ITALIA:Kard. De Donatis amshukuru Papa kwa barua aliyowatumia makuhani wa Roma!
Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican
Kardinali Angelo De Donatis, Makamu wa Papa wa Jimbo Kuu la Roma amemshukuru Papa Francisko kwa ajili ya Barua yake aliyowatumia makuhani wa Roma na kwamba ni zawadi yenye thamani ambayo inaongezwa katika utimilifu wa safari ya Pasaka. Barua hiyo ameiandika kuwatia moyo na kuwaalika katika tafakari ya kipindi hiki cha dharura ya kiafya kutokana na virusi vya corona.
Kwa mujibu wa Kardinali katika barua hiyo anaelezea shukrani zake za dhati kwa Papa na kwa niaba ya Baraza zima la ushauri wa kiaskofu na kwa makuhani wote wa Kanisa la Roma. “Tunakutakia mema. Tunao utumbuzi wa ushuhuda wako wa ubaba na ukaribu wako mbele ya mapadre wote na watu wa Mungu ambapo umejionesha katika kipindi hiki kigumu cha janga”. Kardinali anaandika.
Aidha amebainisha ni kwa jinsi gani wameweza kupata nguvu na msaada katika uweza wa sala zake na hata kwa ajili ya kumsikiliza Misa zake za kila siku na katekesi za kila wiki. “Maneno ya Papa Francisko anasisitiza Kardinali De Donatis, “yametoa mwangwi kwa mara nyingine katika dunia nzima kwa kurithisha matumaini na imani hata wale wasio waamini, licha “kelele kuu katika njia zetu na viwanja vyetu”
“Katika uongozi wako wa kibaba na udhihirisho wa Mfuasi wa Petro umetuimarisha imani yetu wakati wa kipindi hiki cha kuchanganyikiwa” anaandika tena Kardinali De Donatis na akimshukuru kwa ajili ya kupokea kwa imani hisia, mawazo na maombi ya mapadre wote na kuweza kuyawasilisha yote kwa Bwana!
Jitihada za makuhani wa Jimbo Kuu Roma anaandika siku zote zinabaki kujiruhusu “kuumbwa kwa upya na kuwashwa ndani ya mioyo kwa upole na huruma, kwa unyenyekevu na ukuu wa uvumilivu katika uhai wa utendaji na wa mshikamano, ujasiri, lakini pia kutorohusu sintofahamu na tofauti, kukataa, kinzani, wasiwasi na uzushi na badala yake kufungamana”. “Asante Papa kwa sababu unatualika tuangalie siku zijazo kwa ujasiri na mtazamo wa imani.” Amehitimisha Kardinali De Donatis barua yake kwa Papa.