga chini na juu kama vile maji baharini,. wanaandika Maaskofu katika barua iliyotiwa saini na Askofu Ruperto Cruz Santos, mhusika wa kitengo cha Utume wa Baharini wa Baraza la Maaskofu Ufilippino na ambaye anatazama muktadha huo kuwa  mgumu hasa uliochangiwa na janga la Covid-19.

Shukrani kwa jitihada za mabaharia kwa jitihada

Katika ushauri wa Askofu lakini anasema, "kumbukeni hata ikiwa mawimbi yapo juu na upepo ni mkali, inabidi kuinua matanga  na kufunga milango kwa utambuzi ya kwamba Kanisa liko tayari kuwaunga mkono na kuwasaidia". “Hamko peke yenu, kwani  tuko pamoja nanyi, tunafanya kazi na tunawakaribisha kwenye vikanisa vyetu vidogo.” Kutokana na hii ndipo  wanatoa wito  kwa waamini  wote kutokuwa na ubaguzi dhidi ya mabaharia na kusema “Ni mashujaa wa siku zetu. Hawawezi kubandikwa majina ya uwongo kama wabebaji wa Covid-19; badala yake, lazima wakaribishwe, wasaidiwe na wenyeji ”. “Ni wanadamu, ni wafanyakazi walioko mstari wa mbele na  kwa sababu ya kujitoa katika  huduma yao kwamba, sisi sote tunaweka chakula katika meza na kupokea dawa na vifaa". Kwa maana hiyo barua hiyo ya kichungaji inaongeza  kwamba, ni muhimu kuonyesha kwamba hatujasahau au kuachana nao.

Mabaharia wawasiliane zaidi na wapendwa wao

Pili, maaskofu wa Ufilipino wanawahimiza mabaharia kuwasiliana zaidi na wapendwa wao, ili waweze kushirikisha katika maisha ya baharini. “Msiruhusu mazungumzo yenu yajikite tu katika mambo ya kifedha, mahitaji ya vifaa au bajeti isiyokamilika badala yake jaribuni kuruhusu mawasiliano yenu  yawe ya dhati, yaliyojaa  tumaini na daima yategemee kumbukumbu nzuri, ambao ni pumzi nafuu na kutiwa nguvu.” Wanaandika maaskofu.

Mafunzo zaidi na bidii ya uwajibikaji

Pendekezo la tatu ni kuendelea na njia ya mafunzo kila wakati kwa kufanya bidii zaidi, katika utendaji wa uwajibikaji na kujitoa kwenye majukumu waliyokabidhiwa. "Wakati mnapokuwa mkielekea katika fukwe na bandari zilizo mbali kwa hakika mtakabiliwa na shida ambazo zitaweka majaribu ya  dhamira zenu, kanuni zenu na msimamo wenu. Lakini mbele ya haya yote, kuweni waminifu na tunzeni mwenendo wenu huo huo.  Msiteleleke na kumbukeni maneno ya Yesu ambaye alisema: 'Msiogope' (Mt 14: 27). Hatimaye katika barua hiyo ya kichungaji, Mtume wa Bahari kwa ajili ya  Kanisa  nchini Ufilipino anawahakikishia mabaharia sala zake na kuwashukuru kwa huduma inayotolewa nchini humo.  "Ninyi ni mashujaa wetu na tumaini letu”.

02 July 2020, 14:23