MAREKANI.Pax Christi:Tujikite katika haki kwa ajili ya George Floyd,siyo kuhukumu kwa waandamanaji!
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican
Bwana Bob Shine, Mwenyekiti wa Baraza ka Kitaifa la “Pax Christ” yaani Amani ya Kristo” nchini Marekani ameandika katika tovuti ya Chama hicho kufuatana na maandamano makali yanayoendelea ya kupinga yaliyoibuka katika miji yote ya Nchi, mara baada ya kuuawa kwa George Floyd katika uhalifu wa afisa wa polisi huko Minneapolis. “Mtu hapaswi kuhukumu kinachotokea katika maandamano mengine, lakini basi ni kujiuliza ni nini kimekuwa kikijitokeza kwa watu weusi katika nchi hii mara kwa mar ana zaidi kupambana na watu weusi”.
Kwa mujibu wa Shine amesema, “kile ambacho tunatakiwa kukumbuka na kile ambacho hatuwezi kamwe kupoteza hapo ni kwamba mtu mweusi George Floyd, aliuawa na afisa wa polisi baada ya kukamatwa kwa tuhuma za uhalifu wa kulipa kwa kutumia noti ya bandia ya dola 20. Mtu huyo alifariki baada ya afisa wa polisi kuibana shingo yake kwa goti kwa karibu dakika tisa hata wakati ambapo Floyd alikuwa akiomba angalau aweze kupumua. Na wakati huo huo Polisi wengine walibaki wakatizama tu. Tukio kama hili limejirudia lenyewe na kwa njia tofauti, zaidi ya mamia ya miaka katika nchi yetu. Watu weusi wanakabiliwa na vitisho vikali kila siku, na ukweli ambao unaoonekana wazi katika matendo ya polisi wakati wa maandamano.”
Kiongozi huyo Shine amesisitiza kwa kutazama waandamanaji weusi katika wakati wa Trump na virusi vya corona, kwenye makala ya ‘Los Angeles Times’, Kareem Abdul-Jabbar, mmoja wa wachezaji wakubwa wa NBA na mmoja wa wanaosikiliza sauti za Kiafrika zaidi nchini ameandika kuwa “tunapaswa kuona kuwa watu wamesukumwa sana hadi ukomo, siyo kwa sababu wanataka bar na saluni za uzuri zilizo wazi, lakini ni kwa sababu wanataka kuishi. Kupumua”. Kwa maana hiyo, kiongozi huyo wa Pax Christ Marekani kwa kuhitimisha anasisitiza kwamba “Lengo letu na hapa ninazungumzia kwa namna ya pekee kwa wazungu kama mimi, ni kufanya kila liwezekanalo kuzuia uhalifu huu usirudiwe. Umakini unapaswa upewe kipaumbele cha haki kwa wale wote ambao wameuwawa.