Tafuta

Kanisa la Wellington nchini News Zealand limetangaza Wiki ya kusali kwa ajili ya Umoja wa Wakriristo kuanzia tarehe 25 -31 Mei 2020. Kanisa la Wellington nchini News Zealand limetangaza Wiki ya kusali kwa ajili ya Umoja wa Wakriristo kuanzia tarehe 25 -31 Mei 2020.  

NEW ZEALAND#coronavirus:Kard. Dews atangaza Wiki ya kusali kwa ajili ya Umoja wa Wakristo!

Kanisa Katoliki nchini New Zealand,limeandaa Wiki ya maombi kwa ajili ya Umoja wa Wakristo kuanzia tarehe 25-31 Mei 2020 kwa mujibu wa mwaliko wa Kardinali John Dew,Askofu Mkuu wa Wellington alioutoa kwa waamini wake.Wataongozwa na mada ile ile iliyoongoza kanisa zima mwezi Januari iliyopita "tulitendewa kwa ukarimu usioelezeka"kutoka katika kitabu cha Matendo ya Mitume 28,2.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Itakuwa Wiki ya Maombi kwa ajili ya Umoja wa Wakristo kwa namna ya pekee katika Kanisa la New Zealand ambalo linajiandaa na tukio hili kuanzia tarehe 25-31 Mei 2020. Janga la virusi vya corona kwa hakika linawafanya kusikika mambo mengi yanayoanzishwa ya kiroho. Anaamini hivyo Kardinali John Dew, Askofu Mkuu wa Wellington ambaye katika ujumbe wake kwa waamini anathibitisha kuwa “Mada ya Wiki kwa mwaka huu ni “walituonyesha ukarimu usi ona kifani” ( Mdo 28,2), ikiwa na maana ya kuelezea ukarimu walioupata Mtakatifu Paulo, na wenzake wakati walipofikia kisiwa cha Malta na chombo chao baada ya matatizo makubwa ya dhoruba wakiwa baharini na hatimaye kutua katika kisiwa hicho kwa mujibu wa simulizi nzima ya janga hilo la manusura.

Katika ujumbe wa Kardinali anaandika kuwa kuna mambo mengi ya kutafakari katika mada hiyo kwa mwanga wa uzoefu wa sasa wa virusi vya Covid-19”. Katika dharura ya kiafya, kwa hakika anasisitiz Kardina “ tunaombwa kuwa wakarimu na kubaki tumeungana kwa sababu kwa walio wengi katika janga hili ni sawa na manusura, na ukarimu usioelezeka ndiyo wa lazima ambao haujawahi kutokea awali”.

Aidha Askofu Mkuu wa Wellington anakumbusha kuwa “ katika mchakato wa safari ya karne nyingi, Makanisa ya Kikristo yamepitia katika ugumu na uhasama kwa kushambuliwa mmoja baada ya mwingine hususani wakati wa kushirikisha kwa mambo mengi kwa pamoja hasa katika kuwasaidia walio athirika zaidi. Kwa maana hii ndiyo anakazia  ukweli kwamba “ukarimu inaweza kutuunganisha kama wakristo”. Aidha ameongeza: "Ninawaalika ushikiri kwa namna moja au nyingine katika ‘wiki ya maombi kwa ajili ya umoja wa wakristo, na ikiwa mikotano ya moja kwa moja haiwezekani kwa sababu ya dharura ya kiafya basi jiunge katika mitandao kutafuta miongozo ya sala kwa sababu kila chochote kifanyikacho kwa ajili ya umoja, ndicho muhimu kinahesabiwa”, amehitimisha Kardinali Dews.

06 May 2020, 12:58