Tafuta

Mapandekezo ya Maaskofu Nchini Australia kwa Waziri Mkuu Bi Gladys Berejiklian katika matazamio ya ufunguzi tena wa makanisa kwa ajili ya ibada na huduma zote za kiroho. Mapandekezo ya Maaskofu Nchini Australia kwa Waziri Mkuu Bi Gladys Berejiklian katika matazamio ya ufunguzi tena wa makanisa kwa ajili ya ibada na huduma zote za kiroho. 

AUSTRALIA#conavirus:Mapendekezo ya maaskofu kufungua makanisa kwa hatua nne!

Maaskofu nchini Australia wametoa mapendekezo kwa Waziri Mkuu Gladys Berejiklian ya kufungua tena makanisa kwa hatua nne yaliyotiwa sahihi na Askofu Mkuu Anthony Fisher,maaskofu wengine 17 akiwemo askofu Mkuu Christopher Prowse wa Canberra-Goulburn na maaskofu wa Kanda ya New zealand.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Mapendekezo ya Maaskofu nchini Australia yametolewa kwa Waziri Mkuu Bi Gladys Berejiklian yaliyotiwa sahihi na Askofu Mkuu Anthony Fisher (OP) na maaskofu wengine 17 akiwemo askofu Mkuu Christopher Prowse wa Canberra-Goulburn na maaskofu wa Kanda ya New Zealand. “Kufunguliwa tena makanisa mwanzoni itakuwa ni hatua ya sala binafsi na maungamo kwa itifaki kali mahali hapo na itakuwa na maana sana kwa wengi katika jumuiya, kufariji na matumaini kwa walio na wasiwasi. Kutengwa kwa jamii na vizuizi vingine vimeleta hathari kubwa kisaikolojia na ya kiroho kwa watu”, kwa mujibu wa pendekezo la maaskofu waliyotumia Waziri Mkuu wa nchi.

Kwa upande wa pendekezo la Maaskofu wanaandika kuwa: Hatua ya pili inatazamia misa na huduma zinazopaswa kufanyika katika nafasi zilizo wazi mfano nje kama vile kwenye maeneo ya kuegesha magari na idadi ya wanaohudhuria iwe ni mdogo. Maaskofu wanapendekeza  kuwa hakuna vikapu vya kupitisha  au vitabu vya nyimbo; hakuna kupeana ishara ya amani kwa mikono au kushikana mikono… na Ushirika wa komunio utolewe na kupokelewa kwa usalama .

Hatua ya tatu, ya muda inayofanana na zile zilizotolewa inatazamia Misa na huduma kuhamishiwa ndani na hatua ya nne ni ile ya kurudia upya maisha ya kawaida kutoka katika janga la COVID-19.

Mwanzoni mwa misa yake iliyotangazwa moja kwa moja na mitandao  Jumapili, Askofu Mkuu Fisher alisema kuwa walifikiri wale wanaotazama walikuwa salama kwa kupakua programu ya ‘COVIDSafe’ na katika chapisho la mitandao ya kijamii, Askofu wa Kimaronite Antoine-Charbel Tarabay alisema kuwa amepakua programu hiyo na kuwataka kundi lake kufanya hivyo.

Maaskofu pia wametoa wito kwa waziri Mkuu Bi Berejiklian kuruhusu ubatizo na harusi zifanyike sanjari na vizuizi mahali pa mazishi na wahudumu hadi watu 10 tu. Pia wameomba idadi ya waombolezaji katika mazishi na huduma za makaburini ziongezeke.

04 May 2020, 12:46