Tafuta

Papa Francisko amewaandikia barua makuhani wa Roma Papa Francisko amewaandikia barua makuhani wa Roma 

Barua ya Papa Francisko kwa makuhani wa Roma:Sauti ya Bwana imejificha ndani ya janga !

Bwana yupo katikati ya watu wake.Ikiwa uwepo wake usioonekana na wa kimya,njia nyingine za kisasa zilizotukumba hazikutosheleza.Tuache sasa tuingie katika uwepo halisi wenye heshima na ambao siyo ya kuvamiwa,bali unatualika katika upya,unatufundisha tusiwe na hofu ya kukabiliana na hali halisi.Hata wakati mgumu hamkuacha zizi lenu.Haya na mengine yamo katika barua hii ya Papa Francisko kwa makuhani wa Roma.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Papa Francisko ameandika Barua kwa Makuhani kutokana na kutoweza kukutana nao wakati wa kipindi cha Pasaka hasa katika siku ya maadhimisho ya Misa ya Mafuta ya Krisma. Katika barua hiyo anasema kipindi kipya kinachoanza kinahitaji hekima na jitihada za muda mrefu za pamoja ili sadaka zilizofanyika hadi sasa zisiwe za bure. Katika kipindi cha janga, wengi wao wameshirishana na yeye kwa njia ya barua pepe au kupiga simu jambo ambalo amesema ni msingi katika hali hii ambayo haikutarajiwa na isiyo na uhakika. Hata hivyo amebainisha kwamba ushirikishwaji huo, umempatia fursa ya kujua taratibu kile ambacho walikuwa wanaishi. Ushirikishwaji huo umetajirisha sala zake na kwa maana nyingine anawashukuru kwa ushuhuda wao wa ujasiri na ukarimu ambao ameupokea kutoka kwao na kwamba amewaweka katika maombi kwa imani kwa Bwana ambaye daima anatoa msaada (Mt 14,31).

Licha ya kutengwa haukuzuia ushiriki wa matendo ya utume

Papa Francisko katika baru hiyo, amebainisha kuwa licha ya kukaa karantini  kijamii lakini haukuweza kuzuia jitihada kwa maana ya ushiriki wa muungno na shughuli za utume ambazo zimesaidisha kufanya upendo hasa kwa watu na jumuiya za wasio na fursa za kukaa karantini. Yeye binafsi amethibitisha ni kwa jinsi gani ameshuhudia mazungumzo ya dhati na ambayo kwa ulazima wa kuwa  mbali haukufanya watu walale uzingizi na kuzima utume. Kwa kupokea  taarifa zao na kubadilishana habari ndipo ameonelea kuwaandikia kwa sababu ya kutaka kuwa karibu nao ili kuwasindikiza, kushirikisha na kuimarishwa safari yao. Papaamesema matumaini yanategemea kutoka kwao na ulazima wa kuwa na msimano  thabiti  na uwajibikaji. Yaani matumaini yanayoshimiri na kuongeza jitihada katika makuhani na kwa  wengine ambao wao kama zawadi na zoezi vimetolewa ili kujenga ukawaida mpya ambao unatamaniwa.

Papa Francisko wakati wa kuandika barua hiyo amesema mbele yake anawatazama jumuiya ya kwanza  ya kitume ambayo licha ya kuishi kipindi kigumu, cha upwekwe, hofu na kisicho na uhakika waliweza kuvumilia. Kwa siku hamsini wakiwa wameganda ndani wamefunga milango kwa kusubiri  ili watangaziwe jambo ambalo lingebadili maisha yao daima. "Mitume walipokuwapo, milango imefungwa kwa hofu, akaja Yesu, akasimama katikati ya, akawaambia, “Amani iwe kwenu”. Naye akiisha kusema hayo, akawaonyesha mikono yake na ubavu wake. Basi wale wanafunzi wakafurahi walipomwona Bwana. Basi Yesu akawaambia tena, Amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi. Naye akiisha kusema hayo, akawavuvia, akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu. (Gv 20,19-22).

Kama jumuiya ya kikuhani hatukuweza kutoguswa na hali halisi hii

Hata sisi tuache tushangazwe, Papa Francisko ameandika, “Mitume walipokuwapo, milango imefungwa kwa hofu, (Yh 20,19) akinukuu hata Hati ya Gaudium et spes anasema isemayo : “Leo hii kama jana ni kuhisi kuwa furaha na matumaini, huzuni na uchungu wa watu wa leo hii na maskini hasa wale wote wanaoteseka, na ndiyo furaha na matumaini, huzuni  wa wafuasi wake …”(Gaudium et spes, 1). Je ni jinsi gani tulivyo na utambuzi wa hayo yote!  “Sisi sote tumepata kusikia kila siku idadi na asimilia zikipanda; tumeona nyuso na uchungu wa watu wetu. Kile kilichokuwa kinatokea hakikuwa mbali nasi, kwa mfano takwimu zilikuwa na majina, sura na historia za kushirikisha. Kama jumuiya ya kikuhani hatukuweza kutoguswa na hali halisi hii na hatukubaki kutazama kupitia dirishani";  Papa anaongeza "kwa kufunikwa na dhoruba chafu ninyi nyote mmejikita kuwepo na kusindikiza jumuiya zenu. Mmeweza kuona mbwa mwitu anafika na hamkukimbia kuacha zizi” (Yh 10,12-13).

Wote tulitubu kwa ajili ya ndugu zetu, wa karibu, marafiki, wanaparokia, waungamishi, ambao ni mifano ya imani yetu. Tumeona nyuso nyingi zilizokata tamaa kwa wale ambao wasingeweza kusema buriani kwa ndugu zao wapendwa wakati wa saa za mwisho. Tumeona mateso mengi kwa wahudumu wa afya, ambao kwa siku walikuwa wanachoka sana huku na wasiwasi mkubwa wa kutaka kutosheleza maombi. Papa Francisko amebainisha jinsi gani katika kipindi hiki, udhaifu wetu pia umeonekana. “Kama moto unavyojaribu kuchoma vyungu hata sisi tumepata majaribu”( Sir 27,5). Licha ya yote yaliyotokea, tumezidi kwa namna ya kuongeza jitihada zaidi za kitume katika hali hii. Kuishi na adui asiyejulikana, alituweka  bayana kuona ukosefu wa kukabiliana naye, kwa kile ambacho hatuwezi kutawala au kudhibiti na kama wote tulihisi kuchanganyikiwa, hofu na ukosefu wa usalama.  Vile vile tunaishi hata na hasira na ulazima ambao tunapaswa utusukume tusiangukie katika mikono ya ukosefu wa haki, ambao tayari unatuzunguka. Kama Dikodemu wakati wa usiku alivyoshangaa kutokana na maneno ya Yesu yasemayo “kwa maana upepo unavuma mahali unapotaka na kusikia, lakini hujuhi unatoka wapi na kwenda wapi” na ndipo tulijiuliza, “inawezekanaje kutokea hili; lakini Yesu alitujibu, “wewe ni mwalimu wa Israeli na hujuhi mambo hayo? (Yh 3,8-10).

Bwana hakuchagua au kutafuta hali halisi ili kuvunja maisha ya wanafunzi wake 

Bwana hakuchagua au kutafuta hali halisi ili kuvunja maisha ya wanafunzi wake. Hata hivyo tusingependelea lolote ambalo limetokea, lakini basi limetokea. Na kama wafuasi wa Emau labda tunaweza kuendelea kunung’unika njiani (Lk 24,13-21). Lakini Yeye alipojiwakilisha kwenye nyumba ya karamu kuu, milango ikiwa imefungwa na wao wakiwa  katikati ya upekwe, hofu na ukosefu wa usalama waliokuwa wanaishi, Bwana alikuwa na uwezo wa kubadili kila mantiki na kuwapa maana mpya ya historia na matukio. Kwa njia hiyo Papa Francisko amesisitiza “Kila kipindi kimepewa tangazo kwa ajili ya amani na hakuna wakati wowote usiokuwa wa neema. Uwepo wake katika hali kama hii ni kwa ajili ya wanafunzi wa jana na kama ilivyo leo,  siku mpya yenye uwezo wa kuwa na kila majadiliano ya kusimama kidete na siyo kukata tamaa ili kuweza kuzungusha zawadi zote za huduma ya jumuiya.

Papa Francisko akendeleza na barua yake amesema tunapaswa  tuseme kwa imani bila hofu kuwa “mahali palipo na dhambi iliyozidi, kuna neema nyingi zaidi (Rm 5,20).  Tusiogope majanga magumu ambayo tunaishi pale na kati yetu yupo Bwana. Mungu daima ametimiza miujiza kwa matunda yake mengi (Yh 15,5). Furaha ya Kristo inazaliwa katika uhakika huo. Katikati kinzani na kutoelewana ambayo kila siku tunakabiliana nayo hadi kufikia  kuwa na maneno mengi yanayosukana, sauti ya Bwana Mfufuka imejificha ndani humo ikisema “Amani kwenu”.  Inawatia moyo ili kuchukua Injili na kutafakari Yesu akiwa katikati ya watu na wakati akiwapokea na kuwakaribisha katika maisha watu kama wanavyojiwakilisha. Ishara zake zinatoa mwangwi wa wimbo mzuri wa Bikira Maria: “Amefanya nguvu kwa mkono wake; Amewatawanya walio na kiburi katika mawazo ya mioyo yao; Amewaangusha wakuu katika viti vyao vya enzi; Na wanyonge amewakweza. (Lk 1,51-52). Yeye mwenyewe alijikabidhi  mikono yake katika ubavu uliojeruhiwa kama njia ya ufufuko. Yeye hafichi majeraha yake; na zaidi alimwalika Thomasi aguse kwa mikono yake katika ubavu ulio jeruhiwa na ambao unaweza kuwa kisima cha maisha kamili.( Yh  20,27-29).

Ufufuko siyo tukio la kihistoria la wakati uliopita

Barua ya Papa inaendelea, "Basi Yesu akawaambia tena, Amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi. Naye akiisha kusema hayo, akawavuvia, akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu. (Yh 20,21-22). Kama jumuiya ya makuhani ambao wameitwa kutangaza na kutoa unabii wa wakati ujao, kuwa kama walinzi waingojeao asubuhi (Is 21,11), itakuwa ni jambo jipya na zaidi, au mbaya zaidi ya ukawaida. Ufufuko siyo tukio la kihistoria la wakati uliopita wa kukumbuka na kusheherekea. Ni zaidi ya hilo. Ni tangazo la wokovu wa kipindi kipya ambacho kinapaswa kuwa leo hii. “Tazama, nitatenda neno jipya; sasa litachipuka; je! Hamtalijua sasa? (Is 43,19); Papa ameongeza ni pale ambapo Bwana anaita kujenga. Imani inaturuhusu kuwa wa kweli na wabunifu zaidi, wenye uwezo wa kuacha mantiki za mazoea na kubadilisha au kuhifadhi; inatualika kujenga upya, na wakati mpya daima, yaani wakati wa Bwana. Ikiwa uwepo usioonekana, wa kimya, unasambaa, hata njia za kidijitali zimetuweka katika shida, ambayo imetukumba kwa maana hiyo tuache sasa tuingie katika uwepo halisi wenye heshima na ambao siyo wa kuvamiwa, bali unatualika katika upya, unatufundisha tusiwe na hofu ya kukabiliana na hali halisi.

Awe ndiye Bwana peke yake anayetufundisha kusindikiza, kutunza na kuwafunga majeraha ya watu wetu na sio kuwa na hofu bali ile shauku na mwamko wa kiinjili kwa kuona miujiza ya mikate (Mt 14,15-21); kuwa na ujasiri na ukarimu na  uwajibikaji wa Msamaria (Lk 10,33-35); kuwa na furaha na sherehe ya mchungaji baada ya kumpata kondoo wake( Lk 15,4-6); Mkumbatio wa upatanisho wa Baba anayejua msamaha (Lk 15,20); kuwa huruma, ukarimu na upole wa Maria wa Betania (Yh 12,1-3);  Kwa upendo, uvumilivu, na akili ya mitume wamisionari wa Bwana(Mt 10,16-23). Awe ni Bwana mwenye mikono iliyokuja kufariji  huzuni wetu na kutufariji kwa matumaini yetu huku akitoa msukumo wa kutafuta Ufalme wa Mungu mbali na kimbilio la mazoea. Tuache tushangazwe hata na watu wetu waamini na rahisi ambao mara nyingi wamejaribiwa sana lakini pia wametembelewa na Bwana”.

Kujikabidhi katika mikono ya Yesu kama sadaka takatifu udhaifu wa watu 

Kama makuhani, watoto na wajumbe wa makuhani wa watu, wanasubiri uwajibikaji kwa nyakati zijazo kwa maono kama ndugu. Papa Francisko amewaomba Makuhani hao waweke mikono yao katika mikono iliyokunjwa ya Yesu kama sadaka takatifu, ya udhaifu wa watu wao na ule wa ubinadamu wote. “Bwana ni yule anayetubadili, anayetuhudumia kama mkate, anachukua maisha yetu katika mikono yake na kutubariki, anaumega na kushirikisha na kuwapatia watu wake. Na kwa unyenyekevu tuache tufundishwe na maneno ya Paulo ili kupakwa mafuta mazuri yanayonukia katika kila kona ya miji yetu na kwa matumaini ya wengi: “Pande zote twadhikika, bali hatusongwi; twaona shaka, bali hatukati tamaa; twaudhiwa, bali hatuachwi; twatupwa chini, bali hatuangamizwi; siku zote twachukua katika mwili kuuawa kwake Yesu, ili uzima wa Yesu nao udhihirishwe katika miili yetu. (2 Cor 4,8-10)”.

Tushiriki na Yesu mateso yake na mateso yetu ili kwa njia ya haya na Yeye kwa nguvu ya ufufuko wa uhakika wa upendo wa Mungu wenye uwezo wa kutupeleka nje katika njia panda ili kushirikishana Habari Njema na maskini, kutangazia uhuru, kwa wafungwa na vipofu kuona, kutoa uhuru kwa waliokandamizwa na kutangazwa mwaka wa neema wa Bwana (Lk 4,18-19), Papa ameongeza kuandikia,  kwa furaha ya kwamba wote tunaweza kushiriki kwa uhai wote na hadhi yao wana wa Mungu aliye hai. Papa Francisko anaadika, “Yote hayo niliyofikiria na kusikia wakati wa kipindi chote cha janga, nimependa kushirikishana nanyi na ili yatusaidie katika safari ya kusifu Bwana na kwa huduma ya Ndugu. Ni matumaini kuwa sisi sote yatatusaidia kupenda na kuhudumia zaidi. Papa amehitimisha kwa kuwabariki na kuomba ulinzi wa Bikira Maria na wakati huo wasisahau kusali kwa ajili yake.

30 May 2020, 14:31